JUkonga
Member
- Dec 30, 2015
- 14
- 13
MBUNGE WA UKONGA MH. MWITA M. WAITARA ATEKELEZA AHADI YAKE YA GENERETA LA TSH. 1MILIONI KWA SHULE YA MSINGI NZASA II KATA YA ZINGIZIWA:
Katika kutekeleza ahadi aliyoitoa mwaka jana kwenye ziara ya kutembelea shule za Msingi katika Jimbo la Ukonga, Mbunge Wa Ukonga
Mh. Mwita Waitara (Mb) amekabidhi Genereta lenye thamani ya TSH. Milioni 1.0 kwa ajili ya kusukuma Maji katika kisima cha Shule ya NZASA II.
Katika ziara hiyo Mh. Waitara aliambatana na Diwani wa Kata ya Zingiziwa Mh. Husein Togolo na Mwenyekiti wa Mtaa wa Nzasa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Chadema Kata ya Zingiziwa.
Kisima hicho cha maji kinawahudumia Wanafunzi, Waalimu na Wakazi wa maeneo ya jirani Shule ya Msingi NZASA II.
Akizingumza na wananchi hao Mh. Waitara aliwaambia kuwa ataendelea na juhudi za kihakikisha anapambana ili wananchi wa Kata ya Zingiziwa na Jimbo la UKONGA waweze kupata huduma muhimu za Jamii kama Maji, Elimu, Afya, Umeme na Miundomninu mizuri ya Barabara pamoja na Vivuko katika Kipindi chake cha Ubunge.
Pia mh. Waitara amewaahidi kuwawakilisha wananchi wa Ukonga vilivyo katika vyombo vya uwakilishi kama Bunge na Baraza la Halimashauri ya Manispaa ya Ilala ili kuhakikisha miradi Muhimu iliyotengewa fedha kwenye bajeti inatekezwa kwa wakati.
Wakiongea katika hafla hiyo ya kukabidhi Genereta, Waalimu, Wanafunzi na wakazi wa Mtaa wa NZASA walimshukuru Mbunge Mh. Waitara kwa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa na kumwahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika shughuli zake mbalimbali.
Mh. Waitara ametumia Sikuu ya Pasaka kutembelea maeneo mbalimbali ya Jimbo la UKONGA na kushiriki katika shughuli mbalimbali za jamii Katika Jimbo lake.