Mbunge wa upinzani amvutia pumzi Ngeleja Bungeni........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,039
728,455
By PIUS RUGONZIBWA, 5th December 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 22

KASULU South MP (NCCR-Mageuzi) David Kafulila, intends to table a private motion in the National Assembly in February asking the august House to cast a vote of no confidence to the Minister for Energy and Minerals, Mr William Ngeleja, allegedly for failure to rescue the country from frequent power blues.

Addressing journalists in Dar es Salaam on Sunday, Mr Kafulila also accused Mr Ngeleja of failure to implement the National Energy Policy and the National Power System Master Plan causing the country to suffer three serious power rationing in the last two years which has caused a lot of economic damages.

Mr Kafulila who was elected into the House for the first time in the last October general election, said he would also hold the government responsible for negligence that would lead into paying about 185bn/- to Ms Dowans Co. being damages after winning the case against Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) in the International Commercial Court (ICC).

“Since 2006 the government has failed to solve power blues despite regular promises to deal with the problem and Minister Ngeleja’s statements that power problems would remain history have not been practical…and it now looks like a problem that is beyond our leader's capacity to solve,” he said.

On the Dowans and Tanesco controversy, he said it was surprising the government was about to pay billions of shillings in damages to the company it once described as non existent and fake.

Instead, he said, the government should have worked on stakeholders’ recommendation of buying the turbines valued at 70bn/- by then.

“But now it has to pay the company the money which would have been otherwise used to finance generation of at least 200MW for the national grid,” he said.

He further said that he would, in his private motion, ask the government to allocate enough funds for implementation of 2000MW Stigler’s Gorge project, 300MW Mnazi Bay project and 200MW Kiwira project whose execution had been delayed.
 
Dec 2, 2010
15
2
TAMKO LA MBUNGE WA KIGOMA KUSINI KUHUSU MGOGORO WA NISHATI YA UMEME NA KUSUDIO LA KUWASILISHA HOJA BINAFSI BUNGENI

JUMAPILI, DISEMBA05, 2010
Dar es Salaam.


UTANGULIZI
Karibuni wanahabari. Leo nimeamua kuwaomba kama wanahabari na watanzania wazalendo tujadili hatma ya Taifa letu ambalo utaratibu wa kuingizwa gizani na mgogoro wa nishati ya umeme unaelekea kukomaa na kuwa sehemu ya maisha ya watanzania.

Kwanza nipende kuwakumbusha tu kwamba tukiwa na nusu karne tangu tupate uhuru ni asilimia 14 tu ya watanzania ambao wanapata huduma ya umeme, kiwango ambacho ni sawa kabisa na takwimu za huduma hii kabla ya Uhuru takribani nusu karne iliyopita.Kwa vijijini kama jimboni kwangu na mkoa wa Kigoma kwa ujumla hali ni mbaya zaidi kwani kwa takwimu za sasa, ni asilimia 2 tu za watanzania vijijini wanaopata huduma ya umeme.

Lakini pia, tukumbuke kwamba bila nishati ya umeme ya uhakika hatuwezi kutekeleza MKUKUTA, hatuwezi kufikia MALENGO YA MILENIA, hatuwezi kufanikisha mpango wowote wa mapinduzi ama ya uchumi wala ya huduma. Takwimu mbalimbali na hata zile za Benki ya dunia zinaonyesha kuwa asilimia 40 ya uchumi duniani inategema nishati ya umeme.

Hapa Tanzania, kwa kasi ya ukuaji wa uchumi ya sasa ya takribani asilimia 7 kwa mwaka, uzalishaji wa Umeme unapaswa kukua kwa zaidi ya asilimia 15 kwa mwaka. Mahitaji ya Umeme nchini ni zaidi ya 1500 MW kwa mwaka, uwezo wetu ni kuzalisha 1034 MW lakini kiasi kinacho zalishwa ni 690MW tu kwa sasa kutokana na uchakavu wa mitambo na kupotea kwa umeme mwingi kwenye njia za kusafirisha. Hali hii ni mbaya sana kwa uchumi na inahitaji mikakati ya lazima kushughulikia.

Nikatika misingi hii watanzania tunawajibika kuwa wakali inapotokeo watu tuliowapa madaraka kutuongoza wanashindwa kutoa majibu ya msingi kuhusu masuala nyeti kama umeme.

