Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea ajitoa kugombea umakamu mwenyekiti wa CHADEMA, amuachia Lissu

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Wakati Kamati Kuu ikiendelea na uchujaji wa majina ya wagombea nafasi za Mwenyekiti na Makamu Wenyeviti CHADEMA Taarifa za hivi punde zinasema Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara Saed Kubenea amejitoa.

Kubenea amesema amejitoa kwa sababu anaamini mgombea mwenzake Tundu Lissu anafaa kushika nafasi hiyo.

=====

Habari Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amesema mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu anafaa kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho, hivyo amejitoa kugombania nafasi hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Desemba 18, Mwaka huu.
Screenshot_20191216-180704_Facebook.jpg
 
Kichaa kweli wewe.ninyi si mlisema ataishi ughaibuni.Saiz mnakula matapishi yenu moyo unakuuma ukisikia jina Tundu Lissu.Relax moyo usije kupata Tundu kwa sababu ya maumivu.
Kama kubenea kajitoa ndio Demokrasia yenyewe.Hata kujitoa ni Demokrasia ili mradi hajatishiwa ili ajiondoe.Kama amesoma alama za nyakati na na kuona kapitwa na upepo basi asubiri awamu ijayo kama upepo ukiwa sawia nae.CDM haitokufa Milele.
Tundu lisu atakuwa makamu mwenyekiti wa Chadema Marekani sio Tanzania bara.Katiba ya chadema imevunjwa kwa kuchagua mtu ambaye haishi Tanzania bara kuwa makamu mwenyekiti wa Tanzania bara!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe kwa sasa TL kajiridhisha kuwa kahikikishiwa usalama wake kama alivyotaka au office ya MM itakuwa overseas?
 
Tundu lisu atakuwa makamu mwenyekiti wa Chadema Marekani sio Tanzania bara.Katiba ya chadema imevunjwa kwa kuchagua mtu ambaye haishi Tanzania bara kuwa makamu mwenyekiti wa Tanzania bara!!!!

Kwani lissu ni raia wa wapi?
Huyo lisu wa marekani ni lisu gani coz lisu tundu yuko ulaya
 
Tundu lisu atakuwa makamu mwenyekiti wa Chadema Marekani sio Tanzania bara.Katiba ya chadema imevunjwa kwa kuchagua mtu ambaye haishi Tanzania bara kuwa makamu mwenyekiti wa Tanzania bara!!!!
Ibara ipi ya Katiba ya CHADEMA imevunjwa Chicka ?

Sent from my SM-A207F using Tapatalk
 
Hata kwa conference video cal si live au
Anatakiwa kuwepo mwenyewe mbele ya wajumbe katiba haizungumzii kuhojiwa kea Simu,barua pepe,Watsap au njia zingine za kidigitali Vinginevyo hata Vikao vya Kamati kuu kusingekuwa na haja wakutane wangefanya kwa teleconference.Yeye Kama atahojiwa kwa Watsap nk imekula kwake
 
Anatakiwa kuwepo mwenyewe mbele ya wajumbe katiba haizungumzii kuhojiwa kea Simu,barua pepe,au njia zingine za kidigitali Vinginevyo hata Vikao vya Kamati kuu kusingekuwa na haja wakutane wangefanya kwa teleconference

Kwa sababu za usalama wake, wanachama wameridhika na hilo, na hata hiyo kuwa live kidigitali ni sawa na uwepo wake vile vile.
 
Back
Top Bottom