Mbunge Wenje amuumbua m/kiti wa bunge George simbachawene.....

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Mbunge wa CDM kamanda WENJE amefanya kazi moja katika kikao cha jioni ya leo baada ya kumuumbua mwenyekiti wa bunge George Simbachawene ambaye alikuwa akiliilinda serikali wakati wa mjadala wa marekebisho ya sheria ya manunuzi ya 2004…M/kiti huyu alionekana akipinga kila wazo la wabunge wanaosema kuwa serikali isinunue vifaa vilivyotumika yaani USED…baada ya kufanya hivyo uvumilivu ulimshinda kamanda WENJE na kuomba muongozo wa M/kiti juu ya maneno yake yanayoonekana kama yanataka kuwabana wabunge katika michango yao…baada ya kauli ya WENJE m/kiti alinyanyuka kwa aibu akaomba asieleweke vibaya….Alikuwa anaweka mambo sawa kama M/kiti wa Bunge.

Wazo langu:

Huyu jamaa alikuwa anailinda serikali waziwazi....na hii ndio dawa yao.
 
sure ila peter selukamba kunavitu kapayuka imenifanya niwamiss kina zitto na lissu bungeni
 
Hongera sana wabunge wa kweli wa wananchi wote, wabunge wa CCM wapo kulinda maslahi ya mafisadi kwani hiyo ndio sera ya chama chao.
 
Tobaaa!!! serikali inataka nnua mitumba????????? hakyamungu hili kenge la msoga tumelipata...............nimesoma report ya IMF na very soon Greece ya pili itaibuka tanzania..kujifanya Austerity plan..
 
hii nchi bana wananikumbusha hii issue ya vitu vipya lakini havina ubora kabisa kwa mfano tractor mpya la kichina na Massey Furguson second hand ambayo itafanya kazi kwa miaka mitano wakati mpya ya kichina inafanya kazi miezi sita tu, usitake kujua tofauti ya bei unaweza ukazimia.
 
Mbunge wa mbozi magharibi CDM alimalliza kila kitu serikali inataka kuua raia wake kwa kuwanunulia usafiri used tren used 4rm JPN
 
Kila angle ni ufisadi,
Wapeleke na mswada wa kuhalalisha ufisadi maana tumechoka sasa.
 
nashangaa jamaa wanavyokomalia mitumba eti serikali haina uwezo!kama ni hivyo magari ya rais yanunuliwe japan na yawe na mileage ya 65000km ili tujue tunabana matumizi kila eneo.
 
Mimi huwa siangalii USED ama New brand bali naangalia ubora. Huku kwetu H/M wameleta Powertillers mpya zinaitwa Changling zimelima mara moja tu tayari zimeshashushwa engine sasa si bora COBOTA ambayo ni Second hand.
 
Tobaaa!!! serikali inataka nnua mitumba????????? hakyamungu hili kenge la msoga tumelipata...............nimesoma report ya IMF na very soon Greece ya pili itaibuka tanzania..kujifanya Austerity plan..

Kununua vitu Used kwa kisingizio cha Austerity measures, sio sustainable..inahtaji fiscal measures, kipaumbele kwenye growth strategies, BoT kununua government bonds (hahaha, inaweza kweli??), na last but by no means the least effectiveness in public finance management kwa kupga vita ufisadi..
 
Tobaaa!!! serikali inataka nnua mitumba????????? hakyamungu hili kenge la msoga tumelipata...............nimesoma report ya IMF na very soon Greece ya pili itaibuka tanzania..kujifanya Austerity plan..

naweza ipata hiyo report mkuu?ngoja ni ku PM nikupe email yangu.
 
Ma-v8 yao yaletwe toka japan yakiwa na mileage 75000 twende sawa
 
Wapo ndo wanaandaa style mpya ya wizi,na kwa kuwa chama chao cha CCM ni cha kutetea mafisadi utaona mswada huo wataupitisha.
 
tatizo eti wabunge wanaamini watu watakuwa honest katika manunuzi ya used item.kuna mbunge mmoja anasema tusiweke sheria ya kuspecify ni wakati upi tunatakiwa kununua used items,eti tumuamini mbongo!kweli tunafanya makosa sana kupeleka vilaza mjengoni.
 
Mbunge wa CDM kamanda WENJE amefanya kazi moja katika kikao cha jioni ya leo baada ya kumuumbua mwenyekiti wa bunge George Simbachawene ambaye alikuwa akiliilinda serikali wakati wa mjadala wa marekebisho ya sheria ya manunuzi ya 2004…M/kiti huyu alionekana akipinga kila wazo la wabunge wanaosema kuwa serikali isinunue vifaa vilivyotumika yaani USED…baada ya kufanya hivyo uvumilivu ulimshinda kamanda WENJE na kuomba muongozo wa M/kiti juu ya maneno yake yanayoonekana kama yanataka kuwabana wabunge katika michango yao…baada ya kauli ya WENJE m/kiti alinyanyuka kwa aibu akaomba asieleweke vibaya….Alikuwa anaweka mambo sawa kama M/kiti wa Bunge.

Wazo langu:

Huyu jamaa alikuwa anailinda serikali waziwazi....na hii ndio dawa yao.

Kwa wale wanaofuatilia vizuri vikao vya Mikutano ya Bunge basi watagundua kwamba HAKUNA MWENYEKITI WA BUNGE ALIYE MNAFIKI,MKORA,NA KIZABIZABINA KAMA GEORGE SIMBACHAWENE. Huu jamaa ni mpuuzi kwelikweli! Hata akisimama kuchangia mada yoyote hasa kama inahusu upinzani basi ataponda upinzani kama vile Wabunge waliko kambi ya upinzani si Watanzania.

Yaani kama kuna kifungu cha sheria cha kumwondoa M/Kiti wa Bunge kwa KUTOKUWA NA IMANI NAYE basi Simbachawene anastahili kuondolewa kwa njia hiyo. Huyu akipewa uspika anaweza akasababisha ngumi Bungeni.He is too bogus.
 
Back
Top Bottom