Mbunge wa Ushetu Aibana Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Bungeni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,890
939

MHE. EMMANUEL CHEREHANI - MASWALI NA MAJIBU BUNGENI KUPITIA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI

Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Kahama-Shinyanga Mhe. Emmanuel Cherehani katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni ameuliza swali Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambalo limejibiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Godfrey Kasekenya

"Barabara ya Mpunze - Sabasabini - Iponyankolo - Igwamanoni imekatikakatika, haipitiki kabisa na imepandishwa kutoka TARURA kwenda TANROAD. Ni nini mkakati wa Serikali kuijenga Barabara hii ili wananchi waweze kupita kwa urahisi"?

"Barabara hii ilikuwa inahudumiwa na watu wa TARURA, kwa sasa ndiyo imekuja TANROAD, naomba nimuhakikishie Mhe wa Ushetu na wananchi wa Ushetu kuwa tumesikia na ninamuagiza Meneja wa Mkoa wa Shinyanga aende akahakikishe yale maeneo yote ambayo yamekatika anayarejesha ili kuwe na mawasiliano na afanye tathmini kwenye maeneo yote korofi tuweze kuangalia namna ya kuyakarabati vizuri ili yaweze kupitika kipindi cha masika" - Mhe. Geoffrey Kasekenya


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom