Mbunge Wenje: Uwekezaji unarudisha ukoloni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Wenje: Uwekezaji unarudisha ukoloni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Aug 16, 2011.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mbunge Nyamagana Chadema, Hezekia wenje amesema kitendo cha kuwapa ardhi kubwa kwa miaka mingi ( 99 years) watu kutoka nje ya nchi ni sawa na kurudisha Wakoloni Tanzania kwa jina la wawekezaji. Mh Wenje alitoa mifano michache ya maeneo ambayo wawekezaji wamepewa maeneo makubwa sana ya hekta na mahekta ktk nchi yetu, huku akihoji tofauti ya wawekezaji hawa na wawekezaji waliokuwepo kabla ya uhuru ambao tuliwaita wakoloni.

  Mh. Wenje aliyasema hayo wakati akichangia hoja ya wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi leo asubuhi around saa nne na nusu .

  My take:

  Maswali;


  1) Hivi wawekezaji wakipwa maeneo makubwa sana ya Tanzania yasiyokuwa na wakazi ambayo ni zaidi ya robo ya ardhi yetu (not sure) kwa miaka 99, tafsiri yake ni nini kwa uhuru wetu? Imagine maeneo hayo yana milikiwa na wazungu na waarabu tunaowaita wawekezaji kwa miaka 99, watanzania wanaajiriwa humo kwa 80,000 kwa mwezi kwa masaa karibu kumi kwa siku, kama ninavyofahamu mkoa wa pwani wilayani Kisarawe.


  2) Wale watanzania wanaoishi ktk maeneo ya wawekezaji na kufanya kazi humo tunawatofautishaje na wale manamba wa enzi ya ukoloni, waliofanya kazi ktk mashamba ya wakoloni?

  3) Chukua maeneo husika hayana wakazi, Ipi bora, kuyaacha hayo maeneo yakae bure au kuwapa hao wawekezaji au wakoloni (as per Wenje) wapya aka wawekezaji ambao serikali inasema wanaleta ajira na kulipa kodi?

  4) Kwa maeneo yenye wakazi hasa madini,

  Hivi kama mtanzania anaweza kufukuzwa ktk eneo lake ili kumpisha mwekezaji/wakoloni wapya as per Wenje, nini maana yake kwa uhuru wa nchi yetu?


  Am just questioning myself.
   
 2. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amesema pia kwamba kule Zimbabwe Mugabe yamemshinda halafu sisi Tanzania ndo tunashadadia wawekezaji wa mashamba makubwa (99 yrs), kisha akawanyooshea kidole watumishi wabovu wa Ardhi wanaodhulumu viwanja vya watu kwa kushirikiana na matajiri.

  Serikali iliyoko madarakani ndiyo inawakumbatia watendaji hao, kwa sababu wanawapa viwanja kwa njia ya rushwa.
   
 3. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Wakati mwingine unajiuliza. tulipigania uhuru wa nini wakati hata miaka hamsini hatujatimiza bado, tunawarudisha wakoloni walewale.
  Je tulikuwa tayari kujitawala? au ulikuwa wivu wa madaraka?
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tatizo linaanza hapa kwenye hiyo sentensi, ni kweli wafanyakazi wizara Ardhi ni wabovu, hawana maadili na wala rushwa kupindukia.

  Double allocation, allocation of opens spaces, land speculation, kugawa viwanja hata kwenye barabara na cha ajabu hakuna hata mmoja aliyewajibishwa mpaka leo pamoja na madudu yote haya miaka yote hii.

  Vitendo hapo juu ni abuse of office kama alivyofanya Liyumba, haina tofauti
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Vincent Nyerere naye anaongezea kwamba hakuna sababu ya waziri kwendelea kuwa waziri kwa sababu bajeti yake ni finyu na haiwezi kukidhi chochote pia naongelea migogoro ya jeshi na wananchi
   
 6. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #6
  Aug 16, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Habari hiyo inanikumbusha kufikiria waliotunga 'salamu' za chadema
  kati ya Kiongozi na waitikiaji/wananchi
  1)Chadema - vema
  2)Chadema - mabadiliko ya kweli, uhuru wa kweli.
  3)Peoples' - Power
   
 7. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  Tumethubutu ...tumeweza ...tunasonga mbele!
  ...hivi niko sawa!?
  Tuna matatizo mengi zaidi ya tulivyofikiri hapo awali, mfano angalia kinachoendelea Dar es Salaam kati ya mayor na subordinates wate (akina Zungu na Mtenvu) kama sample tu, ni aibu kwa watu waliojitawala kwa miaka 50! tusisahau Dunia inatufuatilia.