Msingi mkubwa wa tatizo la umeme Tanzania ni serikali kufumbia macho miradi ya umeme ya uhakika ambayo ingetoa majibu ya kudumu ya tatizo hili na badala yake imebaki inasimamia sekta ya umeme kwa kudunduliza ikitumia mitambo ya kukodi ambayo kwa miaka sasa, tangu IPTL mwaka 1994 hadi Agreko, Songas, Richmond, Dowans imekuwa ikinyonya vibaya uchumi wa Taifa. Asilimia 86 ya mapato ya TANESCO yanatumika kulipia umeme unaozalishwa na mitambo ya kukodi ambayo inazalisha takribani asilimia 45 tu ya umeme wote. Hivi sasa mitambo ya kukodi inayotumika ni Songas na IPTL peke yake baada ya Agreko kumaliza mkataba wake na Dowans kufutwa mkataba wake. TANESCO wanailipa kampuni ya Songas takribani shilingi 266m kila siku kwa kununua 186MW za umeme. Mitambo ya IPTL ikiwa imewashwa TANESCO wanailipa kampuni hii shilingi 300m kila siku! Itakumbukwa kuwa TANESCO walikuwa wanapaswa kuilipa kampuni ya RICHMOND/DOWANS shilingi 152m kila siku kwa kununua 100MW za umeme.

Tangu mwaka 2006, serikali imeshindwa japo kupunguza tatizo hili la mgawo wa umeme. Viongozi wakuu wa serikali na hasa Waziri wa Nishati na Madini mara kadhaa wamekuwa akipotosha watanzania kuwa serikali inashughulikia kwamba mgawo wa umeme utakuwa historia lakini siku hadi siku sekta ya umeme imevuka upeo wa viongozi hawa kiasi cha kauli zao kupoteza imani kwa watanzania.

Leo tukiwa tunazungumza mgawo wa umeme, pembeni tunakabiliwa na deni la zaidi ya billioni 185 ambazo kwa uamuzi wa mahakama ya usuluhishi ya kimataifa (ICC) tunapaswa kuilipa kampuni ya Dowans, ambayo mpaka sasa serikali imekosa ujasiri kusema mmiliki wake ni nani lakini imekiri kushindwa kesi mahakama ya kimataifa.

Kwamba serikali isiyomjua wala kutambua uhalali wa mmiliki wa kampuni ya Dowans iko tayari kukiri kwa watanzania kuwa kampuni hiyo isiyojulikana mmiliki wake imeshinda kesi? Ni dhahiri kuwa Mahakama ya kimataifa yenye kuheshimika duniani kote haiwezi kukaa na kushiriki katika shauri ambalo Kampuni inayoshitaki haijulikani . Suala la umiliki wa Kampuni ya Dowans limekuwa likichezewa tu kwa maslahi ya makambi ya kisiasa ndani ya chama tawala.

Itakumbukwa pia kuwa mkataba ule ulikuwa ni wa miezi 24 na wenye thamani ya shs 172bn. Lakini kwa ukosefu wa uongozi na siasa duni ndani ya mfumo wa utawala wetu tunalipia shs 185bn tena bila kupata umeme. Billioni 185 zingetosha kuongeza 200MW za Umeme kwenye grid ya Taifa lakini sasa zinakwenda kulipwa kizembe. Huu ni unyama usio vumilika kwa watanzania maskini. Na ni unyama zaidii kwa watanzania masikini wa vijijini ambao asilimia 98 hawajui radha ya umeme lakini kodi zao sasa zinakwenda kutumika kijinga kabisa! Haiwezekani.

Mwanzoni mwa mwaka 2009 kulikuwa kuna mgogoro kuhusiana na ama TANESCO wanunue au wasinunue mitambo ya kampuni hii iliyotushinda kesi. Kundi moja la wabunge likisema isinunuliwe kwani itakuwa ni kukiuka sheria ya manunuzi (hakuna aliyethubutu kusema ni kifungu gani cha sheria ya manunuzi) na utata kuhusu mkataba wa Dowans(Hii ndio hoja ya msingi).

