Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,444
- 7,808
Mbunge wa viti maalum Wafanyakazi, Janejelly James Ntate amesema watumishi wameweza kuifikisha Tanzania Uchumi wa Kati kabla ya wakati wake mwaka 2025.
Akiwa kwenye vikao vya bajeti vinavyoendelea mjini Dodoma amesema watumishi walifanya hayo kwasababu serikali kupitia vyama vya watumishi iliwaomba watumishi waivumilie miaka mitano wajenge uchumi na baada ya hapo wataenda na maslahi ya wafanyakazi.
Ntate amesema ilani ya CCM ukurusa wa 180/1 inaongelea maslahi ya watumishi lakini waziri Jenster Mhagama alipowasilisha bajeti ya waziri mkuu hajaona nyongeza ya mishahara na TAMISEMI haijasema kama kutakuwa na nyongeza ya mishahara.
"Tunasema matatizo lakini hatuangalii chanzo cha tatizo, yawezekana hata kushuka kwa utendaji ni watumishi wamefika mahali wamekufa ganzi, tujiulize kwa miaka mitano ni watumishi wangapi wamestaafu kwa mshahara wa zamani na kikokotoo hufanyika kwenye mshahara" Alisema mbunge.
"Tumeshajenga uchumi umefika uchumi wa kati tena kabla ya muda wake na mambo ya kufanyia watumishi kwenye ilani yako 16. Kama wizara ya fedha ikija haina nyongeza ya mishahara, wabunge mnisapoti tukamate shilingi, watumishi wanaumia" Alipiga mkwara mbunge Janejelly.