Mbunge wa TEMEKE, Abdallah Mtolea (CUF) alala Korokoroni, Bima ya gari yamponza

Hivi hizi jela zetu zipo kwa ajili ya rehabilitation au kukomoana?gari bila bima ni kosa la kukulaza ndani?polisi wetu naamini wanafundishwa jinsi ya kutumia busara wanapokabiliwa na mtuhumiwa mwenye hasira as far haatarishi usalama wa polisi,raia wengine na yeye mwenyewe,na kuendesha gari bila bima lina hasara zaidi kwa mwenye gari hasa linapohusika kwenye ajali sio kosa la kumpeleka mtu rumande,again narudia tunazidi kujenga chuki kati ya raia na polisi na kutengeneza generations ya ghasira,visasi na chuki,time will tell.
Kosa lolote la barabarani linaweza kukufikisha mahakamani mahabusu au jela kabisa. Mbunge lazima uwe mfano Kwani ndiye mtunzi wa sheria ni aibu Kwa mbunge kuendesha gari bila bima. Raia mwema hawezi kumchukia polisi bali atampenda sana lkn mhalifu ndiye humchukia polisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahyo mtu akitaka kufikishwA mahakamani mpk alale rumande kwa makosa ya barabaran?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Sipendagi kurumbana na polisi maana wanaweza kukulaza ndani ili wakuoneshe wao wanaweza kufanya hivyo.
Na ndio maana huwa wakinikamata nawaambia waniandikie au wachukue rushwa, kupotezeana muda kisa 30000 hapana

Tujitahidi kuwa makini maana hawa watu wana hasira na sifa juu
...Ubatakiwa ukamatwe kwa kutoa rushwa, tena kuhonga polisi.
 
Hawa jamaa afadhali wamngoje Lowasa awe rais kwani ataruhusu wananchi wote kutokufuata sheria na kuishi watakavyo. Wanachosha na makelele yao.
Cku ukitiwa ndani huyo rais wako atakuja kukuto, endelea kuita hoja makelele, kwan nani kakutuma kuchangia humu jf, soma kauli mbiu ya jf ujue humu wanatakiwa which kind of people... Cyo kila kitu unakuwa inzi tuu

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kwahyo mtu akitaka kufikishwA mahakamani mpk alale rumande kwa makosa ya barabaran?

Post sent using JamiiForums mobile app
Kosa ni kosa tu kulipishwa fine au kupelekwa ni uamuzi wa polisi anayekukamata lkn hata anayekamatwa ana haki ya kukataa kulipa fine na kutaka apelekwe mahakamani...juu sio wakati wa mazoea na kukariri sheria ni zile zile sio mpya bali zinatekelezwa kikamilifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona Mzee wa vijisenti Mh. Chenge aligonga mama muuza mchicha asubuhi kwenye bajaji, na gari yake haikuwa na Bima sikumbuki kama alilala korokoroni!!! Pamoja na kutoa roho! Je huyu Mh. Temeke Ametenda mbaya kuliko yule Mzee nyoka wa makengeza? Au kwa vile yeye ni mwenzetu na vijisenti vipo Vya kutosha kukwepa lupango.??? "Tumwogope Mungu malipo ni hapa duniani"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ANGEKUWA WA UPANDE WA PILI WALA ASINGEKAMATWA... Hivi ni kweli wabunge wa ccm ni watakatifu? Mana hawakamatwi
 
Tukisema CDM ni Genge la Wahuni tunakosea? Hata Mbunge Bima inamshinda?
Kwa hiyo chenge hakuwa na Bima na akaua asubuhi asubuhi na hata haijulikani alikuwa anataka wapi, ingawa ilisemekana baadae alikuwa ametoka kwa Mtaalamu kuchukua ungaunga wa kumwaga bungeni kupumbaza wenzake, sasa huyu tumwite nani kama mbunge wa cdm kukosa Bima ni mhuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa huyu mbunge dah ama kweli magufuri kazi anayo hapo akifungwa au akiwekwa sana ataambiwa ..... Mchwara imradi wapate kiki tu
 
Mwandishi wa habari hajafanya utafiti, maana kapewa taarifa za upande mmoja - polisi. Unajua taarifa za polisi huwa zinakanwa mahakamani?

Hata mimi nililiona hili...

Ni kwa sbb hata mimi mara nyingi nimekamatwa Bima ya gari yangu ikiwa imeisha muda wake...

Ni aidha polisi hunionya na kuniekekeza kulipia kwa kunipa muda kadhaa ama huongea nao tu "kiutu uzima" na kuyamaliza palepale..

Nina hakika hata kwa tukio la mbunge kuna kitu hakiko sawa. Nina hakika alikuwa anatafutwa kwa kitu kingine na ishu ya Insurance imetumika tu...

Wampeleke mahakamani kikajulikane hukohuko...
 
Back
Top Bottom