Kundi lingine lilikuwa likijenga hoja ya kununuliwa kwa mitambo ile ili kuepusha mgawo na vile vile iwe ni fursa ya kufuta kesi ambayo DOWANS waliifungulia TANESCO (mitambo ile ilikuwa inunuliwe kwa thamani ya shs 70bn). Kwa uamuzi tuliouchukua kama Taifa wa kutonunua mitambo ile, tunapaswa kulipa 185bn shs, mitambo wamebaki nayo na wataiuza watakapo baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kitengo cha Biashara kuamuru tarehe 22.10.2010 kuwa zuio la TANESCO dhidi ya Dowans kubeba mitambo ile lilikuwa batili. Mbaya zaidi Mgawo bado unaendelea na kuunyonya uchumi wa Taifa letu (bleeding the economy). Kinachosumbua hapa ni kwamba inawezekanaje serikali kushindwa kesi na kampuni ambayo tulielezwa mkataba wake ni batili( hapa ndio kuna siri nzito ndani ya serikali na chama tawala na ni siri hiyo nzito inayoendelea kukamua watanzania masikini mabilioni ya fedha ambayo yangepelekwa kwenye huduma za maji, Afya na Elimu).

MADHARA YA MGAWO

 • Uzalishaji viwandani : Shirikisho la wenye Viwanda nchini mara kwa mara limekuwa likieleza namna ambavyo wanachama wake wanaathirika na mgawo wa umeme. Mifano ya viwanda vya simenti imekuwa ikitolewa ambapo mgawo wa umeme unaongeza gharama za kuzalisha Simenti kwa kiwango cha dola za marekani 10 kwa kila mfuko wa kilo 50 wa Simenti na hivyo kuongeza gharama, kupata hasara na kushindwa kulipa kodi Serikalini.
 • Gharama za uzalishaji kuongezeka: Vijana wanaojishughulisha na kunyoa nywele jijini Dar es Salaam hupoteza zaidi ya asilimia 45 ya Mapato yao kutokana na kutumia majanereta ili kupata umeme wa kutoa huduma kwa wateja wao (REPOA report on electricity access for job creation 2010).
 • Bei za bidhaa kupanda kutokana na gharama za uzalishaji kuongezeka. Wafanyabiashara hujaribu kusukuma kuongezeka kwa gharama kwa walaji wa kawaida na hivyo kumdidimiza mwananchi wa kawaida. Maeneo ya vijijini ambapo hutegemea umeme kusaga nafaka zao kama Mahindi na Mpunga huathirika sana unapotokea mgawo kwa kutembea umbali mrefu kusaga nafaka na kwa gharama kubwa kutokana na gharama za mafuta ya kuendeshea majenereta kuwa kubwa.
 • Kusimama kwa shughuli nyingi za huduma kama benki, hospitali, vyuo na shule, na hata vyombo vya habari katika utendaji wake.


HATUA ZA KUCHUKULIWA.

  1. Serikali ione kwamba suala la mgawo wa umeme linaathiri maendeleo kuliko hata mtikisiko wa uchumi, hivyo ifanye maazimio magumu kwa kutenga fedha za kutosha kutekeleza mradi mkubwa wa umeme wa uhakika, kwa mfano Stigler’s gorge (2000MW), Mnazi Bay 300MW na kufufua KIWIRA 200MW. Miradi yote hii inaweza kuendeshwa na sekta Binafsi iwapo tutaweka mazingira mazuri ya uwezekezaji. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii sasa iachane na kujenga majengo na ijielekeze kwenye uwekezaji wa uzalishaji umeme ili kutatua kabisa tatizo la umeme nchini kwetu.
  2. Kwa kuwa Serikali ndiyo iliyoielekeza TANESCO iingie mkataba na RICHMOND na baadae kuuhamisha mkataba kwa kampuni ya DOWANS. Vile vile kwa kuwa BUNGE ndio lililotoa azimio la kuvunjwa kwa mkataba na TANESCO kufanya hivy; Hivyo basi TANESCO wasibebeshwe chembe ya lawama katika suala hili. Mzigo huu ni mzigo wa Serikali unaotokana na ukosefu wa umakini, woga na kutowajibika kiuongozi kwa viongozi wa Serikali. Serikali haipaswi kujitenga na gharama zitokanazo na madhaifu ya TANESCO katika hatua zote kwani serikali ndio msingi wa matatizo yote ya TANESCO na hivyo inawajibika kubeba deni lote.
  3. Kwa kuwa Serikali itapaswa kulipa deni hili kutoka katika fedha za walipa kodi wa Tanzania na kwamba fedha hizi zitaondolewa katika bajeti ya Elimu, Afya na kadhalika, ni lazima Serikali itoe maelezo ya kina ya sakata zima mpaka kufika tulipofikia. Haiwezekani serikali itumie kodi ya wananchi kulipa deni la mabilioni ya fedha kwa kampuni ambayo serikali imeshindwa kuthibitisha uhalali wake na hata kutaja mmiliki wake.

