Mbuzi wa barafu wanaweza kuuzika Tanzania?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
1634535305423.jpeg

Mbuzi ni mnyama anae lika sana Tanzania, kwa sherehe za kifamilia au hata social gatherings mfano birthdays, kutoa mahari, ubatizo nk. Pamoja na hayo mbuzi choma ni kitafunwa pendwa kwa wanaokunywa pombe na wasiokunywa pia.

Wengi tunanunua mbuzi na kumtafuta mchinjaji. Anachinjwa mbuzi saa 11 alfajiri na saa mbili watu wakunywa supu ya utumbo.

Kuwa na machinjio ya mbuzi kwaajili ya kuuza walioganda. Wateja watapatikana kweli? Hapa tunaongelea mbuzi alietolewa utumbo, kichwa na miguu.

Kwa wale wanaotaka sehemu tu mguu pia unaweza kupatikana.
 
Kama kuna Need, basi utapata wateja (issue ni Need), sababu sioni kama wachinjaji ni tatizo, hivyo gharama za storage ni kuongeza gharama tu....

Kama unaweza kupata fresh bila tatizo why ununue refrigerated ?, Pia sidhani kama kuna butchery yoyote ambayo haina fridge / cold room
 
Jiulize tu kwa nini kuna neno mbuzi wa kafara na si kondoo wa kafara.simply nataka nitafte connection ya waganga kama kumi ili niwe nafanya hii biashara. Hasa kufungua ofisi karibu na kijiwe cha mganga
 
huko ni sawa na kuuza nyama tu. Tofauti kabisa na kuuza Mbuzi.

Biashara Ngumu hiyo
 
View attachment 1978107

Mbuzi ni mnyama anae lika sana Tanzania, kwa sherehe za kifamilia au hata social gatherings mfano birthdays, kutoa mahari, ubatizo nk. Pamoja na hayo mbuzi choma ni kitafunwa pendwa kwa wanaokunywa pombe na wasiokunywa pia.

Wengi tunanunua mbuzi na kumtafuta mchinjaji. Anachinjwa mbuzi saa 11 alfajiri na saa mbili watu wakunywa supu ya utumbo.

Kuwa na machinjio ya mbuzi kwaajili ya kuuza walioganda. Wateja watapatikana kweli? Hapa tunaongelea mbuzi alietolewa utumbo, kichwa na miguu.

Kwa wale wanaotaka sehemu tu mguu pia unaweza kupatikana.
Mama yangu mlezi amini , huo mradi ni mzuri na utatoboa tuliza akili kisha anza hata na mbuzi wawili .
Mimi eneo nilipo nauwazia huo mradi wa kununua mbuzi mmoja kila siku kisha kuchinjwa aliwe na aaishe changamoto yangu ni mda hio kazi.
Niko bize sana majukumu mengine na hapa kwangu NACHINGWEA, VIJANA NI WAVIVU .
NIMEJARIBU WASHAWISHI VIJANA AMBAO NI JOBLESS KUA TUANZE KAZI LAKINI NOW WATU WANNE WANANIKATALIA .
ILA NITAFANYA NIKIPATA KIJANA NA MZIGO AUZIE KWANGU
 
Kama una cold storage na unachinja halal...piece ina 16+ kg, cheki Bahrain, Kuwait na Qatar. Huko mbuzi waliogandishwa wana soko.
 
View attachment 1978107

Mbuzi ni mnyama anae lika sana Tanzania, kwa sherehe za kifamilia au hata social gatherings mfano birthdays, kutoa mahari, ubatizo nk. Pamoja na hayo mbuzi choma ni kitafunwa pendwa kwa wanaokunywa pombe na wasiokunywa pia.

Wengi tunanunua mbuzi na kumtafuta mchinjaji. Anachinjwa mbuzi saa 11 alfajiri na saa mbili watu wakunywa supu ya utumbo.

Kuwa na machinjio ya mbuzi kwaajili ya kuuza walioganda. Wateja watapatikana kweli? Hapa tunaongelea mbuzi alietolewa utumbo, kichwa na miguu.

Kwa wale wanaotaka sehemu tu mguu pia unaweza kupatikana.
Hapo ni ngumu kidogo,sababu nyie wachaga mnaweza kutuuzia hata frozen dog
 
Machinjio ya mbuzi yanayo chinja kwa request maalumu na delivery ya uhakika ni njema zaidi. Watanzania wengi hawaamini katika mabarafu ya chakula.
 
Mimi sikushauri mama ufanye huo mradi.

Watanzania wewe mwenyewe unatujua jinsi tulivyo na mambo ya ajabu!

Utaanza kuambiwa nyama haina ladha e.t.c
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom