Mbunifu wa Nembo ya Taifa anaishi maisha duni sana

Hakulipwa Kwa kazi yake ya ubunifu? Kama ndiyo
Anataka nini Leo? Hakujipanga enzi za ujana wake asilie lie kutaka msaada Kwa kigezo cha kubuni nembo ya taifa..........

Kuna watu wengi wameifanyia makubwa hii nchi na wana hali mbaya je wote walalamike/kuhitaji msaada wa serikali?
Ungefutilia ujue kama alilipwa au hakullipwa...na kwa kazi kubwa kama hiyo angetakiwa kulipwa maisha yake yote na kizazi chake...kama hiyo kazi yake itaendelea kutumika...ITV wafutilie vizuri watuletee muuendelezo wa hii habari..pia ningefurahi ITV wangefuatilia na mtu aliyebuni jina la Tanzania hali yake ikoje..yupo wapi kwa sasa...na alifanyiwa nini na serikali yake kwa kazi ya kubwa aliyofanya..
 
Halagu leo hii wakisimama jukwaani wanataka watu tuwe wazalendo.bora brother mwigulu yeye kakwepa lawama kwa kuuamua kutembea na bendera shingoni .

Muheshimiwa najua umo humu jf,so isiwe taaaabu kwa nilichokiandika hapo juuu.just joking.maana siku hizi hamkawii kutoa hadharani kweupeee kitu cha Ak47.
 
Ujumbe umefika..kina mzee Moris Nyunyusa licha ya kuwa kipofu na kufanikiwa kupiga ngoma zaidi ya kumi na mbili ambazo zinatumika mpaka leo radio Tanzania hawakusaidiwa mpaka wanaingia kaburini! Nchi hii usipokuwa na maarifa ya kutoka pindi ukiwa kijana imekula kwako! Inasikitisha sana ila ndio maisha!
 
Wewe ndio wa kutumia akili vizuri. Kwani huyo alikua kiongozi wa kitaifa? Hao wakitaifa wanalipiwa kwa mujibu wa katiba.....yeye unataka alipwe nini na kwa utaratibu upi. Tuseme tu anaomba msaada. Msitumie kigezo cha kubuni nembo.
Kuna watu wengi sana nchi hii wameifanyia mambo kubwa nao wasemeje? Mfano kuna yule aliyebuni jina Tanzania nayeye tumpe nini?
Ndugu...huyu Mzee angetakiwa aenziwe sana..kama ni kwa nchi za wenzetu..angetakiwa ale matunda ya kazi ya mikono yake yeye na kizazi chake...labda mwisho uwe siku ambayo serikali itaacha kuitumia hiyo nembo.ni jambo la aibu kubwa kwa mtu aliyefanya kazi kubwa kama hiyo kuishi kwenye maisha duni kama Yale.ninawapongeza ITV na mwandishi aliyemuibui huyu Mzee huko alikokuwa...kongole kwenu..wito ni kwa serikali yetu kuchukuwa atua za haraka kumsaidia huyu Mzee..na wengine wote waliofanya mambo yaliyoweka alama katika nchi yetu..
 
Mchoraji wa Nembo ya Taifa maarufu kama Adam na Hawa, Mzee Francis Maige Ngosha anaishi maisha duni yasiyoendana na mchango wake aliotoa kwa taifa kabla na baada ya kupata uhuru ambapo anaishi kwa kuomba msaada wa kujikimu.

View attachment 513421

Mzee huyu anaishi Buguruni kama sikusika vibaya.

Chanzo: ITV

Hongereni sana ITV maana hii ndio moja ya kazi za vyombo vya habari.
Ukiona wanaopata nafasi wanaiba, kwa upande mwingine huwa wanaona mbali sana
 
Habari kama hizi hazipendwi kabisa na bwana yule!
Me nashangaa unavomuhusisha sizonje na habari kama hii kama vire kaanza ongoza toka uhuru, jamani sometym tuwe na moral justice usikute hajui hata yeye kitu kama hiki!..
Huyo mzee tuanze uliza alilipwa ama hakulipwa na je alifanya kwa msaada ama alidhulumiwa usikute alilipwa akajikuta mr. nice then anataka huruma ya jamii saa hivi!!..

NB: Nachukia sana kumsaidia mtu halafu nije kuta ameuchezea msaada wangu.
 
Wanaotumia hiyo ngao ya taifa wanalindwa na kuishi maisha ya pepo hapa duniani. Lakini mchoraji anafadhiliwa ktk kibanda cha kupanga bila chochote. Hii ndiyo dunia na inanikumbusha kisa cha Morice Nyunyusa na alivyomalizia
Umemsahau na Capt. Nyirenda aliepandisha bendera mlima Kilimanjaro... Alikufa alikufa kama mtu ambae hajawahi kufanya chochote, matibabu tu ilikuwa ni shida.
 
Back
Top Bottom