Mbunge wa Viti Maalum, Mahawanga Janeth ashiriki katika uzinduzi wa mradi wa Digimali

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
871
951
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Mahawanga Janeth ameshiriki kama Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa mradi Maalum wa Digimali unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la Her Initiative chini ya ufadhili wa ubalozi wa uholanzi.

Mradi wa Digimali unatokana na neno digitali na mjasiriamali, yaani ujuzi wa kidigitali kwa mjasiriamali ambapo umebeba umuhimu mkubwa wa matumizi ya mitandao kwa watu wa rika zote katika nyanja mbalimbali, mfano biashara na mawasiliano na dhumuni kubwa la mradi ni kuwapatia vijana elimu juu ya usimamizi wa fedha na matumizi sahihi ya mtandao ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kwa kutumia vizuri technolojia iliyopo viganjani mwao mda wote katika biashara zao.

Katika uzinduzi huo Mhe. Mahawanga amempongeza Mwenyekiti wa Shirika la Her Initiative Bi Lydia Moyo kwa namna ambavyo anafanya kazi akishirikiana na wenzake kwa kuja na mradi ambao umeweza mpaka sasa kuwafikia vijana 100 kutoka sehemu mbalimbali Tanzania kama Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga, Kahama, Lindi, na Mikoa mingine ambapo Kati ya vijana 100 ambao ni wanufaika wa awali 86 walikuwa wasichana na 14 walikuwa ni Wavulana.

Aidha Mh. Mahawanga alisisitiza juu ya kuendelea kushirikiana na Taasisi na Mashirika mbalimbali yanayoshughulika na mambo ya kijamii hususani Wanawake na vijana ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam maana dhamira yake ni kuhakikisha wanawake ndani ya mkoa wa Dar es Salaam wanajikwamua kiuchumi kutokana na fursa zilizopo ndani ya mkoa lakini pia kuendana vyema na fursa za kiteknolojia.

Naye Mkurugenzi wa shirika la Her Initiative Bi Lydia Moyo ameeleza kupitia mradi huo wanufaika wameweza kuboresha biashara lakini pia ameahidi kuendelea kushirikiana na Mhe Mahawanga Janeth kwa pamoja ili kuweza kuwasaidia wasichana kwenye masuala la elimu juu ya biashara na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

#TishaMama
#ItazameDarKiutofauti
#KaziIendelee
 
Back
Top Bottom