Uchaguzi 2020 Mburahati, Dar: Yaliyojiri mkutano wa kampeni wa Dkt. Magufuli

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli leo anaendelea na kampeni zake katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo atanadi Sera na ilani za Chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba, 28, 2020.

Pia anatarajia kuwanadi wagombea Ubunge na udiwani majimbo ya Ubungo na Kibamba.

===



Dkt. Magufuli amekwishafika kwenye Mkutano kwa ajili ya kuanza kampeni, kwa sasa viongozi wa dini wamepewa nafasi ili kufungua mkutano kwa maombi.

Wagombea wa Ubunge wa majimbo ya Kibamba, Kinondoni na Ubungo wamepewa nafasi ya kuongea na Wananchi pamoja na kuomba kura na kuwaombea Wagombea wengine wa CCM.

Dkt. Magufuli anasema:

Kwanza nasema kwa dhati sijawahi kuona upendo mkubwa kama ambao mmenionesha ndugu zangu wa hapa Mburahati. Japo kuwa mvua inanyesha lakini mmekaa na kunisubiri hapa, kwa hili naomba niwaambie nina deni kubwa sana. Upendo huu mliouonyesha kwangu na kwa Wagombea wengine lazima tuulipe mara mia.

Nataka niwaahidi, na tulichelewa zamani, kwa sababu tatizo la Mahakama ya Ndizi halikushughulikiwa na mliowachagua zamani.

Kutokana na heshima mliyoionesha kwa wananchi kukaa na mvua, kwa mamlaka niliyopewa kama Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, itabaki chini ya wananchi wa hapo wanaofanya biashara.

Kama patakuwepo na taratibu nyingine, kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi namba 4 na 5 ya mwaka 1999, pamoja na Sheria ya Matumizi Bora ya Ardhi ya mwaka 2007, kuanzia leo wanaofanya kazi kwenye Mahakama ya Ndizi, hakuna kulipa ushuru, watalipa kitambulisho tu.

Kwa hiyo ukiwa na kitambulisho chako cha 20,000 nenda kafanye biashara na asitokee mtu wa kwenda kuwatoza hela wananchi wa Mahakama ya Mbuzi.

Mmenifurahisha mno, ninaweza kutoa ahadi ambazo nitashindwa kuzitekeleza!

Hata hapa tumezungukwa na barabara za lami, hii ni miradi ya kitaifa ambayo tuliamua kuifanya kwa nguvu, lakini si miradi ambayo ilitakiwa isimamiwe na madiwani pamoja na wabinge wenu, inawezekana pia ndio sababu mwaka huu, waliokuwa wabunge wa jimbo la Ubungo na Kibamba hawakuja kuomba ubunge maeneo haya, wamewakimbia kwa sababu mtawauliza "Mmetufanyia nini?" Kwa sababu Wamewadhulumu katika kipindi chote walichokuwa wabunge.

Mara nyingi niwekuwa nikiwahimiza Watanzania, kila mahali, msichanganye. Nimekuwa nikisema hivyo kwa sababu si kuwa ninawachukia watu wa vyama vya upinzani, la hasha. Ninawapenda sana. Lakini najua wengi wao hawapo kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi, isipokuwa maslahi yao binafsi. Na wapo pia wanaotumiwa kama vibaraka. Ninyi Wana-Ubungo mnafahamu, nisingependa kuwafafanulia zaidi.

Wakati tumeleta mradi mkubwa Dar es Salaam wa Bilion 660, waliokuwa wanatakiwa kugawana ule mradi, ni waheshimiwa wabunge na madiwani. Lakini wale wa vyama vingine hawakushiriki. Ndio maana wakati wa kugawana zile bilioni 660 wakakosa. Ndio maana utaiona Ubungo na Kibamba haina barabara nyingi za lami.

Wilaya ya Ubungo haina Makao Makuu ya Wilaya, lakini Kigamboni wana Makao Makuu, na nimeshaenda kufungua na nyumba zinajengwa. Ni kwasababu mbunge wa kule, Ndugulile, aliniomba. Lakini mbunge wa huku wala hata simjui sura yake, wala hata alikuja kuniona lini.

Nimeteseka mno kuisaidia Ubungo, sana! Ukitaka mradi huu, unakwamishwa. Hata mradi wa Mbezi Louis ulikwamishwa na hawa wa vyama. Wao hawataki maendeleo ya watu. Ninyi mlikuwa mashahidi, hata walipokuwa Bungeni walikuwa wanatoka, mara wanaziba midomo na plastiki. Sasa unapoziba midomo na plastiki utaomba saa ngapi maji ya Kibamba? Sasa naomba msiwarudishe ili watakaporudisha midomo yao, wawe wanakunywa maji yaliyoletwa na CCM.

