Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Siku zote majuto ni mjukuu. Majuto huja baada ya kufanya kosa kubwa ambalo haliwezi kurekebishwa kwa namna yoyote ile.
Ninakuona Mbunge wangu Godbless Lema jinsi ulivyojikunyata kwenye Selo usijue nini hatma ya maisha yako. Jukwaa lilikudanganya kuwa ukiwa mbunge, unaweza kusema lolote hata kama kusema lolote juu ya mamlaka kuu ya nchi. Hii yote ni kutokana na kibri cha madaraka, malezi mabaya ya utotoni pamoja na athari ya shughuli zako kabla hujawa mbunge.
Inaniuma sana kuona sasa wana Arusha wakiachwa bila kuwa na mbunge kwa sababu ya ujinga wa mtu mmoja tu na kutochunga kauli zake. Inaniuma sana. Kila nikifikiria jinsi wana Arusha walivyokupigia kura nyingi sana kwa matarajio utawawakilisha vema, sikutegemea kama leo hii utawaacha yatima. Walikutuma uende Bungeni ukawasemee kero zao na kuwasaidia kutatua matatizo yao. Hawakutuma umtukane Rais wala kuwasemea juu ya ndoto ulizoota kuwa Rais atakufa kabla ya 2020.
Mbunge wangu Lema, nayajua maisha ya Selo kwa vile niliwahi kupitia huko kuanzia usiku wa Oktoba 26, 2015 tulipokamatwa pale King D Sinza tukimsaidia Mzee aibuke mshindi. Nayajua maisha ya Selo tangu siku hiyo na sina hamu tena ya kurejea huko. Ukimuona mtu anatamani kurejea Selo basi unapaswa kumtafakari mara mbili mbili kwani kuna wengine wanafurahia maisha ya kule hasa nyakati za usiku.
Mbunge wangu Lema, nikikumbuka yaliyonipata usiku nikiwa Selo nikihamishia kwa mbunge wangu Lema hakika napatwa na huzuni kubwa sana. Kama yale ambayo mimi nilifanyiwa na wale niliowakuta anafanyiwa mbunge wangu basi kwa hakika ni fadhaha kubwa sana. Sehemu ya kulala inakuwa ni ndogo, watu wanakuwa na harufu za aina tofauti, mbu wanatung'ata kila kona, nafasi hata ya kunyoosha miguu hakuna, msosi unakuwa ni wa manati, hakuna nafasi ya kuongea na mwenzi wako kwa vile hayupo huko. Hakika ni tabu na mateso makuu.
Mbunge wangu Lema, wale waliokuwa wanakushangilia na kusema "Na Iwe Hivyo" wakati unamuombea mabaya Rais wa nchi leo hii hawapo pamoja nawe. Umebaki mpweke usipate hata wa kukushauri. Kosa umelitenda na limetendeka.
Mbunge wangu Lema, chama kimeshakupa kisogo. Hii ina maanisha kuwa hawaungi mkono kile ulichotamka na kwa hiyo kosa hilo ulilotenda limekosa baraka ya chama. Si Mbowe wala Mashinji wala Lowasa ambao wamediriki hata kuja Arusha kukuona na kukujulia hali. Wapo busy na kujenga chama. Jifunze kitu. Hata wale mawakili Nguli, Peter Kibatala, John Mallya na Tundu Lissu wameshindwa kabisa kukuokoa ili usiendelee kusota Selo. Ngoma imekuwa ngumu kwao.
Mbunge wangu Lema, ona jinsi Mkeo anavyogalagala kitandani usiku wa manane huku akijaribu kupapasa huku na huku pande zote za kitanda akitaraji kukugusa. Wapi! Lema hayupo tena chumbani bali yupo Selo ambako wamelala kwa kubanana.
Mbunge wangu Lema, watoto umewaachia majonzi makubwa sana. Jana nimemsikia mtoto wako mdogo akisema kwa huzuni kubwa sana! Alisema hivi;" Baba, mbona umekosa mapenzi kwa watoto wako kwa kukaa nje ya familia kwa zaidi ya wiki mbili sasa?". Iliniuma sana kwa sababu mtoto yule hajui nini kinaendelea kwa baba yake. Umemkwaza sana na unamtesa mno.
Mbunge wangu Lema. Nakuhurumia sana