Mbunge wetu J. Mnyika uko wapi?wakazi wako wa ubungo hatuna maji

Yule

Member
May 4, 2012
14
5
Sasahivi inaenda wiki ya pili hatuna maji na mpaka sasa hatujaambiwa tatizo nini, tunakuomba mbunge wetu ulifatilie maana tunapata taabu kwa kuuzima maji si salama na bei kwasasa ni mia 5 kwa dumu.
 
Nivea

JF-Expert Member
May 21, 2012
7,458
4,717
Yuko bize kuhakikisha yake majibilioni 80 yaliyochotwa kule wizara ya nishati na madini yanarudishwa .inauma sana kila mwezi tunalipia umeme wenzetu wanazichota kwenda kujengea makwao jamani lol viongozi tuoneeni hata huruma watu tunaweka umeme wa elfu tano kwa mwezi mnatuibia?
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
Sasahivi inaenda wiki ya pili hatuna maji na mpaka sasa hatujaambiwa tatizo nini, tunakuomba mbunge wetu ulifatilie maana tunapata taabu kwa kuuzima maji si salama na bei kwasasa ni mia 5 kwa dumu.
lazima utakuwa si mkazi wa ubungo kwani wakazi wa ubungo wanajua kwanini hawana maji na hawawezi kumuuliza mnyika swali kama hilo kwani wanajua ni nani anayekwamisha maji ubungo.
 
AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
5,027
Kwani shida y maji ni ubungo 2? Hebu achen lawama za kitoto na badala yake muungeni mkono mbunge wenu ktk kuisimamia serkali ili tupate maisha bora.
 
nemasisi

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
1,957
566
Nadhani swali kwanini maji hayatoki ubungo lingekuwa sahihi kama ungewapigia dawasco au serikali kupitia wizara ya maji unless kama huo mradi uko chini ya mbunge
 
Codon

JF-Expert Member
Dec 16, 2011
629
93
J.j Mnyika,wasipokutaja humu Jf wk tu nadhani wanapewa adhabu!Wameanza kama swali toka jimboni lakini utaona post zao zinavyoondelea!
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,395
Tulimuuliza meneja wa DAWASCO Magomeni akasema barabara ya Morogoro inayojengwa upya inaharibu sana mtandao wao wa mabomba ya maji mara kwa mara. Maendeleo nayo yana gharama zake.
 
Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,260
5,156
Hivi dar yoote jimbo lenye shida ya maji ni Ubungo tu?enyi wana JF ifike mahali muone aibu sasa kumshambulia Mnyika,hakuna sehemu kuna shida ya maji kama kinondoni na temeke ila hizo malalamiko hutayaona hapa why and why mnyika always?
 
FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
314
Mimi mkazi wa kimara maji yanatoka kila siku jioni usiku na asubuhi mpaka saa 2 ndo yanakatika.

Kama maji yakikatika kwetu ujue dar nzima hakuna maji sema kwetu ni karibu na barabara labda.

Nitasema kitu tatizo la maji dar ni miundombinu hivi wakazi wa ndani ndani si karibu na barabara inakua ni vigumu maji kufika mengi yaishia njiani na dawasco hawajitanui masikini wa Mungu.

Kama tungekua na miundombinu bora matatizo ya maji yasingekuwepo nawapa challenge hii dawasco waboreshe miundombinu ya maji maana ya sasa ni ile ya zamani ya wakazi wachache wachina wamekuja wameshindwa kuna sehemu korofi kuna vilima maji yansindwa kupandwa.

Wajenge visima venye uwezo wa kuchukua maji zaidi lita za ujazo laki 5 sasa tuseme maji si yataoka usiku wale wakazi wa mbali maji yanavuta hadi kwenye hiko kisima na baadaye kutoka pale yataanza kusafirishwa kwenda majumbani hii itamfikia kila mkazi na hakutakua na malalamiko.

Kuongozea dawasco wanapoteza maji mengi njiani mengi yanawagika wanashindwa yatumia vizuri haya maji kwa mfano nilikua kiluvya mabomba yamekatika watu wanajichotea maji.

Je watu wangapi mnatumia maji bila kulipia bill mwisho wa mwezi na sisi tuwe wazalendo tulipie bill ili shirika lianza kufanya mambo ki sayansi

Fred kavishe
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,563
7,141
Sasahivi inaenda wiki ya pili hatuna maji na mpaka sasa hatujaambiwa tatizo nini, tunakuomba mbunge wetu ulifatilie maana tunapata taabu kwa kuuzima maji si salama na bei kwasasa ni mia 5 kwa dumu.

Kariakoo sasa ni wiki ya tatu,umeme ni wa kubip kila siku tunaungurumisha majenereta huku tukipoteza pesa nyingi kuupata umeme wa jenereta.Aibu kwa Serikali ya ccm,usisahau kazi za Wabunge ni kuishauri Serikali kama Mnyika keshazisema kero za wakazi wa Ubungo na Serikali haijatekeleza unataka Mnyika aingie mfukoni mkuu kukupatia maji?
 
mayoscissors

JF-Expert Member
Nov 24, 2009
975
470
Serikaliya ccm ndo inastahili hili swali na wala si mnyika,mimi naishi ubungo kibangu yapata miaka minne nanunua maji ila sitamuuliza mnyika kwani hakusanyi kodi
Sasahivi inaenda wiki ya pili hatuna maji na mpaka sasa hatujaambiwa tatizo nini, tunakuomba mbunge wetu ulifatilie maana tunapata taabu kwa kuuzima maji si salama na bei kwasasa ni mia 5 kwa dumu.
 
kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
8,136
5,763
Sasahivi inaenda wiki ya pili hatuna maji na mpaka sasa hatujaambiwa tatizo nini, tunakuomba mbunge wetu ulifatilie maana tunapata taabu kwa kuuzima maji si salama na bei kwasasa ni mia 5 kwa dumu.
hivi waziri w. Maji na naibu wake wapo wapi? Dawasco wapo wapi? Mnyika mtamuu na maneno.
 
kipuyo

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
1,766
1,428
Sasahivi inaenda wiki ya pili hatuna maji na mpaka sasa hatujaambiwa tatizo nini, tunakuomba mbunge wetu ulifatilie maana tunapata taabu kwa kuuzima maji si salama na bei kwasasa ni mia 5 kwa dumu.

Mkuu afadhali ya ubungo,mi nipo Singida mjini,tangu nihamie hapa miezi minne cjawahi kuona maji yakitoka bombani.Huku ndoo inauzwa kati ya shilingi za kitanzania1000 hadi 2000.Najuta kutoka survey jimbo laHalima Mdee kwenye maji mengi muda wote.

Naomba mwenye namba za mbunge wetu wa singida Mjini ndugu Mohamed Dewji,amueleze kuwa tunataabika kwa shida ya maji.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom