Mbunifu wa Nembo ya Taifa anaishi maisha duni sana

Serikali inapaswa kumsaidia mzee huyu.
Itamsaidia vipi wakati hakujitokeza?
Alafu usikute yeye alichora wazo lilofanyiwa kazi na wengine.
Anyway kama amebainika yupo ni wajibu wa mamlaka husika kubaini ushiriki wake ili maamuzi yafanywe.
Kwa sasa ni kumsaidia kurejesha afya yake,makazi,chakula na mavazi mambo mengine yatafuata.
Kama kweli ni yeye aliyebuni National log ni jambo Jema sana.
Uhuru na Umoja ni nguzo ya Amani,upendo na mshikamano wa Taifa letu.
Hekima na Uzalendo wake yapasa kuuenzi walau kwa kumsaidia katika kipindi hiki kigumu anachopitia.
 
Maisha hayana usawa
Mkuu Nyagei,maisha yako poa tu,tatizo ni Serikali ya Tanzania & Watanzania ndio hatuna usawa. Moja ya sababu ya kutokuendelea kwa nchi hii ni pamoja na vilio,majonzi & masononeko ya watu kama hawa yanayotengeneza laana na kuweka wingu la kuzuia baraka za Mwenyezi Mungu kutufikia.
 
Hivi yule aliyeshinda shindano la jina la chi yetu tunalotumia leo "Tanzania" alilipwa miadi aliyoahidiwa na serikali? Je yule "Lutenant" aliyepandisha mwenge wa kwanza wa uhuru juu ya mlima k/njaro, alikufa akiishi maisha gani? Yule mnyamwezi Mwinamila, aliyelienzi taifa kwa kiyamwezi alikufa na kuacha ukwasi kiasi gani? Enhe na yule mzee Moris na ngoma zake7, alienziwaje kabla "hajavuta"? Na bi kidude gwiji wa taarabu asilia, amekufa akimiliki nini?
 
Mkuu Nyagei,maisha yako poa tu,tatizo ni Serikali ya Tanzania & Watanzania ndio hatuna usawa. Moja ya sababu ya kutokuendelea kwa nchi hii ni pamoja na vilio,majonzi & masononeko ya watu kama hawa yanayotengeneza laana na kuweka wingu la kuzuia baraka za Mwenyezi Mungu kutufikia.
Sivyo Mkuu,tatizo ni wasanii wa Sanaa za uchoraji na ubunifu kushindwa either kutambuana au kupuuza michango ya wakongwe wao.
Jiulize kwanini wasanaa wa uchoraji wameshindwa kufikisha kilio cha Mzee huyo hadi ITV wameibua kilio hiki.
Hapa pana ubinafsi na uchoyo wa mafanikio miongoni mwa wasanii uchoraji na ubunifu.
Kuilaumu Serikali na kuibambikia laana si sawa Mkuu.
 
Nikiingia akilini mwake huyu mzee namuona kabisa jinsi anavyojilaumu kuiremba vile hiyo nembo...yaani kwa sasa anajisemea ''bora ningeyachora manyoka,mavyura,mijusi alafau niwakabidhi,... wakiniuliza nini hii? Nawaambia Tunu za Taifa...."
Shubaaamit!
 
Maisha ni mechi isiyo na sare uyashinde au yakushinde, hivyo unapocheza mchezo huo ni lazima uwe makini, unatakiwa ushinde ukiwa bado kijana mechi hiyo sio mchezo fainali iko uzeeni.
 
kwani huyo mzee ndiye JEREMIA WISDOM KABATI? ALIYE BUNI HIYO NEMBO MWAKA 1961 HUKO BWIRU ?
 
1964 wakati akipewa tender alilipwa pesa yake yote hadai hata senti kwahivyo Jamhuri haina deni nae. Hakufanya iyo kazi Bure yaani kwa Uzalendo
Una uhakika alipewa tender na kulipwa? Au aliteuliwa na kipewa zawadi?
 
1964 wakati akipewa tender alilipwa pesa yake yote hadai hata senti kwahivyo Jamhuri haina deni nae. Hakufanya iyo kazi Bure yaani kwa Uzalendo
Mimi nilitaka kuuliza, kwani hakulipwa?

Au walitaka ajengewe nyumba na kupea pensheni ya uzeeni?

Mngeambiwa mlipie kodi gharama hizo mngekubali?
 
Mwalimu wa nyerere mwenyewe kafa bila kulipwa haki zake.Tz ni shida sometime.

Haki gani wakat Kajengewa Hekalu la Ma Million kwao Butiama?,

Nyerere Mwenyewe ndie Muasisi wa hako ka Mchezo ka kudhulumu wenzie hela za Wazee wa Jumuia ya EA alijifanya kwenda kupigania Vita ya Kagera wakat wenzetu walilipwa hela zao
 
Nimeiona hiyo taarifa ya habari.

Godfrey Monyo wa ITV is such a horrendous journalist.

Eti anamuuliza babu "wewe ndio umechora nembo ya Taifa"? Babu nae akaona ulaji huu umejileta, akaitikia NDIO!

Nani alikwambia uchore, akajibu NYERERE!

Godfrey Monyo, what is your independent source? Unajuaje kama babu haongopi?

Hakuna profession mbovu nchi hii kama the press.

who designed tanzania coat of arms - Google Search
 
Back
Top Bottom