  1. Kwakuwa Taifa linaingia hasara kubwa ya mabilioni haya ya fedha kutokana na udhaifu wa serikali kusimamia mikataba na mpango mzima wa nishati, nakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni katika Bunge la Februari ya KWANINI SERIKALI ISIWAJIBIKE KWA KULINGIZA TAIFA HASARA KWENYE SEKTA YA UMEME.


  1. Pamoja na mambo mengine na vile Bunge litaona inafaa, nitalitaka Bunge liazimie kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini kwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati, na Mpango Kabambe wa usambazaji umeme (Power System Master Plan) na hivyo kusimamia migawo 3 ya umeme ndani ya miaka 2 ya uongozi wake.

Asanteni kwa kunisikiliza
Limetolewa na kusainiwa na;


David Zacharia Kafulila
Mbunge Jimbo la Kigoma Kusini
0716 42 62 20
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,744
28,934
Ni hoja yenye mantiki. Inastahili kuungwa mkono

Hoja ni nzuri yenye mantiki. Kuna ujanja unaotumika katika kupata ukweli. Leo tunaongelea mkataba kati ya serikali na Dowans. Hii si kweli hakuna mkataba kati ya serikali na Dowans, bali upo mkataba kati ya serikali na Richmond. Richmond iliuza mktaba[ kama ulikuwepo] kwa Dowans na kama hivyo, maana yake ni kuwa mkataba huo ni valid, basi tuambiwe lini serikali na Dowans walisaini maridhiano ya kuhamisha mkataba wa Richmond, na ni nani alisaini mkataba huo kwa niaba ya Serikali. Na kwa vile sula lhili lilikuwa chini ya ofisi ya Waziri mkuu [Lowasa], je ni nani aliridhia kuhamishwa mkataba toka Richmond kwenda Dowans? na kama kulikuwa na mkataba mpya na Dowans nani alisaini kwaniaba ya serikali na alisaini dhidi ya mwakililshi gani kutoka Dowans.

Pili, hela zinazotarajiwa kulipwa Dowans zinalipwa ni zile za kuvunja mkataba na Richmond ambayo haikuwepo[rejea kamati ya bunge ya Mwakyembe]. Sasa kampuni ambayo haikuwepo iliuza au kutoa mkataba kwa kampuni nyingine ambayo haijulikani kwa Serikali kwa njia gani?

Tatu, Wananchi wasikomalie Dowans, kwanza tujue mkataba na serikali ulitolewa kwa Downs lini na kwanani.
Kinachofanywa hapa ni kutaka kuitumia Dowans[ ambayo haipo] kuificha Richmond[Haipo]. Richmond inataka kufichwa kwasababu inagusa watu wa mzee. Tusirukie Dowans, tujiulize iliingiaje mkataba na Serikali?
Mwisho serikali ituambie, imeshindwa kesi na nani Richomnd au Dowans, kama ni Dowans basi tuambiwe mkataba na Dowans ullianzaje na lini, nani anamiliki Dowans.
Tufike mahali tukatae kugeuzwa mazezeta ili hali tuna akili zetu.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,725
104,908
Ni aibu kuwa hili tatizo licha ya kuwepo miaka nenda rudi, bado halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Only in Africa where you will this kind of foolishness.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,039
728,455
SAKATA LA DOWANS: Spika Makinda apata kigugumizi


