Mbunge wa Viti Maalum Mahawanga ashiriki katika uzinduzi wa kongamano kubwa la wanawake wakristo

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
878
955
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Mahawanga Janeth leo ameshiriki katika uzinduzi wa Kongamano kubwa la Wanawake wakiristo, Women For Christ Alliance (WOCA) 2021 lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto ambapo Muasisi wake ni Hayati Bishop Mh. Dkt Getrude Lwakatare ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba.

Kongamano hilo ambalo litaendeshwa kwa muda wa wiki moja lililohudhuriwa na Wanawake 600 lenye dhamira ya kutoa elimu katika masuala mbalimbali kwa Wanawake ikiwemo masuala ya Uchumi, Vikundi, Fursa, Afya ya Mwanamke, Sheria ya fedha na masuala ya familia.

Akizingua katika uzinduzi wa Kongamano hilo Mh. Mahawanga amewasisitiza Wanawake kutumia vyema fursa ya kuishi Dar es Salaam kwa kuwekeza kwenye biashara mbalimbali za kiuchumi lakini pia kuhakikisha wanaendelea na zoezi la kuunda vikundi rasmi ambavyo vitaweza kuwasaidia kupata mikopo kwenye Halmashauri, Taasisi za kifedha na wadau mbalimbali wanaounga mkono juhudi za kuwakomboa Wanawake kiuchumi.

Mh. Mahawanga amepongeza Uongozi mzima wa Kanisa la Mlima wa moto wakiongozwa na Askofu Mkuu Bishop Anna Rosemary Mgeta na msaidizi wake Mhe. Muta Lwakatare ambaye pia ni Diwani Kata ya Kawe kwa kuendelea kumuenzi Muasisi Dkt. Getrude Lwakatare kwa kuendesha Kongamano ambalo aliliasisi linalokwenda kuleta tija ya kuwainua kiuchumi Wanawake kutoka pande mbalimbali ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Vile vile.Mh. Mahawanga amewaahidi akina mama hao kuwa nao bega kwa bega kuhakikisha wanaendelea kupata elimu ya vikundi lakini pia kupitia mikopo ya Halmashauri waweze kuanzisha miradi yenye tija itakayosaidia kukuza uchumi wao sambamba na kutengeneza ajira baina yao.

#TishaMama
#KaziIendelee
#ItizameDarKiutofauti
 
Back
Top Bottom