Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 674
jamani hivi alivyofanya mbunge huyu kuwahusia wanafuni kusoma kwa bidii ili wapate hayo aliowaeleza ni sawa au amekosea?
na kustaarabika ni kuoa mzungu?
hivi ndio watanzania tunavyofikiri? au ni mbunge huyu tu ?
Mbunge aingia darasani, kufundisha
na George Maziku, Njombe
MBUNGE wa Njombe Magharibi, Yono Kevela, amelazimika kuingia darasani kufundisha kama njia ya kuhamasisha watoto kupenda elimu.
Tukio hilo la kuvutia lilitokea katikati ya wiki hii, wakati mbunge huyo alipokuwa katika ziara ya kukagua shughuli za maendeleo na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Mbunge huyo aliingia darasani na kufundisha somo la hesabu kwa wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Mayale, iliyopo Kijiji cha Mayale, Kata ya Wangingombe, jimboni humo.
Yono alitumia karibu dakika 30 kufundisha hesabu za maumbo, huku akiwapa wanafunzi nafasi ya kumuuliza maswali mbalimbali yanayohusu somo la hesabu.
Mbunge huyo alifika shuleni hapo majira ya mchana na kwenda moja kwa moja darasani na kumwomba mwalimu aliyekuwa akiwafundisha, ampatie nafasi ya kuonyesha utaalamu wake katika somo hilo.
Mwalimu huyo, Isack Joram ambaye ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, alimruhusu mbunge Yono kuwafundisha wanafunzi.
Baadaye mbunge huyo alipata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo, na kuwasihi kuongeza bidii katika masomo, ili baadaye waishi maisha mazuri.
Someni kwa bidii mpaka mfike sekondari na chuo kikuu, ili baadaye mgombee ubunge kama mimi, mpate ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa, uwaziri, na hata urais wa Tanzania kama Kikwete.
Mkisoma mtapata kazi nzuri, mtanunua gari nzuri kama yangu, mtajenga nyumba nzuri, mtapata fedha za kuwatunza wazazi wenu, mtapanda ndege na kusafiri mpaka Ulaya, Marekani na kuoa au kuolewa na Wazungu, alihamasisha na kushauri mbunge huyo.
Yono alisema hakuna lisilowezekana hapa duniani, lazima mtu asome kwa bidii na kuhitimu vema masomo yake, ndipo atafanikiwa kimaisha.
Pia aliwasihi wanafunzi hao kujihadhari na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) na ugonjwa wa ukimwi, ili waweze kufikia ndoto zao za kimaisha.
Baada ya kufundisha, mbunge huyo alitoa msaada wa mpira mmoja wa miguu na kuahidi kuchangia ujenzi wa madarasa ya shule hiyo unaotegemewa kuanza hivi karibuni.
Shule ya Msingi Mayale ilianzishwa mwaka 1972, lakini haikuwa na maendeleo mazuri kitaaluma, mpaka mwaka jana ilipofaulisha wanafunzi 23 kati ya 28 waliofanya mtihani wa mwisho.
Kwa sasa shule hiyo ina wanafunzi 294 na walimu saba, ambao hawatoshelezi mahitaji halisi ya shule hiyo.
source tanzania daima