na Janet Josiah


amka2.gif
WAKATI Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) likiwa linajipanga kuilipa kampuni ya Dowans sh bilioni 185 kwa kosa la kuvunja mkataba, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda, ameahidi kulizungumza suala hilo baadaye. Makinda alitoa kauli hiyo jana mbele ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea Namibia alikokwenda kuhudhuria Bunge la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.
Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata kauli yake kuhusu sakata hilo, Makinda alimwomba amuulize siku za baadaye, ili aweze kupata maelezo kuhusiana na suala hilo kwa kuwa ndiyo amerejea nchini na hafahamu kitu chochote.
Taarifa ya Tansesco kwa umma mwishoni mwa wiki iliyopita, ilieleza kuwa shirika hilo linapaswa kuilipa Dowans fedha hizo huku Kampuni ya Richmond nayo inapaswa kuilipa serikali dola 1,201,933.08 za Marekani.
Taarifa hiyo ilibainisha Richmond ambayo iliishtaki TANESCO kwa kuvunja mkataba na kuikashfu, ilitaka ilipwe dola milioni 169, lakini TANESCO ndiyo iliyoshinda kesi hiyo, hivyo kustahili mabilioni hayo ya shilingi.
Aidha, Richmond nayo ilishinda kipengele cha kukashfiwa, hivyo kustahili kulipwa dola 50,000 za Marekani (zaidi ya sh 50,000,000).
Sakata la TANESCO kununua mitambo ya Dowans lilijadiliwa kwa kina huku wabunge wengine wakitaka inunuliwe na wengine isinunuliwe kwa kuwa ni mitumba, hata hivyo ombi hilo la TANESCO halikupata nafasi kwani Kamati ya Nishati na Madini, iliyokuwa chini ya William Shelukindo, ilipinga jambo hilo na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alihitimisha kwa kusema halitawezekana.
Katika hatua nyingine wanachama wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam jana walikwenda kumpokea na kumpongeza Makinda kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa Spika.
Akizungumza na wanawake hao jana, Makinda alishukuru kwa mapokezi hayo na kuwaahidi kuwa atafanya kazi yake kwa kujiamini na kamwe hatawaangusha.
Makinda alisema amechaguliwa kuwaongoza Watanzania wote, anao wajibu wa kutenda haki kwa wananchi ambao wamemchagua na haendi kufanya kazi ya mtu.
"Ushindi wangu umetokana na kura nyingi za wabunge ambao ni wawakilishi wenu na wangu, hivyo ninakwenda kutenda kazi ya wananchi kwa haki na si ya mtu," alisema Makinda.
Aidha, aliwataka wanawake hao kujikwamua kimaisha wao wenyewe kwa kutafuta mikopo na si kusubiria mabilioni ya Rais Jakaya Kikwete.
"Sasa hali ya maisha ni ngumu hivyo wanawake wenzangu ninawaomba mjipange vizuri kutafuta mikopo kwa ajili ya kuendesha maisha yenu, msisubiri mabilioni ya Rais …hata wabunge wanawake nao wafungue fursa.
"Mwanamke aliyejipanga vizuri hawezi kushindwa, kwani ushindi wa leo ni kampeni ya ushindi wa mwaka 2015," alisema.
Awali, akitoa salaam za wanawake hao, Mbunge wa Viti Maalum, Angela Kairuki (CCM), alisema wameamua kufanya hivyo kwa kuwa ameonyesha ujasiri na kwamba anapaswa kuigwa na wanawake wengine.
Kairuki alisema kutokana na majukumu aliyokuwa nayo sasa, wanawake wote nchini wanayo kila sababu ya kumlinda, kumsaidia kimawazo na kumuombea kwa kuwa ameonyesha mfano mzuri.
Katika mapokezi yao yaliyopambwa na matarumbeta, wanawake hao walimpa tuzo ya hongera kwa kupata nafasi hiyo na zawadi nyingine za mavazi.
 

Questt

JF-Expert Member
Oct 8, 2009
3,010
422
Its a nice move and HEKO kwa Kafulila ila kuliongela sasa ni kosa koz anampa muda wa Kujipanga kujibu mashambulizi....Yeye angmshitukiza kama kujikwaa ndo ingekuwa sawa...Si huyo tu wapo wengi...Waziri wa Maji/Umwagiliaji wote hawajafanya cha maana.....
 

mams

JF-Expert Member
Jul 19, 2009
614
30
Its a nice move and HEKO kwa Kafulila ila kuliongela sasa ni kosa koz anampa muda wa Kujipanga kujibu mashambulizi....Yeye angmshitukiza kama kujikwaa ndo ingekuwa sawa...Si huyo tu wapo wengi...Waziri wa Maji/Umwagiliaji wote hawajafanya cha maana.....

