Mbunge wa TEMEKE, Abdallah Mtolea (CUF) alala Korokoroni, Bima ya gari yamponza

Kuna baadhi ya matukio wanayofanya wapinzani inakuwa tabu hata kuwatetea.....

Sasa kumtetea mbunge kwa makosa kama haya inakuwa tabu...
 
Hivi hizi jela zetu zipo kwa ajili ya rehabilitation au kukomoana?gari bila bima ni kosa la kukulaza ndani?polisi wetu naamini wanafundishwa jinsi ya kutumia busara wanapokabiliwa na mtuhumiwa mwenye hasira as far haatarishi usalama wa polisi,raia wengine na yeye mwenyewe,na kuendesha gari bila bima lina hasara zaidi kwa mwenye gari hasa linapohusika kwenye ajali sio kosa la kumpeleka mtu rumande,again narudia tunazidi kujenga chuki kati ya raia na polisi na kutengeneza generations ya ghasira,visasi na chuki,time will tell.

Huyu unayemtetea hakulala ndani kwa sababu ya gari kukosa bima, kalalazwa ndani kwa kudharau amri halali ya polisi... "Utii wa sheria bila shuruti" waujua?
Hii ndio shuruti sasa.
 
Siri kubwa ya kutosumbuliwa na askari wa usalama barabarani ni kuwa na kauli nzuri tu, hutakiwi kumuogopa askari wala kumjibu jeuri, ongea nae kirafiki huku mkitaniana kidogo, hatokukagua kitu chochote wala kukuomba rushwa na maisha yako yatakua mazuri tu. Traffic police ni watu waelewa sana ukitumia kauli nzuri anapokusimamisha.
 
Kama mbunge angetumia busara na lugha nzuri, badala ya kumkagua wangemuomba wapige nae selfie.
 
Na RAIA wengine wasiokuwa na Bima ya gari huwa wanawekwa korokoroni!!? Au ni huyu kwa vile si mwenzetu? na angekuwa ni Mh. Zungu angefanyiwa the same???! Let's treat each equally and not according to partisizim

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu tunapenda tu kulalamika lakini traffic case kwa nchi yetu Zipo poa sana, kama mh Mtolea angewasikiliza polisi wala isingefika huko ilipofika, tatizo ni kulifikilia jambo kwa upande mmoja tu kuwa huyu ni mpinzani,
Kama unamkumbuka yule mkurugenzi alietemeshwa kibarua na JPM ndani ya saa 24, kwa kumdharau askari polisi bahada ya kusimamishwa.
Pia unakumbuka sakata la mke wa waziri Maige, na hatua zilizochukuliwa juu yake?
Pia unakumbuka mh Sugu dereva wake alipomgonga mtoto kwenye zebra hadi kumsababishia kifo, yupo wapi......? maisha yanaenda kama kawa....
Msilalamike bila ya kukumbuka ya nyuma, huu utawala mwingine.
"TII SHERIA BILA SHURUTI"
 
Dah... Tutanyooka tu zama hizi.... "Unajua mimi ni nani? "

Sent from my chips yai using JamiiForums Mobile App
 
YEYE Mbunge aliondoka na kudharau police, umeelewa kilichoandikwa? Huenda angesikiliza police angepigwa faini tu ya kuendesha gari bila insurance, sasa kuwaacha traffic police ni kuwadharau na kudharau sheria za barabarani.

Lazima tuwe fair sana ktk kutii sheria, mbunge mzima anaendesha gari bila INSURANCE? Halafu anasimamishwa anahojiwa anawadharau police anaondoka zake?

Hii ni dharau sana na kuvunja sheria, Lazima tuwe makini while judging mtu akifanya kosa.

Dhana ya kuona wapinzani wanaonewa tu ni kosa..
Awamu kiwango chetu cha kufikiri kinaporomoka sana. Polisi akisema mtuhumiwa aliwadharau usikimbilie kuwaamini kuwa eti ni kweli wakati mtuhumiwa huna maelezo yake! Na ndio maana kuna mahakama ambako polisi wanapaswa kuthibitisha!
 
Hivi hizi jela zetu zipo kwa ajili ya rehabilitation au kukomoana?gari bila bima ni kosa la kukulaza ndani?polisi wetu naamini wanafundishwa jinsi ya kutumia busara wanapokabiliwa na mtuhumiwa mwenye hasira as far haatarishi usalama wa polisi,raia wengine na yeye mwenyewe,na kuendesha gari bila bima lina hasara zaidi kwa mwenye gari hasa linapohusika kwenye ajali sio kosa la kumpeleka mtu rumande,again narudia tunazidi kujenga chuki kati ya raia na polisi na kutengeneza generations ya ghasira,visasi na chuki,time will tell.
Sisi ni Tit for Tat...unamwaga mboga wao ugali unamwagwa hapohapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata siku moja usiamini maneno ya polisi.
Rejea kauri za zombe kama mnakumbuka
 
Sipendagi kurumbana na polisi maana wanaweza kukulaza ndani ili wakuoneshe wao wanaweza kufanya hivyo.
Na ndio maana huwa wakinikamata nawaambia waniandikie au wachukue rushwa, kupotezeana muda kisa 30000 hapana

Tujitahidi kuwa makini maana hawa watu wana hasira na sifa juu
Dawa ni kutokufanya makosa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom