Mbunifu wa Nembo ya Taifa anaishi maisha duni sana

Wanaotumia hiyo ngao ya taifa wanalindwa na kuishi maisha ya pepo hapa duniani. Lakini mchoraji anafadhiliwa ktk kibanda cha kupanga bila chochote. Hii ndiyo dunia na inanikumbusha kisa cha Morice Nyunyusa na alivyomalizia
 
1964 wakati akipewa tender alilipwa pesa yake yote hadai hata senti kwahivyo Jamhuri haina deni nae. Hakufanya iyo kazi Bure yaani kwa Uzalendo
Sababu Kipindi cha ujamaa watu walikuwa wanafanya kazi kwa uzalendo ndio maana akina mzee mwamwindi waliambiwa walime mashamba za vijiji na kuacha mashamba zao ndio sababu iliyompelekea amuue RC ..

Uzalendo uzalendo ilikuwa kauli mbiu yao ,utajiri dhambi
 
Akifa ndio tutamkumbuka
M
IMG-20170522-WA0006.jpg

Tatizo serikal yetu vitu vya msingi huvipa kisogo. Sijui huwa wanafikiria nn?
 
Hakulipwa Kwa kazi yake ya ubunifu? Kama ndiyo
Anataka nini Leo? Hakujipanga enzi za ujana wake asilie lie kutaka msaada Kwa kigezo cha kubuni nembo ya taifa..........

Kuna watu wengi wameifanyia makubwa hii nchi na wana hali mbaya je wote walalamike/kuhitaji msaada wa serikali?
 
[HASHTAG]#Habari[/HASHTAG]:Mchoraji wa Nembo ya Taifa maarufu kama Adam na Hawa, Mzee Francis Maige Ngosha anaishi maisha duni yasiyoendana na mchango wake aliotoa kwa taifa kabla na baada ya kupata uhuru ambapo anaishi kwa kuomba msaada wa kujikimu.

Chanzo:ITV
Ajiongeze. Kwa vile kabuni nembo tu anategemewa imlishe maisha? Nadhani alitakiwa awe mbunifu zaidi na zaidi. Ndiyo maana wabunifu wote inabidi wawe wabunifu daima ili ubunifu wao uwalipe.
 
[HASHTAG]#Habari[/HASHTAG]:Mchoraji wa Nembo ya Taifa maarufu kama Adam na Hawa, Mzee Francis Maige Ngosha anaishi maisha duni yasiyoendana na mchango wake aliotoa kwa taifa kabla na baada ya kupata uhuru ambapo anaishi kwa kuomba msaada wa kujikimu.

Chanzo:ITV
Ndivyo wazalendo wanavyotakiwa kuishi chini ya "oyeee!"

Hivi mnadhani kwanini makao makuu ya nchi yamepelekwa kwa Matonya? Hamuelewi tu? Ncho Ombaomba huzaa ombaomba! Ujuzi wa kuomba omba unapatikana Dodoma pekee...

Bastola ya nini kama natania watani zangu jee?
 
Ajiongeze. Kwa vile kabuni nembo tu anategemewa imlishe maisha? Nadhani alitakiwa awe mbunifu zaidi na zaidi. Ndiyo maana wabunifu wote inabidi wawe wabunifu daima ili ubunifu wao uwalipe.
Mkuu, kumbe Nembo ya Taifa kumbe ni kitu kidogo eeh? Hata kama hawalipwi!! waendelee tu kubuni kibashite bashite labda!!! Hakuna hakimiliki wala haki bunifu hivi ingelikuwa yale mataifa tuyaitayo makubwa kauli yako ingekuwa sahihi angelikuwa masikini?
 
94fa81ef5ada97f56e30fac7fbcca1ee.jpg
[HASHTAG]#Habari[/HASHTAG]:Mchoraji wa Nembo ya Taifa maarufu kama Adam na Hawa Mzee Francis Maige Ngosha anaishi maisha duni yasiyoendana na mchango wake aliotoa kwa taifa kabla na baada ya kupata uhuru ambapo anaishi kwa kuomba msaada wa kujikimu.
 
Kwani hakulipwa? Au ulikua mkataba wa kudumu? Au alifanya bure msaada kwa taifa? Mi sielewi mjue....mi ni bepari
 
Salary slip, ni kweli kabisa. Maana nakumbuka hata yule Mzee Moses aliye piga ngoma za Kabla ya Taarifa ya habari pale Redio Tanzania alikufa akiwa masikini sana.
Sahihisho Mzee Morris Nyunyusa!! Usimsahau na John Komba!! Ndio utajua umaskini wa nchi hii ni wa makusudi kama sio wa kulaaniwa!!! Sijui ni zile nyumba, viwanda na mali walizodhulumu 1967 ndio vinawarudi watawala?
 
Yaani inatia huruma!
Nimeiona taarifa ya huyu mzee. Jambo hili ni gumu sana ila hata km alifuja mali ujanani bado taifa lazima limkumbuke hata kwa kumjengea nyumba tu.
Hii ni changamoto kwa ngazi zote za serikali hasa tukianza na mtaa.
 
Back
Top Bottom