Mbunge wa Tarime Nyagwine Nyambari na Mauaji ya Nyamongo

Wana JF,

Naomba kufahamishwa hivi hali ya Tarime kuhusu mauaji inaendeleaje? Manake sijui kinachoendelea, nani anafanya utaratibu wa Mazishi CDM au serikali? Timu iliyotumwa na Mbowe ya Tundu Lisu na Marando wanasemaje?
 
Nyie wenyewe chadema mlichemka kumleta Waitara alikua hakubaliki hata kidogo...Mwera angeteta hilo jimbo bila shida ama hata heche
 
hivi kale kaduka kake pale mtaa wa Livingstone na Ukami hajakafunga tu duH? Na bado mara kibao anashinda pale kwenye ofisi yake mkabala na Lion Hotel Sinza. Wana Tarime mkimtaka mbunge wenu njooni pale Lion Hotel Sinza, Kariakoo mtaa wa Mkunguni na Ukami au Pale jogoo kwenye nyumba yake ya ghorofa moja sawaaaaaaaa!!!!!

Au kwa msaada mwambieni arudi Tarime tena mumtwangie kwa namba 0773 959 500 ingawa itaita weeeeee bila kupokelewa mpaka atakapojisikia mwenyewe tehtehtehteh
 
kumbe ndiko anakopatikana na saizi ana tigo hata ukimpigia apokei hata roadland wake kuna siku kamtafuta sana kwa kumpigia simu akawa apokei na wapambe wake waliokuwa wanamsaidia kawakimbia na line kawabadilishia wana usongo naye aliwapromic kuwapa kazi na pesa kama mitaji ajaonekana mpaka leo na swala la weitara alishinda sema waliiba mmkuu lakini siyo kwamba alikuwa akubaliki ni wizi ulifanyika mkubwa sana na madhala yake ndo hayo ya nyambari kupigwa mawe kwa sababu siye waliyemchagua
 
Nyie wenyewe chadema mlichemka kumleta Waitara alikua hakubaliki hata kidogo...Mwera angeteta hilo jimbo bila shida ama hata heche

kama ni kweli point taken, inabidi chdema wasitumie ubabe kama wa ccm, kama mtu hakubaliki hakuna haja ya ku force mnaona mnapoteza majimbo nyeti kama haya
 
tafuta lingine la kuongea hapo ni pontiless kwa hiyo angekuwa na nhyumba tarime ingekuwaje tafuta la maana kultea kwenye meza
 
Kwanza itaundwa TUME ajili ya kuandaa mchakato wa kuunda TUME ya kuchunguza.
Hizi tume zinaundwa kimasilahi zaidi.
Stay tuned.
 
SAKATA la Mbunge wa Tarime, Nyangwine Nyambari (CCM) la kudaiwa kutoa lugha ya matusi kwa wanachama wenzake na wapiga kura wakati akihutubia mkutano wa hadhara wiki moja iliyopita wilayani hapa limechukua sura mpya baada ya chama chake kuibuka na kudai "matusi ya mbunge huyo yasichukuliwe kuwa matusi ya chama."
Badala yake chama hicho kimelaani matumizi ya lugha za matusi zinazotolewa na baadhi ya makada na viongozi wake kwa maelezo kuwa kauli kama hizo zinachochea chuki na migawanyiko ndani ya chama na wananchi kwa ujumla.
Mwenyekiti wa CCM wilayani hapa, Rashid Bogomba, amewaambia waandishi wa habari mjini hapa leo kuwa wanalaani kwa nguvu zote kauli zilizotolewa na mbunge huyo na kusisitiza kuwa zilikuwa ni kauli zake binafsi na hazikuwakilisha chama hicho.
"Sisi kama chama hatuungi, hatujawahi na hatutawahi kuunga mkono kauli kutoka kwa mtu yeyote mwenye itikadi yoyote kutumia lugha zinazoashiria matusi wala uchochezi kwa wananchi na kwa sasa tunachukulia kauli ya mbunge wetu kama yake binafsi na si vinginevyo," alisema mwenyekiti huyo.
Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na taarifa kuwa jitihada za vikao vya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mara CCM vilivyofanyika wiki hii kujaribu kumnusuru mbunge huyo kwa kumtaka aombe radhi kwa wananchi zilishindikana.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya chama hicho kililidokeza gazeti hili kuwa mbunge huyo aligeuka mbogo kwa wajumbe baada ya kutamba kuwa yeye ni shujaa aliyelikomboa jimbo hilo kutoka kwa wapinzani hivyo wamuache hivyo hivyo.
"Unajua mwandishi, mbunge aliwageukia wajumbe kwa kuwaeleza ugumu aliopata katika kukomboa Jimbo la Tarime lililokuwa ngome ya CHADEMA na kudai alitumia nguvu na rasilimali nyingi kiasi cha kuwabwatukia wajumbe kuwa wamwache jinsi alivyo," alieleza mtoa taarifa wetu.
Wiki iliyopita mbunge huyo akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Sabasaba wilayani hapa alitoa kauli iliyoonekana kuwa ya matusi kwa wapinzani wake kutoka ndani na nje ya chama chake kwa kudai kuwa wote waliompinga wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wakimuita mbunge wa briefcase waende wakawaambie hivyo mama zao. "Briefcase ni mama zenu," alisikika akisema hivyo mbunge huyo wakati wa hotuba yake hiyo.
hapo katika nyekundu alimaanisha rushwa, yaani yeye ameteketeza pesa zake kwa kununulia watu pombe kanga na pilau kisha anatokea mtu mwingine na kuanza kumzingua, sinema inaendelea.....................
 