Ni kweli maisha bila umeme na maji ni hatari
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,039
728,455
Mbunge kuliomba Bunge limng'oe Ngeleja
Imeandikwa na Hellen Mlacky; Tarehe: 6th December 2010 @ 07:13 Imesomwa na watu: 23; Jumla ya maoni: 0


12_10_8hbzn0.jpg

Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR- Mageuzi, David Kafulila akisisitiza jambo wakati anazungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu hali ya mgawo wa umeme nchini.(Picha na Yusuf Badi).
MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR- Mageuzi, anakusudia kupeleka hoja binafsi katika Bunge la Februari 2011, kutaka Serikali iwajibike kwa kuliingiza Taifa hasara kwenye sekta ya umeme.

Hoja hiyo ya Kafulila imekuja siku chache baada ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kushindwa kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) na kutakiwa kuilipa Kampuni ya Dowans Sh bilioni 185 kwa kuvunja mkataba kinyume na sheria.

Katika hoja hiyo, Kafulila anataka Serikali aliyosema ndiyo inayopaswa kulipa deni hilo, kutoa maelezo ya kina ya sakata zima mpaka kufikia hapo, kwa sababu haitakuwa sahihi kulipa mabilioni ya fedha kwa kampuni aliyodai kuwa mmiliki wake hafahamiki.

Kafulila pia anakusudia katika hoja hiyo, kulitaka Bunge liazimie kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kwa madai kuwa ameshindwa kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati na Mpango Kabambe wa Usambazaji wa Umeme nchini.

Kwa mujibu wa madai ya Mbunge huyo, kushindwa kazi kwa Waziri huyo, kumesababisha kutokea kwa mgawo wa umeme nchini mara tatu ndani ya miaka miwili ya uongozaji wake.

Akizungumza jana katika makao makuu ya chama hicho Ilala jijini Dar es Salaam, Kafulila alisema kuwa mgogoro wa nishati ya umeme unaelekea kukomaa na kuwa sehemu ya maisha ya Watanzania.

Kafulila aliendelea kudai kuwa haitawezekana kufanikisha mpango wowote wa mapinduzi ya uchumi wala ya huduma nchini kwa kuwa takwimu zinaonesha asilimia 40 ya uchumi duniani inategemea nishati ya umeme.

Alidai chanzo kikubwa cha tatizo la umeme nchini ni Serikali kufumbia macho miradi ya umeme ya uhakika ambayo ingetoa majibu ya kudumu ya tatizo hilo na badala yake imebaki kusimamia sekta ya umeme kwa kudunduliza ikitumia mitambo ya kukodi ambayo alidai kwa miaka kadhaa sasa imekuwa ikinyonya vibaya uchumi wa Taifa.

"Asilimia 86 ya mapato ya Tanesco yanatumika kulipia umeme unaozalishwa na mitambo ya kukodi ambayo inazalisha takribani asilimia 45 tu ya umeme wote... hivi sasa mitambo ya kukodi inayotumika ni Songas na IPTL peke yake baada ya Agreko kumaliza mkataba wake na Dowans kufutwa mkataba," alidai.

Alidai Tanesco inalipa Kampuni ya Songas takriban Sh milioni 266 kila siku kwa kununua megawati 86 za umeme na mitambo ya IPTL ikiwa imewashwa, Tanesco inailipa kampuni hiyo Sh milioni 300 kila siku.

"Tangu mwaka 2006 Serikali imeshindwa japo kupunguza tatizo la mgao wa umeme huku viongozi wake hasa Waziri wa Nishati na Madini akipotosha Watanzania mara kadhaa kwamba Serikali inalishughulikia na mgao wa umeme utakuwa historia," alidai.

Alisema, Serikali inapaswa kuona athari ya matatizo ya umeme katika maendeleo kuliko hata mtikisiko wa uchumi na kuitaka ifanye maazimio magumu kwa kutenga fedha za kutosha kutekeleza mradi mkubwa wa umeme na wa uhakika kama wa makaa ya mawe Kiwira na gesi asilia ya Mnazi Bay.

