mbunge Yono Kevela yuko sawa au amekose?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
jamani hivi alivyofanya mbunge huyu kuwahusia wanafuni kusoma kwa bidii ili wapate hayo aliowaeleza ni sawa au amekosea?

na kustaarabika ni kuoa mzungu?
hivi ndio watanzania tunavyofikiri? au ni mbunge huyu tu ?


Mbunge aingia darasani, kufundisha



na George Maziku, Njombe



MBUNGE wa Njombe Magharibi, Yono Kevela, amelazimika kuingia darasani kufundisha kama njia ya kuhamasisha watoto kupenda elimu.
Tukio hilo la kuvutia lilitokea katikati ya wiki hii, wakati mbunge huyo alipokuwa katika ziara ya kukagua shughuli za maendeleo na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Mbunge huyo aliingia darasani na kufundisha somo la hesabu kwa wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Mayale, iliyopo Kijiji cha Mayale, Kata ya Wanging’ombe, jimboni humo.

Yono alitumia karibu dakika 30 kufundisha hesabu za maumbo, huku akiwapa wanafunzi nafasi ya kumuuliza maswali mbalimbali yanayohusu somo la hesabu.

Mbunge huyo alifika shuleni hapo majira ya mchana na kwenda moja kwa moja darasani na kumwomba mwalimu aliyekuwa akiwafundisha, ampatie nafasi ya kuonyesha utaalamu wake katika somo hilo.

Mwalimu huyo, Isack Joram ambaye ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, alimruhusu mbunge Yono kuwafundisha wanafunzi.

Baadaye mbunge huyo alipata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo, na kuwasihi kuongeza bidii katika masomo, ili baadaye waishi maisha mazuri.

“Someni kwa bidii mpaka mfike sekondari na chuo kikuu, ili baadaye mgombee ubunge kama mimi, mpate ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa, uwaziri, na hata urais wa Tanzania kama Kikwete.

“Mkisoma mtapata kazi nzuri, mtanunua gari nzuri kama yangu, mtajenga nyumba nzuri, mtapata fedha za kuwatunza wazazi wenu, mtapanda ndege na kusafiri mpaka Ulaya, Marekani na kuoa au kuolewa na Wazungu alihamasisha na kushauri mbunge huyo.

Yono alisema hakuna lisilowezekana hapa duniani, lazima mtu asome kwa bidii na kuhitimu vema masomo yake, ndipo atafanikiwa kimaisha.

Pia aliwasihi wanafunzi hao kujihadhari na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) na ugonjwa wa ukimwi, ili waweze kufikia ndoto zao za kimaisha.

Baada ya kufundisha, mbunge huyo alitoa msaada wa mpira mmoja wa miguu na kuahidi kuchangia ujenzi wa madarasa ya shule hiyo unaotegemewa kuanza hivi karibuni.

Shule ya Msingi Mayale ilianzishwa mwaka 1972, lakini haikuwa na maendeleo mazuri kitaaluma, mpaka mwaka jana ilipofaulisha wanafunzi 23 kati ya 28 waliofanya mtihani wa mwisho.

Kwa sasa shule hiyo ina wanafunzi 294 na walimu saba, ambao hawatoshelezi mahitaji halisi ya shule hiyo.


source tanzania daima
 
KWA MAWAZO HAYA NADHANI HATA KAMPUNI AMBAYO ILIKUWA INAHUSIKA KUVUTA MAGARI YA WATU HUKU WENYEWE HAWAPO UKIRUDI UNATAHAMAKI GARI HALIPO ITAKUWA NI YA HUYU HUYU....!
LAKINI AMESEMA YALIYOUJAZA MOYO WAKE NA KUWAKILISHA KUNDI LA 'MATAWI YA JUU'.........SASA NAJIBU SWALI......AMEKOSEA....!
 
Mbunge ameteleza kidogo,

kwa sasa hatuhitaji wanasiasa. Tunahitaji zaidi wataalamu kwenye science and technology.

Yeye kama mwalimu wa hesabu nadhani alikuwa kwenye nafasi nzuri kuwaasa waweke bidii kwenye mrengo wa science na awashawishi wajiandae wasome uhandisi, udaktari, uchumi n.k.

Hawa watoto wanahitaji msingi imara na wa kweli na si bla bla za kusoma eti uje kuoa mzungu.

Wanatakiwa waandaliwe vizuri kulijenga taifa na si kama wanasiasa wa sasa wanavyolibomoa kwa kasi ya ajabu.
 
Populism and colloquism at its best.

Mbunge kafanya vizuri kutaka kuwa involved na elimu ya constituency yake, lakini amekosea jinsi alivyofanya (inaonekana spontaneous) halafu hatujui kama ana taaluma ya ualimu (wanasiasa kuvamia kila kitu) halafu hiyo quote kama ni direct quote kama ilivyoonyeshwa imepinda!

