Leo Mh. Rais wakati akizindua stand ya mabasi ya mbezi luis amepokea maombi murua kutoka kwa mwakilishi wa wananchi ambaye ni mbunge, nitapenda kuongelea ombi moja kati ya mengi aliyoyaomba kwa maana yote yamepata majibu safi sana.
Ombi lenyewe ni barabara za jimbo la Kibamba. Nakupongeza sana mh mbunge kwa kuomba kupatiwa japo barabara kidogo za lami. Ukikumbuka majibu ya Mh Rais ni kwamba umepewe majukumu ya kuungana na team ya TANROAD ili kuandaa barabara ambazo wananchi wako wanaomba ziwekwe katika kiwango cha lami.
Mimi kwenye hili nakukumbusha kujitahidi kwa hali na mali kuhakikisha unaendelea kufuatilia TANROAD ili wasije fanya yale ambayo hukuomba kwa mh rais. Barabara za kibamba unazijua vizuri sana, mfano barabara ya kutoka mbezi mwisho, msakuzi mpaka mpigi magoe kupitia makabe, mbezi mwisho kupitia Mbezi High School mpaka Mpigi Magoe, Kibamba Shule mpaka Mpigi Magoe, Mpigi Magoe mpaka Bunju n.k.
Hizi zote ni barabara za TANROAD na kwa ukubwa wake na umuhimu wake nitashangaa kama zote hizi tatu zitakosa kwenye huu ujenzi kwa maana ni kiungo muhimu sana na ziko busy sana na pia ukizingatia kwa mfano, hii inayotoka mbezi mwisho kupitia mbezi high-machimbo mpaka mpigi magoe, ni barabara yenye daladala kubwa ambazo hupotea kipindi cha mvua na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Kwa ushauri wangu, hizi ndo barabara kiungo ambazo mm naona ndo zinatakiwa ziwe za kwanza kuwa presented kwa mheshimiwa rais ili ziweze kuingia kwenye bajeti ya 2021/2022. (Kwa maana pia ziko chini ya TANROAD).
Nawasilisha