mandingo6262
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 424
- 81
Habari zenu wana jamvi, kwa wakati mwingine ningependa nilete kwenu na suala hili. Katika jimbo la Tarime kuna shule moja ambayo ipo takriban kilometa nne kutoka mjini kati na ipo jirani na nyumba ya mbunge wa jimbo hilo Mh. Nyambari Nyangwine. Shule hiyo ijulikanayo kwa jina la Nkende sekondari imefungiwa na wakaguzi wa shule kanda baada ya kukuta kwamba haina mashimo ya kutosha kwa ajili ya huduma ya choo kwa wanafunzi mnamo tarehe 8/5/2013 hadi sasa.
Maswali ya kujiuliza?
Maswali ya kujiuliza?
- Kama shule hii iliyopo jirani na nyumbani kwa mbunge ipo katika hali hii na imefungiwa vipi kuhusu shule ambazo zipo mbali na eneo lake la makazi?
- Anayeathirika na kufungiwa shule hiyo ni nani kama si wanafunzi?
- Wanafunzi wakianza kidato cha kwanza hutakiwa kupeleka michango mbalimbali kama michango ya majengo, ulinzi, madawati na kadhalika je michango hiyo ina mantiki na inatumika vipi?
- Kuna haja ya kuchunguza chanzo cha kufeli kwa wanafunzi hao na wakati sababu zinaonekana wazi?