Angenifurahisha zaidi kama angesponsor motion bungeni kuboresha elimu.Instead anataka kampeni za populism kwa taaluma ambayo obviously hana.
 
Only in TANZANIA after three years of being in office bado mtu anashukuru wananchi kwa kumchagua! baada ya kuwaambia katika hiyo miaka miatatu kawafanyia nini!

Back to the argument nadhani ni kitu kizuri kuwaencourage wanafunzi especially wa rika kama la hao. Iam speaking this from experience ya kusomea kijijini, kiongozi hata katibu wa CCM alikuwa akiwatembelea shuleni inakuwa ni inspiration kubwa sana. Tunaweza tusiwe na mtizamo mmoja, lakini to me, nikijiweka kwenye viatu vya hao wanafunzi...Nakumbuka mbaaaali sana.

Sema tuu viongozi wa siku hizi sio model tena kama tulivyowategemea kwa sababu ya ufisadi na uzembe. Otherwise what he did was good. na kuoa mzungu? well ni ile ile kasumba ambayo imejengeka miaka mingi sana kwamba mzungu ni SI unit ya mafanikio na kila kitu kizuri. Whether it is right or wrong, I cant tell! Perhaps ask Nyani Ngabu kama mzungu ni SU unit ya kila kitu bora!
 
Only in TANZANIA after three years of being in office bado mtu anashukuru wananchi kwa kumchagua! baada ya kuwaambia katika hiyo miaka miatatu kawafanyia nini!

Back to the argument nadhani ni kitu kizuri kuwaencourage wanafunzi especially wa rika kama la hao. Iam speaking this from experience ya kusomea kijijini, kiongozi hata katibu wa CCM alikuwa akiwatembelea shuleni inakuwa ni inspiration kubwa sana. Tunaweza tusiwe na mtizamo mmoja, lakini to me, nikijiweka kwenye viatu vya hao wanafunzi...Nakumbuka mbaaaali sana.

Sema tuu viongozi wa siku hizi sio model tena kama tulivyowategemea kwa sababu ya ufisadi na uzembe. Otherwise what he did was good. na kuoa mzungu? well ni ile ile kasumba ambayo imejengeka miaka mingi sana kwamba mzungu ni SI unit ya mafanikio na kila kitu kizuri. Whether it is right or wrong, I cant tell! Perhaps ask Nyani Ngabu kama mzungu ni SU unit ya kila kitu bora!


kwa nn asiwaencourage kutumikia taifa lao kwa uadilifu na moyo wa kuleta mabadiliko kwa jamii kubwa.

kwa nn asiwahamasishe kukataa kutoa au kupokea rushwa

kwa nn asiwagusie kuhusu kulinda rasilimali za nchi yetu na si kuzigawa kwa wageni huku wananchi wakiumia?

kwa nn azungumzie ubinafsi ? hivi ni sawa kwa kiongozi mbunge kuzungumzia haya kwa wanafunzi amabo ndio warithi wa taifa hili?

hii haipelekei kwa wanafunzi kuwa na uroho wa mali kuwa watasoma ili wafikie malengo hayo ambayo si malengo muhimu kwa ustawi wa taifa ukilinganisha na nilioyataja?
 
Sijawai kuona mbunge mjinga kama huyu. Sialipendekeza watu wenye HIV wawekwe alama kwenye paji la uso ili wasiambukize watu wengine. Hana concept ya haki za bi Adam... hana akili. Tena sijui alisoma wapi. Mtu mpuuzi kweli. Sasa kuoa wazungu na kuolewa na wazungu ndio maisha ambayo watanzania wanatakiwa wayatafute. Viongozi wajinga kama hawa sijui wanatokaga wapi!??!?!
 
All in all
Ni CCM pekee ambapo unaweza ukakuta viongozi aina hii
BINGO
 
Ukitaka kujua kwamba wabunge wa CCM wananunua Ubunge basi huyu ni mmoja wao.Hivi nyie wabunge mko serious au mnafanya mzaha.Tangu Dec,2005 eti unakwenda jimboni kwako kuwashukuru wapiga kura wako,hivi hamuoni aibu.Mbunge huyu hana maadili ya uongozi.LAKINI NADHANI ILIKUA NI BORA ZAIDI TUKAPATA CV YAKE.Hivi inawezekana Prof.akaenda shule ya msingi akafundisha na wanafunzi wakamuelewa au itakua kichekesho,yaani mbunge umekwenda kufundisha darasa la saba P/S,hii hainiingii kichwani.It shows how you are not serious.