  Tatizo lingine ni EXPOSURE ya mambo, maana utashangaa mtu anauza barabara ili iwe makazi, lakini ukienda miji ya watu wengine ukaona faida ndogo ya planning za miji labda wangekuwa na modeartion kidogo katika kuharibu. Lakini pia tukumbuke sio viongozi tu bali hata sisi wenyewe akili zetu 'zimepinda' na hatuko tayari kupokea madadiliko!

  Masikitiko makubwa sana
   
 8. m

  mndeme JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  amemtaja jamaa anaitwa Otieno kuwa mekuwa mungu mtu kwa migogoro ya ardhi mwanza, anayemfahamu hyu tunaomba atupe cv yake maana kawa gumzo leo mpaka baadhi ya magamba wakawa wanaomba mwongozo ili kumzuia wenje kutamka jina lake, nikashangaa sana maana wakat wanamchana Jairo hakuna aliyetaka mwongozo
   
 9. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Nchi taabani,walishaikalia mabepari basi tena.
   
 10. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Bila shaka wale tuliokuwa tunawaita wakoloni leo hii tunawaita wawekezaji. Prof CHACHAGE anasema katika chapisho lake lijulikanalo kama ' Globalisation and Democratic Governancein Tanzania nanukuu "In this era, neo-colonialism is dubbed"globalisation" and exploiters are crowned the cap of "investors" or better still called, "the vital force of our nations" mwisho wa kunukuu. Kwa maneno hayo ya the late prof chachage utaona kabisa hoja ya wenje ina hold water.
   
 11. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Miaka 50 ya uhuru Hatuna MAENDELEO' kisa hatuna uongozi bora.Ardhi ipo na watu wapo,sema hv 2nakosa SIASA SAFI NA UONGOZI BORA.
   
 12. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Haya ni matokeo yakuongozwa na serikali legelege.Wiki iliyopita mgao wa umeme ulikuwa umekoma ghafla saiv Budget ya Nishati na Madini imepita imekuwa Bora ya ule mgao wa Mwanzo yaani mgao to the maximum,mafuta pia yameshapanda bei ghafla kisa wabunge wamepitisha Budget kwahiyo kumbe haya mambo yanafanywa makusudi kwamba tutawafanya nini?
   
 13. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Kwa nini Tusiutangazie tu Ulimwngu kuwa Ardhi ya Tanganyika Inakodishwa kwa Miaka 99 Hao wakina Onyango wamalize Biashara yao ya kuuza Wapumzike sio kila siku Marumbano....
   
 14. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  naaam...tumethubutu na tunaweza! pambaff sana hii nchi na viongozi wake
   
 15. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli ardhi ya Tanganyika imewekwa rehani kwa "wawekezaji" waliofukuzwa na baba na babu zetu miaka ya nyuma tukiwaita wakoloni
   
 16. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mchango wako una tafakuri kubwa sana, Ni kweli tulidai uhuru wa nini kama hatukuwa na uwezo wa kitawala na kuwekeza wenyewe, tunawaita wakoloni warudi kuwekeza ili iweje inaleta picha gani hii. Wajinga sisi sijapata kuona.

   
 17. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,061
  Likes Received: 417
  Trophy Points: 180
  Nani kasema tulipigania uhuru? kama tungepigania, Tanzania isingekuwa hivi. Matatizo tuliyonayo yanatokana na kupewa uhuru kwenye 'sahani ya shaba'
  Angalia walipigania uhuru: Kenya, Zimbabwe, Algeria nk.
   
 18. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,018
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama kenya na zimbabwe ni mifano mizuri ya wapigania uhuru, tusiache wabunge wafikirie badala yetu manake mengine ni kasa.

  Mandela ndio mfano sahihi ambaye ameruhusu uwekezaji wa mabepali uendelee na wamatumbi waendelee kupiga siasa na kaburu alete maendeleo. Nyerere na mugabe wameshindwa kwa kuamini wamatumbi, ambao wanapingana kila kukicha na hawapendani.
  Maendeleo yanakwenda tofauti na wenje, uwekezaji ni lazima
   
 19. S

  Safre JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi kwa uelewa wangu mdogo cthan kama ni busara kila cku waziri kuongeza pesa za mabajet mbugen hiv wataalam wao wanakuwepo wapi kabla.Hiv serikali hii ni makin kwel fine imeongezwa bungeni lakin kwenye vitabu pesa hazipo c wangeludi waandae vitabu upya da celewi hii system
   
 20. R

  Raila Member

  #20
  Aug 17, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  big up mh. Wenje you have told them the truth
   
Loading...