MTUNZA AMANI
Senior Member
- Jun 2, 2012
- 187
- 21
Wadau, kitendo cha simba kuwasainisha mkataba wachezaji wa kigeni na kuwatimua hata kabla ya msimu kuisha kimeendelea, itakumbukwa baada ya kombe la Kagame kuna wachezaji wa kigeni walifukuzwa bila sababu za msingi, kama hiyo haitoshi leo tena Rage katangaza kumfukuza Daniel Akuffor ikiwa ni muda mfupi sana kasajiliwa kama ajira na hatimaye anafukuzwa tena bila sababu maalumu. Itakumbukwa miongoni mwa sababu ambazo zilimfanya Mbuyu Twite akatae kuchezea club ya Simba ni pamoja na Tabia ya simba kutowathamini wachezaji wa kigeni na kuwakatishia mikataba yao bila hata sababu za msingi. Itakumbukwa Simba imedhihirisha hilo,kwa anayetathimini kiwango na nafasi ya Akuffor mtakubaliana na mimi kuwa hakuna kosa la kisoka alilofanya.
Wadau nawasilisha hii siyo tabia nzuri kwa sababu unavomsajili mchezaji na kumfukuza unamharibia ajira yake na siyo haki kabisa.
Wadau nawasilisha hii siyo tabia nzuri kwa sababu unavomsajili mchezaji na kumfukuza unamharibia ajira yake na siyo haki kabisa.