Jamani mbona alichozungumza huyu Mbunge mimi kinanichanganya au mnamsingizia?Naamini hata mtendaji wa kijiji mwenye maadili ya uongozi hawezi kuongea utumbo kama huu.Nadhani miongoni mwa wabunge ambao ni vilaza na husubilia tu posho za wabunge basi huyu ni mmoja wao.Huyu mbunge huwa analala bungeni.Nchi inasisitiza watu wasome ili waweze kujitegemea na kuanzisha miradi yao wenyewe.We Yono hivi kwa akili yako umeona uwazili ni "deal"kina meghji wako wapi,lowasa,dialo hebu acha utoto.Hivi kweli wewe Yono unaliandaa taifa la kesho kwa fikra hizi potofu,hapa umejikashifu mwenyewe kabla ya kukashifiwa kwamba huu ubunge wako ni wa kununua.

NIMALIZE KWA KUSEMA AMEKOSEA JAMANI TENA KAMA NI KUMPA MAKSI KWA KUA NI MBUNGE NAMPA 0.5 KWA MIA.AMEKOSEA.
 
Sijawai kuona mbunge mjinga kama huyu. Sialipendekeza watu wenye HIV wawekwe alama kwenye paji la uso ili wasiambukize watu wengine. Hana concept ya haki za bi Adam... hana akili. Tena sijui alisoma wapi. Mtu mpuuzi kweli. Sasa kuoa wazungu na kuolewa na wazungu ndio maisha ambayo watanzania wanatakiwa wayatafute. Viongozi wajinga kama hawa sijui wanatokaga wapi!??!?!

Mawazo yake ni sambamba na mwelekeo wa uongozi wa CCM - UBINAFSI MBELE. Hata angekua amesomea wapi, bado ubinafsi wake utamfanya aseme bila kuwajibika na huu ubinafsi ni kwa sababu amepigwa msasa wa CCM. Sikia Karamagi ama Lowasa wanavyojitetea kuhusu ufisadi, hawana tofauti na fikra za huyu mbunge.
 
Kwa Hili Tayari Amekosea,.......!kama Kuna Mengine Pamoja Na Mema Yake Yawekwe Jamvini Ili Justice Ichukue Nafasi Yake.....!
 
hatari kuhusisha maneno yake aliowaeleza wanafunzi ni sera au yanatokana na ccm, hii si kweli na kukionea chama cha mapinduzi.


si haki kusema kuwa yule padri aliewapeleka wafuasi wake porini ndio ukristo ulivyo, ile na akili yake na msimamo wake ambao wengi wengine wameuelezea kuwa mkuu alichemsha.

kosa au uzembe wa mtu ubakie wa mtu na hasa anapofanya kazi ambazo hawakilishi mtu au watu.

na hata hapa mtu akileta pumba kwa kuwa member wetu haimaanishi JF sio makini
 
kwa nn asiwaencourage kutumikia taifa lao kwa uadilifu na moyo wa kuleta mabadiliko kwa jamii kubwa.

kwa nn asiwahamasishe kukataa kutoa au kupokea rushwa

kwa nn asiwagusie kuhusu kulinda rasilimali za nchi yetu na si kuzigawa kwa wageni huku wananchi wakiumia?

kwa nn azungumzie ubinafsi ? hivi ni sawa kwa kiongozi mbunge kuzungumzia haya kwa wanafunzi amabo ndio warithi wa taifa hili?

hii haipelekei kwa wanafunzi kuwa na uroho wa mali kuwa watasoma ili wafikie malengo hayo ambayo si malengo muhimu kwa ustawi wa taifa ukilinganisha na nilioyataja?


"KWA NINI" Ni neno la ajabu saaana. always linakuja baadaye kama kutafuta alternative. Hivi nikiuliza kwa nini wewe hukwenda kufanya hayo unayoyasema hapa what will you say of me? tuta argue endlessly. Mi nadhani mtu akifanya kitu haina mantiki kuja na presumptive za alternatives nyingine ambazo unaona angefanya! hii haiwezekani kwa hiyo huyu mbunge asingefanya hayo uliyotaka wewe kwa sababu mna mawazo tofauti. What is good to you is not the same kwa mwingine. Unapouliza kwa nini hakufanya vile na yeye atauliza kwa nini hukufanya vile...


So ni vema tuka comment kwa kuangalia yale aliyoyafanya na sio kuanza kutoa alternative ambazo unajua kabisa zitazua maswali mengi. Ndo maana yeye kaongelea kuoa mzungu na wewe unaona sio sawa! you cant think in the same way. .