Kafulila alisema miradi yote inaweza kuendeshwa na sekta binafsi iwapo kutakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na kuishauri mifuko ya hifadhi ya jamii iache kujenga majengo na ijielekeze katika uwekezaji wa uzalishaji umeme ili kutatua kabisa tatizo la umeme.

Alidai kwa kuwa Serikali ndiyo iliyoielekeza Tanesco iingie mkataba na Richmond na baadaye kuuhamisha mkataba huo kwa Kampuni ya Dowans na kwa kuwa Bunge ndio lilitoa azimio la kuvunjwa kwa mkataba na Tanesco ikafanya hivyo, shirika hilo lisibebeshwe lawama.

Gazeti hili lilimtafuta Ngeleja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema ili watoe ufafanuzi kuhusu hoja hiyo lakini hawakupatikana katika simu zao.

Hata hivyo Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah alisema ni mara yake ya kwanza kusikia Mbunge akitaka waziri mmoja, apigiwe kura na wabunge ya kutokuwa na imani naye.

Alifafanua kuwa kisheria waziri anaweza kupigiwa kura hiyo endapo yeye binafsi atakuwa na tatizo la kimaadili. Dk. Kashililah alisema katika tatizo la umeme, Waziri Ngeleja anaiwakilisha Serikali hivyo hoja hiyo ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani kwake, haiwezi kuelekezwa kwake binafsi na badala yake inapaswa kuelekezwa kwa Serikali nzima.slices_04.gif
slices_05.gif
 

Questt

JF-Expert Member
Oct 8, 2009
3,010
422
Jamaa hajaonyesha hata chambe ya Siasa....PURE uzalendo......safi kabisa Kafulila...these are things to discuss now....Vp tutatua tatizo la umeme.....yeye kaiongelea serikali kwa mabaya yake nami namuunga mkono kwa asilimia mia......
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,520
Tonge hilo limepokonywa midomoni mwa watu, Kafulila anaanza kupalilia upiganaji mapema!
 

MWANALUGALI

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
601
34
Kwanza huyo kafulia anakaribia kujifia kwa utapiamlo hata kabla hajalifikisha suala hilo Bungeni!! Huyo Bwana mdogo hana lolote zaidi ya kutaka attention na publicity tu! Nani atamuunga mkono na hoja yake hiyo bungeni? Zitto ameisha lambishwa kitu kidogo, CHADEMA amewatukana sana na haafikiani nao chochote, CUF ni CCM B na wala hawana interest na kitu chochote cha bara; Sasa ataungwa mkono na nani? Mwambieni aache utoto na akome kuanzisha threads kibao kwa majina tofauti ili aonekane onekane kama anaishi!!!!!!!
 

Michelle

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
7,376
2,816
Kwanza huyo kafulia anakaribia kujifia kwa utapiamlo hata kabla hajalifikisha suala hilo Bungeni!! Huyo Bwana mdogo hana lolote zaidi ya kutaka attention na publicity tu! Nani atamuunga mkono na hoja yake hiyo bungeni? Zitto ameisha lambishwa kitu kidogo, CHADEMA amewatukana sana na haafikiani nao chochote, CUF ni CCM B na wala hawana interest na kitu chochote cha bara; Sasa ataungwa mkono na nani? Mwambieni aache utoto na akome kuanzisha threads kibao kwa majina tofauti ili aonekane onekane kama anaishi!!!!!!!

Katika watanzania wenye akili duni,wewe ni mmoja wapo,nawe tafuta publicity kwenye masuala kama haya.sisi tutamuunga mkono Kafulila kwenye hili.Kafulila si Zitto na kamwe hatokuwa Zitto.USELESS!
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,039
728,455
SAKATA LA DOWANS: Spika Makinda apata kigugumizi


