Mbunge wa zamani Felix Mrema Matatani, adaiwa kutelekeza Mkewe wa Ndoa suala latinga kwa DC na Polisi

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini ,Felix Mrema(CCM) anatuhumiwa kumtelekeza mkewe wa ndoa,Mchungaji dr.Milcah Mrema na kusababisha kuishi maisha ya shida na kulala nje ya nyumba yao baada ya mumewe kuipangisha kinyemela.

Akiongea kwa masikitiko akiwa nje ya nyumba hiyo aliodai wamechuma na mumewe iliyopo mtaa wa uzunguni jijini Arusha,amesema kuwa amelazimika kurejea katika nyumba yake baada ya kuchoka kuishi katika nyumba za kupangisha.

Alisema kuwa walishindwa kuelewana na mumewe na kulazimika kila mmoja kuishi kivyake kwa muda mrefu huku mumewe akioa mke mwingine.

Alisema baada ya kushindwa kuelewana na mumewe alienda kuishi katika nyumba moja iliyopo eneo la uzunguni ambapo mumewe( Mrema )alimlaghai kuwa alishainunua kutoka serikalini jambo ambalo si kweli kwani mwaka jana Juno,17 mama huyo alitolewa vitu nje kwa aibu na watu shirika la zana za kilimo na Teknolojia( Camatec) wakidai ni nyumba yao.

Hata hivyo hapo Jana Sep.2,2020 mama huyo aliamua kurejea katika nyumba yake akiwa na vitu vyake vya ndani na kulala nje kwa tabu huku akiogelea baridi na kung'atwa na Mbu alitaka mpangaji mwenye asili ya kiasi aliyepangishwa na mumewe kinyemela aondoke.

Akiongea kwa njia ya simu Mrema ambaye alikuwa mbunge wa Arusha kati ya mwaka 1997 hadi 2010 alidai kwamba suala hilo lipo mahakamani na wanasubiri maamuzi ya mahakama.juu ya hatima ya kugawana Mali zikiwemo nyumba.

Hata hivyo asubuhi ya Leo Mrema aliitwa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arusha na kituo cha polisi kuhusiana na mgogoro huo na mkewe.

Mama huyo ambaye alifanikiwa kuzaa watoto watatu na Mrema na mmoja kufariki amemwomba rais John Magufuli na jamii kwa ujumla imsaidie kuweza kupata haki yake kwani mumewe anamnyanyasa sana na hivi sasa hana kipato chochote na anaishi kwa kubangaiza.
IMG_20200902_131422_1.jpg
IMG_20200902_130624_6.jpg
IMG_20200902_131523_8.jpg
IMG-20200903-WA0014.jpg
 
Back
Top Bottom