Na kuwalaumu hawa viongozi...ni vema tukajiuliza nani anawapigia kura. Kwani walijipa ubunge? Usitake kuniambia hapa kwamba "elite" mmoja anajua what is good on behalf ya wapiga kura laki moja waliomchagua. Its the essence of the demon we call democracy! So get used to it my friend!
 
Nakubaliana na Masanja kuwa mbona amechukua muda mrefu sana alafu anapita kuwashukuru wananchi.Tunaongea 2008 na 2010 kuna uchaguzi au ndio maandalizi.

Sikubaliani kuwa anachosema mwana CCM ni sera ya chama la hasha,hii ilitokea ata kwa upande wa Chadema aidha kukubali uteuai wa Zitto ktk kamati ambapo Wangwe alitaka ajitoe na Chadema wakasema haikuwa sera na msimamo wa chama.Maneno ya Kevera si sera wala msimamo wa CCM.

Kila mahali pana mantiki yake na pana level fulani ya maongezi.Alichokifanya mbunge ni kuhamasisha wajitahidi ktk masomo.Kwa sisi Watanzania kuendelea kwetu ni kwenda Ulaya na ndio maana tunaamini kila aliyekwenda Ulaya nanapesa waliopo huko watadhibitisha kwa matatizo wanayopelekewa ya kifedha toka ama kwa ndugu au marafiki waliopo huku Tanzania ingawa si woote.

Kwa vijana wa Darasa la saba anachoamini ni kusoma na kupata kazi mzuri ikiwemo Ubunge na Ukuu wa Wilaya au Uwaziri.Sasa sio yote tunayofikiri angeweza kuyasema ktk muda mfupi aliowafundisha vijana.

Lamsingi na kubwa tumeona amewaasa vijana wasome kwa bidii hilo ndilo la kujivunia na ndiyo msg kubwa ambayo tunatoka nayo.Kuoa mzungu na kupata kazi mzuri ni namna ya vivutio vya kuwafanya wasome kwa bidii.

Mimi sioni kama amefanya kosa kwa kusema kuwa wataoa mzungu.Na bado miongoni mwetu tunaona dili ni kuoa mzungu huu ndio ukweli uliopo.

Nawasilisha.
 
Tunakumbuka ''maslow's needs hierarchy?, kwamba mtu huwa anakuwa motivated kwa namna tofauti na wakati tofauti kutokana na khali yake ilivyo(socio economic status). Kwa mazingira ya kijijini hilo linaweza kuwa ni motivation factor kubwa sana lakini sisi humu ndani ambao ''at least'' tupo in other planet tukaona ni pumba, halafu as much as we have read kuwa pamoja na kuwa motivate kivingine i.e kupata kazi,kwenda ulaya, kuwasasaidia wazazi wao etc he aslo mention hili la kuoa mzungu, so I personal think he was RIGHT as far as the socio-economic situation alipokuwa is concerned.
 
Huyu Mh. ni kilaza sana
Nakumbuka kuna siku alipata nafasi ya kuchangia hoja bungeni aliinuka na kusema namnukuu "Mh. Spika kwanza nakushukuru kwa kunipa nafasi hii kuchangia hoja, pili ningependa kuwashushukuru wananchi wangu wa jimbo la Njombe Mashariki kwa kunichagua kuwa Mbunge wao........ ndugu wananchi wa Njombe Mashariki, mimi mnayemuona kwenye TV ndiye Mbunge wenu Yono Kevela" Mwisho wa kunukuu. Na katika kuchangia hoja yake alisema yafuatayo, namnukuu...." Mh. Spika ningependa kuongelea kuhusu 'vinyungu' ikiwa serikali itapiga marufuku wananchi wasilime 'vinyungu' itakuwa haijawatendea haki wananchi wa jimbo langu maana 'vinyungu' ni mkombozi kwa wananchi wa jimbo langu" Mwisho wa kunukuu.
Achilia mbali suala la kuwaweka alama watu wenye virusi mithili ya ng'ombe mnadani, juzi alinifanya nisiamini nilichokuwa nikikisoma baada ya kuona forecast zake ni very primitive eti watoto wasome kwa bidii ili waweze kuwa na magari kama lake, waweze kuwa wabunge kama yeye, wawe mawaziri wawe marais kama Kikwete, akazidi kunichanganya eti waweze kuoa au kuolewa na wazungu.
Huyu ni mtu muwazi sana ameweza kutoa aliyonayo moyoni mwake ambapo yeye anaona ni mapya yanayoendana na ari mpya nguvu mpya na kasi mpya. Lakini tukikumbuka kwamba tupo karne ya 21 tunajua wazi kwamba bado tunatambaa wakati wenzetu wanapokezana vijiti. Hata hivyo katiba yetu inasema kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake ili mradi havunji sheria.
 
Back
Top Bottom