Mbunifu wa Nembo ya Taifa anaishi maisha duni sana

wata muhimu kama hawa inabidi serikali iwaangalie na kuweka data base kwa historia ya nchi yetu
 
Naamini kabisa historia ya kweli ya nchi hii ni ile iliyoandikwa kabla na wakati wa ukoloni,
Kuibuka kwa huyu mzee inaonekana kabisa historia ya nchi hii baada ya Uhuru eidha haijulikani vizuri au kuna mengi yalipindishwa kwa maslahi ya kisiasa. Tusubiri majibu ya serikali juu ya nembo ya Taifa na mchoraji wake.
Mimi nilikutana na hii huko fesibukuni nilipokuwa namtafuta mwandani.Ninashindwa kuelewa nani ni nani.
 

Attachments

  • FB_IMG_1495619209798.jpeg
    FB_IMG_1495619209798.jpeg
    29 KB · Views: 33
Mkuu haki miliki kwa product moja tu haikutoi. Inabidi ubuni products nyingi sana na uwe unazibadili badili kulingana na mahitaji ya wateja. Wateja tunabadilika sana kila siku. Leo unapenda design hii kesho huipendi. Mfano mzuri angalia design za simu zinavyobadilika kila siku. Hata viwanda vikubwa kama Cocacola wamebadili mtindo wa biashara na products. leo wana products zaidi ya zile traditional walizoanza nazo. Mtindo wa kuziuza pia wamebadili. Hebu iprice hiyo nembo. Ungekuwa wewe ungempa shilingi ngapi kwa kuown hiyo nembo kama angekuwa na haki miliki?
Kitanzania ni kweli haki miliki moja haikutoi!! Mkuu NEMBO ya Taifa haifananishwi na vitu vya kijinga
 
Serikali msaidieni huyu mzee ni muhimu sana kwa historia ya taifa letu haipendezi kuwatelekeza na ukizingatia hivi sasa afya yake si nzuri na uzee kwa kweli anahitaji msaada.


Tuanze mimi na wewe, huko ulikotaja sidhani kama kuna msaada wowote
 
Vijana wengi wanaojirusha leo hawajajiandaa na maisha ya uzeeni na inatakiwa wachukue funzo hapo.

Kama wanataka kuishi mpaka uzeeni at all, maana wengine hata huo uzee hawataki wanataka waishi maisha mazuri na mafupi,
 
MZEE HUYU TUACHE STORI ANAPASWA KUTAZAMWA UPYA NA SERIKALI
Wako waliokuwa wanaona mada hii ni upuuzi mtupu hatimae baada ya kelele wamejitokeza rasmi sasa na ameshakuwa "mzee wetu" matibabu yanaendelea ni jambo la kushukuru. Ila inasaidia kuwa sasa Wazalendo na wala nchi tunajitambulisha kwa namna zetu
 
Husika na kichwa cha habari hapo juu,Mzee Francis Ngosha ndie mchoraji na mbunifu wa nembo ya taifa hivi sasa anaishi maisha ya kichokoraa huko Buguruni jijini Dar es salaam. Kibanda anachoishi ni cha hovyo sana ni kama banda la kuku limezungushwa na Bati juu mpaka chini.

Serikali msaidieni huyu mzee ni muhimu sana kwa historia ya taifa letu haipendezi kuwatelekeza na ukizingatia hivi sasa afya yake si nzuri na uzee kwa kweli anahitaji msaada.

img_6907-jpg.513421


Chanzo: Itv habari.
Hatimaye serikali yachukua hatua
 
Ni jambo jema la kupongezwa na Kila raia mwema.
Hongereni Sana.
Wengi wamelitendea taifa hili haki, lakini wame disappear katika mazingira yenye utata
 
Back
Top Bottom