na Janet Josiah


amka2.gif
WAKATI Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) likiwa linajipanga kuilipa kampuni ya Dowans sh bilioni 185 kwa kosa la kuvunja mkataba, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda, ameahidi kulizungumza suala hilo baadaye. Makinda alitoa kauli hiyo jana mbele ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea Namibia alikokwenda kuhudhuria Bunge la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.
Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata kauli yake kuhusu sakata hilo, Makinda alimwomba amuulize siku za baadaye, ili aweze kupata maelezo kuhusiana na suala hilo kwa kuwa ndiyo amerejea nchini na hafahamu kitu chochote.
Taarifa ya Tansesco kwa umma mwishoni mwa wiki iliyopita, ilieleza kuwa shirika hilo linapaswa kuilipa Dowans fedha hizo huku Kampuni ya Richmond nayo inapaswa kuilipa serikali dola 1,201,933.08 za Marekani.
Taarifa hiyo ilibainisha Richmond ambayo iliishtaki TANESCO kwa kuvunja mkataba na kuikashfu, ilitaka ilipwe dola milioni 169, lakini TANESCO ndiyo iliyoshinda kesi hiyo, hivyo kustahili mabilioni hayo ya shilingi.
Aidha, Richmond nayo ilishinda kipengele cha kukashfiwa, hivyo kustahili kulipwa dola 50,000 za Marekani (zaidi ya sh 50,000,000).
Sakata la TANESCO kununua mitambo ya Dowans lilijadiliwa kwa kina huku wabunge wengine wakitaka inunuliwe na wengine isinunuliwe kwa kuwa ni mitumba, hata hivyo ombi hilo la TANESCO halikupata nafasi kwani Kamati ya Nishati na Madini, iliyokuwa chini ya William Shelukindo, ilipinga jambo hilo na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alihitimisha kwa kusema halitawezekana.
Katika hatua nyingine wanachama wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam jana walikwenda kumpokea na kumpongeza Makinda kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa Spika.
Akizungumza na wanawake hao jana, Makinda alishukuru kwa mapokezi hayo na kuwaahidi kuwa atafanya kazi yake kwa kujiamini na kamwe hatawaangusha.
Makinda alisema amechaguliwa kuwaongoza Watanzania wote, anao wajibu wa kutenda haki kwa wananchi ambao wamemchagua na haendi kufanya kazi ya mtu.
“Ushindi wangu umetokana na kura nyingi za wabunge ambao ni wawakilishi wenu na wangu, hivyo ninakwenda kutenda kazi ya wananchi kwa haki na si ya mtu,” alisema Makinda.
Aidha, aliwataka wanawake hao kujikwamua kimaisha wao wenyewe kwa kutafuta mikopo na si kusubiria mabilioni ya Rais Jakaya Kikwete.
“Sasa hali ya maisha ni ngumu hivyo wanawake wenzangu ninawaomba mjipange vizuri kutafuta mikopo kwa ajili ya kuendesha maisha yenu, msisubiri mabilioni ya Rais …hata wabunge wanawake nao wafungue fursa.
“Mwanamke aliyejipanga vizuri hawezi kushindwa, kwani ushindi wa leo ni kampeni ya ushindi wa mwaka 2015,” alisema.
Awali, akitoa salaam za wanawake hao, Mbunge wa Viti Maalum, Angela Kairuki (CCM), alisema wameamua kufanya hivyo kwa kuwa ameonyesha ujasiri na kwamba anapaswa kuigwa na wanawake wengine.
Kairuki alisema kutokana na majukumu aliyokuwa nayo sasa, wanawake wote nchini wanayo kila sababu ya kumlinda, kumsaidia kimawazo na kumuombea kwa kuwa ameonyesha mfano mzuri.
Katika mapokezi yao yaliyopambwa na matarumbeta, wanawake hao walimpa tuzo ya hongera kwa kupata nafasi hiyo na zawadi nyingine za mavazi.
 

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
10,692
6,455
Hivi huyu Anna Makinda ndo anatoa picha gani hapo???
Anasema kwamba ndo kwanza anaingia hivyo masuala ya DOWANS na TANESCO hayajafahamu vyemaq mpaka apate briefing.
Huu ndio mwenendo wa viongozi wetu kukwepa hoja. huwezi kuwa wewe ni kiongozi kwenye nafasi nyeti halafu ukiwa safarini usiwe briefed na yanayojiri kila siku nchini.
MAKINDA yupo kimaslahi zaidi.
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,520
Ni aibu kuwa hili tatizo licha ya kuwepo miaka nenda rudi, bado halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Only in Africa where you will this kind of foolishness.

Yes John McCain we hear you! Can we even measure the magnitude of foolishness to figure out if we are making any progress out of sheer foolishness?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom