Mbunge wa Ubungo John Mnyika anyimwa na polisi kufanya mkutano

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Feb 9, 2010
899
1,084
Polisi wamepiga simu kwa viongozi wa Chadema Ubungo kuzuia mkutano wa hadhara wa mbunge wa kueleza kazi za mbunge kwa mwaka mmoja pamoja na kupokea maoni ya wananchi kuhusu muswada wa katiba mpya usifanyike.

Sababu walizotoa polisi kwa simu ni kuwa kuna tishio la Alshabab. Polisi walipewa taarifa ya mkutano toka tarehe 3 wakakumbushwa tena tarehe 4 lakini hawakujibu.

Taarifa ndani ya Chadema zinasema kwamba mbunge ameamua kuendelea na mkutano kama kawaida kwa kuwa hakuna katazo la maandishi lililotolewa na polisi.

Mkutano unatarajiwa kuanza saa 10 jioni eneo la Ubungo mwisho pembeni ya stand ya daladala karibu na Yenu Bar.

Update

polisi yakamata gari na kuchukua nyaraka za katiba pamoja na viongozi wa chadema ubungo. Waweka rumande. Mnyika aendelea na mkutano bila vipaza sauti na kuzungumza na wananchi. Wananchi walaani hatua ya polisi, waamua kwenda na mbunge kituo cha polisi kuwatoa waliokamatwa na kudai nyaraka zilizochukuliwa
 
Jamani mimi mbona sielewi vizuri hapa, kwa nini serikali inaishi kwa mashaka namna hii?

Pia ni kwa nini Al-Shabaab ni threat sana kwa CDM zaidi hata ya CCM wala Serikali?

Kwa nini hakuna tishio la Al-Shabaab kwenye maadhimisho mbalimbali yanayofanyika zaidi ya mikutano ya CDM tu? Au kuna deal kati ya CCM na Serikali yake kwa kushirikiana na Al-Shabaab?

Mnaipa CDM umaarufu zaidi kwa gharama nafuu sana
 
Al-Shabaab threat should by no means be taken lightly.

The insurgents are said to have been angered by JK approval of Kenyan military invasion in Somalia and have pledged to carry out attacks in different major towns starting with DSM.

So we must help ourselves by trying to avoid entertaining political interests in such grave matters like nation security.
 
Hawa polisi yani akili yao wanawaza kuwakandamiza CHADEMA,Wapo kisiasa na wanatumika na mkoloni mweusi CCM.
 
duuh, mi nilidhani ulijivua gamba!!!! kwa nini makongamano ya miaka 50 yapo kila siku? ina maana hao alshaabab hawayaoni mpaka wavamie cdm walipo tu? kwani cdm ndiyo k? kama ni kuwaudhi basi jk ndiyo aliwaudhi, wangeanza na maazimisho ya 5o years of tz poverty!!!
Al-Shabaab threat should by no means be taken lightly. The insurgents are said to have been angered by JK approval of Kenyan military invasion in Somalia and have pledged to carry out attacks in different major towns starting with DSM. So we must help ourselves by trying to avoid entertaining political interests in such grave matters like nation security.
 
Jeshi la polisi limefanya vyema kuwataarifu wananchi mapema.
 
Polisi wamepiga simu kwa viongozi wa Chadema Ubungo kuzuia mkutano wa hadhara wa mbunge wa kueleza kazi za mbunge kwa mwaka mmoja pamoja na kupokea maoni ya wananchi kuhusu muswada wa katiba mpya usifanyike.

Sababu walizotoa polisi kwa simu ni kuwa kuna tishio la Alshabab. Polisi walipewa taarifa ya mkutano toka tarehe 3 wakakumbushwa tena tarehe 4 lakini hawakujibu. Taarifa ndani ya Chadema zinasema kwamba mbunge ameamua kuendelea na mkutano kama kawaida kwa kuwa hakuna katazo la maandishi lililotolewa na polisi. Mkutano unatarajiwa kuanza saa 10 jioni eneo la Ubungo mwisho pembeni ya stand ya daladala karibu na yenu bar.

"Siku moja nguvu ya umma itaishinda nguvu ya dola" by Dr.Slaa
 
Al-Shabaab threat should by no means be taken lightly. The insurgents are said to have been angered by JK approval of Kenyan military invasion in Somalia and have pledged to carry out attacks in different major towns starting with DSM. So we must help ourselves by trying to avoid entertaining political interests in such grave matters like nation security.
Katika hizi shuhuli za miaka 50 ya uhuru wa bendera na ktk ila mechi ya simba na yanga Alshabaab waliwapa taarifa polisi kuwa hawatafanya shambulio that why polisi haijazuia mikusanyiko hiyo kufanyika.
 
Hivi kwa nini serikali yetu inaishi maisha ya woga namna hii? Sasa inawaogopa mpaka wananchin wake!
 
Serikali badala ya kufanya kazi wako bize na cdm, hakika cdm ndo wanaongoza hii nchi! Vitu vidogo kama mkutano wa mbunge unawapa pressure je angekuwa kamanda Dr. Slaaka mwenyewe anafanyia pale jangwani nini kingetokkea?

Ukiona uchaguzi umeisha na sasa ni mwaka umepita lakini wananchi bado wanahangover ya uchaguzi na wengine wanatamani hata kesho uwepo uchaguzi basi ujuwe hawakuridhika na uchaguzi uliopita. Mbona 2005 uchaguzi ulipoisha kila mtu alikuwa kimya mpaka 2010? Hii inaashiria watu walipata mtu waliyempigia kura lakini uchaguzi uliopita ni wazi kabisa hawakumpata yule waliyekuwa wamemchagua.

Hivyo serikali watabaki kwenye tension ya kujihami na chadem mpka 2015 na hawatakaa wafanye kitu cha maana cha kuwavutia wananchi. Lakuvunda halina pafumu!
 
Waendelee na mkutano wao ila wawe makini kwani ccm na serikali yake walivyo sasa wanaweza kuwashambulia kwenye huo mkutano na wakawasingizia al-shabab. Nasema hilo linawekana na wala si lakupuuziwa.
 
Polisi wamepiga simu kwa viongozi wa Chadema Ubungo kuzuia mkutano wa hadhara wa mbunge wa kueleza kazi za mbunge kwa mwaka mmoja pamoja na kupokea maoni ya wananchi kuhusu muswada wa katiba mpya usifanyike.

Sababu walizotoa polisi kwa simu ni kuwa kuna tishio la Alshabab. Polisi walipewa taarifa ya mkutano toka tarehe 3 wakakumbushwa tena tarehe 4 lakini hawakujibu. Taarifa ndani ya Chadema zinasema kwamba mbunge ameamua kuendelea na mkutano kama kawaida kwa kuwa hakuna katazo la maandishi lililotolewa na polisi. Mkutano unatarajiwa kuanza saa 10 jioni eneo la Ubungo mwisho pembeni ya stand ya daladala karibu na yenu bar.

Hivi hili tishio la Alshababu lipo au litatokea pindi Chadema wanapofanya mikutano tu?Nna wasiwasi na polisi wetu hapa Tz kutumika vibaya hasa kwa matakwa ya viongozi walioko Serikalini.Mechi ya Simba na Yanga vipi mbona Alshababu hawakuwapo ktk kitisho hicho?
 
When the people fear their government, there is tyranny; when the government fears the people, there is liberty. “Thomas Jefferson”

Ni serikali ya ccm inataka watu waigope, wanatumia vyombo vya dola kutisha watu na kuweweka kwenye hali ya hofu kwa kisingizio cha Al-Shaab. Mbona kuna maonesho kila siku mnazo mmoja na watu wengi wanajitokeza?
 
Irrelevant argument since government of Tz and its people do not seem to fear each other but we are all fearing the common foe Al-Shabaab.
 
Hivi hili tishio la Alshababu lipo au litatokea pindi Chadema wanapofanya mikutano tu?Nna wasiwasi na polisi wetu hapa Tz kutumika vibaya hasa kwa matakwa ya viongozi walioko Serikalini.Mechi ya Simba na Yanga vipi mbona Alshababu hawakuwapo ktk kitisho hicho?
na nina uhakika John Mnyika hawezi kujaza watu wengi kama simba na Yanga....
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom