Mbunge wetu kuendesha V8 naweza kuelewa, lakini “mchungaji” wa Kanisa!!

Ndege Mwema

Member
Nov 30, 2013
9
1
Pamoja na kuwa “posts” nyingi sasa hivi ni Zitto hivi, Chadema vile nitafurahi kama wanajamvi wenzangu hawatanishangaa ninapoleta post hii ambayo ipo nje kabisa ya “Zittoism” na “Chademaism”.



Katika moja ya makala iliyotafitiwa mwaka 2011 na mmoja wa waandishi mahiri wa jarida la Forbes, Mfonobong Nsehe, utafiti alioufanya kwa baadhi ya “wachungaji” nchini Nigeria inaonyesha wengi wa “Wachungaji, Maaskofu, Mitume na/au Manabii”ambao walijianzishia makanisa yao nje ya yale ya zamani yaliyozoeleka k.m Katoliki, Lutheran na Anglican wana utajiri mkubwa usio wa kawaida.



Kwa mujibu wa maelezo ya Nsehe mchungaji anayeongoza kwa utajiri nchini Nigeria (jina nalihifadhi) ana utajiri unaokadiriwa kufikia dola za kimarekani milioni mia moja hamsini ($150 million). Tangu alianzishe kanisa lake mwaka 1981 likiwa kikanisa kidogo tu, kanisa hilo limekuwa hadi kufikia kuwa ndio kanisa lenye uwezo wa kuchukua watu wengi kwa wakati mmoja barani Afrika, lina uwezo wa kuingiza watu 50,000 kwa mara moja na ambapo siku za jumapili huwa na ibada tatu. Mchungaji huyo anamiliki ndege binafsi nne na ukiacha nchini kwake anamiliki pia jijini London na nchini Marekani nyumba kadhaa za kifahari. Anamiliki Chuo Kikuu, Sekondari ya juu (High School) na kampuni ya Uchapishaji inayochapisha vitabu vyake.



Ingawa naweza kutia shaka kama kweli kukua huko kwa kanisa lililotolewa mfano kumetokana na sadaka za waumini wa hicho kilichoitwa kikanisa wakati kinaanzishwa mwaka huo wa 1981 bado si nia yangu kumaanisha kwamba watumishi wa Mungu wawe na maisha ya kimaskini, lakini ninapoangalia tofauti ya hali za maisha za baadhi ya hao tunaowaita watumishi wa Mungu waliopo hapa kwetu kwa ulinganisho na sehemu kubwa ya maisha ya waumini wao ambao (naamini) ndio huchangia kiasi kikubwa cha hali za maisha za watumishi hao kupitia sadaka zao n.k, kidogo nakuwa na mashaka kama kweli huyo Yesu wanaedai kumtumia katika kutoa mapepo, kuponya, kuleta neema kwa waumini wao n.k anafurahia tofauti hiyo huko aliko. Inapotokea Mtume/Mchungaji anatumia gari ya fahari kama Hummer, Land Cruiser V8 n.k ambayo ni gharama kubwa kuwa nayo na kuyatumia wakati katika jamii anayoihudumu kuna umaskini uliopitiliza, mayatima kwa maelfu, wajane wasio na msaada, wasiojiweza n.k, nalazimika kubaki na maswali yasiyo na majibu ingawa pia simaanishi kwamba viongozi hao wa makanisa watembee kwa miguu ama wapande punda kama zama za Yesu.



Kwa mishahara, posho na marupurupu wanaojipangia hao wanaojiita wawakilishi wetu (wabunge, mawaziri n.k) ukiongezea na “takrima” wanazozipata baadhi yao “kiaina” kutokana na nyadhifa zao sitashangazwa na staili zao za maisha zinapokuwa za kimungu watu (rejea mmoja wao aliyewahi kudai siku kadhaa zilizopita kwamba wao ndio wenye nchi, hakuna wa kumfanya lolote), lakini kwa “watumishi wa Mungu” wanaodai kumkiri Yesu ambaye kiimani ndiye kimbilio la wanyonge kuishi maisha ya staili za “Hummer” na “V8” nadhani sitatenda dhambi nikisema wengi wa wanaojiita watumishi wa Mungu siku hizi badala ya kutanguliza mapenzi yao katika kuokoa roho za waumini wao ili hatimaye wafike peponi kama lilivyokuwa kusudio la kiongozi wao Yesu Kristu, wamekuwa wakilitumia jina la “Masiha” huyo kufanikisha malengo yao ya kidunia.
 
Back
Top Bottom