Tunahitaji viwanda. Viwanda hivi vilijengwa tangu enzi za Nyerere - Kiwanda cha Urafiki, Kiwanda cha UFI, kiwanda cha Maziwa. Tunataka kutengeneza Tanzania ya Viwanda, ile miradi itakayosaidia ku 'boost' viwanda. Tuna bwawa la Mwl Nyerere, ambalo litakuwa linatoa umeme megawat 2,115; hili litasaidia kuja kuendesha viwanda vyetu ikiwamo hivi viwanda vya hapa Ubungo, ili watu wetu Watanzania wa hapa Dar es Salaam wapate ajira.

Hii hospitali ya wilaya ya Ubungo iliombwa siku ile kwenye sherehe tulipokuwa Airport, na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Wewe mpaka Mkuu wa Mkoa akaombe, mbunge alikuwa wapi kuomba hiyo zahanati na kituo cha afya? Tukaijenga kwa sababu Ubungo na Kibamba ilikuwa kama yatima. Msiendelee kuwa kama yatima. Chagueni viongozi watakaowawakilisha.

Sijawahi kuhutubia mkutano mkubwa namna hii mvua ikiwa inanyesha. Na maji ni baraka.

Tunajenga interchange nyingine Dar es Salaam, au flyover katika miaka inayokuja, zaidi ya 10. Lakini bado mtu anaweza akasema haya yote ni bure. Ni kawaida, shukrani ya punda ni mateke. Unaweza ukambeba mtu ukamvusha kwenye mto, akishavuka ng'ambo atasema mgongo wako una jasho. Ndiyo shukrani ya punda. Unaweza mama kuwa na mume wako ukamtunza miaka karibu 10 ukamzalia na watoto, unamtandikia kitanda, mambo yote unampa ya chakula na ugali, inafika wakati anasema “wewe mama umepitwa na wakati” Na ndio maana hata sisi tunajenga hizo barabara kwa ajili ya kurahisisha usafiri.

Niwaombe Watanzania, tusije tukatenganishwa kwa sababu ya uchaguzi. Bado kuna maisha baada ya uchaguzi. Na niwaombe wanasiasa, wasitumie siasa kama kichaka cha kutugombanisha. Kwa sababu wao watakimbia, tutakaobaki kuumizana ni sisi.

Kule bungeni kuna baadhi ya wabunge wa vyama fulani walikimbia bunge wakati wa bajeti. Badala ya kukaa na kupanga bajeti na kupanga mipango ya kuwahudumia watu waliondoka. Wao kwao maisha ni muhimu zaidi kuliko maisha ya wapiga kura wao. Jamani, hamuelewi tu ndugu zangu wa Ubungo? Kuongoza panahitaji upendo wa kweli.
 
Hiyo kampeni imepata "laana" ya mvua inayonyesha mfululizo siku ya Leo......

Kama alivyowaambia wahanga wa tetemeko kule Bukoba, kuwa serikali yake haijaleta tetemeko........

Awe mpole tu kwa kuwa mvua hii inayoendelea hadi hivi sasa, kwa kuwa nayo haijaletwa na CHADEMA!
 
Hiyo kampeni imepata "laana" ya mvua inayonyesha mfululizo siku ya Leo......

Kama alivyowaanbia wahanga wa tetemeko kule Bukoba, kuwa serikali yake haijaleta tetemeko........

Awe mpole tu kwa mvua hi inayoendelea hadi hivi sasa, kwa kuwa nayo haijaletwa na CHADEMA!
Kwa Lissu watu walivumilia mvua tuone na kwa dikteta kama watavumilia
 
Leo atahutubia
🐸
🐸
🐸
 
Huko angeachana nako tuu ..kuna watu wasomi ,waelewa wame survive kwenye economic hardship miaka mitano tayari wanajua nani wata munyima kura...labda ayende vijijini kama Kapwili -Kyela.
 
Hiyo kampeni imepata "laana" ya mvua inayonyesha mfululizo siku ya Leo......

Kama alivyowaanbia wahanga wa tetemeko kule Bukoba, kuwa serikali yake haijaleta tetemeko........

Awe mpole tu kwa mvua hi inayoendelea hadi hivi sasa, kwa kuwa nayo haijaletwa na CHADEMA!
Laana au baraka ndugu. Joto lilikuwa linatuua. Tumshukuru mungu kwa neema hii. Nipo kioski Ya jirani nakunywa soda. Kweli watu wameamua kwani hawakimbii mvua hii kali.
 
Ee, Mungu Baba, tunakuomba Mh. JPM kipenzi cha watanzania wachapa kazi ashinde kwa kishindo, 98.3% zinatosha tu Baba.

Leo binadamu wenzetu wa Uingereza wametangaziwa "karantini" nyingine mpya maana ugonjwa wa corona umeongeza speed hadi 200 km/h kwenye kona, na hapa Tanzania kuna mgombea ambaye kila kitu anacopy na kupaste kutoka kwao, Mungu baba ukimpitisha ndio hivyo basi tunafungiwa ndani kwa matakwa ya mabwana zake akina Amstredam.

Ameen!
 
Back
Top Bottom