Wana JF,

Naomba kufahamishwa hivi hali ya Tarime kuhusu mauaji inaendeleaje? Manake sijui kinachoendelea, nani anafanya utaratibu wa Mazishi CDM au serikali? Timu iliyotumwa na Mbowe ya Tundu Lisu na Marando wanasemaje?

Hapatoshi cdm watasimamia mazishi serikali imepeleka magari ya maji ya kuwasha, af nasiki aviongozi wa cdm watahutubia kabla ya mazishi kwenye uwanja wa sabasaba hii imekuja baada ya serikali kugonga mwamba kwa kuwataka wafiwa wachukue maiti zao na kuzika kabla ya uchunguzi wa kisheria kukamilika. Pia Marando na Tundulisu wanataka kusimamia madai ya wanatarime sambamba na wanasheria wa kituo cha LHRC ambao pia wameahidi kuwapigania wanatarime. Cdm wamesema hawaogopi vitisho vya polisi lazima shughuli ziendeshwe kama zilivyo pangwa.
 
Huyu jamaa kapoteza dira nadhani hapa nimepata weakness moja wapo ya katiba yetu, jamaa kama huyu kachuja katiba ingeturuhusu angepigwa chini sio mpaka miaka 4 pite ina pain sana.
 
Mimi simemi kitu mpaka briefcase itakapokuwa mama zao, nimepita tu hapa naelekea nyamongo kwenye mazishi.
 
Mgodi wa Nyamongo uko karibu sana na wananchi. Nnavojua wawekezaji lazima wanatoa pesa ya kuwapa wenyeji na fidia zingine lakini UJAMBAZI wa watumishi wa serikali inayoyelelewa na serikali ndiyo chanzo kikubwa cha matatizo. Watendaji wa serikali ndio wanawadhulumu wananchi pesa zao hata Geita ni hivo hivo. Walionufaika na pesa zilizotolewa na AShantiGoldfields ni watumishi wa halmashauri ya Geita, mkuu wa wilaya kipindi hicho bi Halima Kiemba, mkurugenzi wa halmashauri, wafanyabiashara wa mjini Geita, watu wa benki na viongozi wa mahusiano ya jamii katika kampuni ya Ashanti.
Cha ajabu serikali inakuwa inajua kabisa uchafu na udhalimu huu lakini haichukui hatua zozote. Mpaka sasa Geita kuna watu walihamishwa mgodini tangu miaka ya tisini lakini wajanja walikula pesa zao wakawaacha hawana makazi. Mpaka sasa hawa watu wanaishi kwenye kambi wamechoka kuliko wakimbizi. Wamejimbaza tu kwenye kijumba ambacho zamani kilikuwa mahakama enzi za ukoloni; halina madirisha wala milango. Kwa kuwaonea huruma kanisa la AIC limewapa mahema ambayo wameyawekea kambi karibu na hilo jengo la mahakama. Unaweza imagine inakuwaje mtu ana familia kuishi kwenye hema lisilozidi urefu mita mbili.
Huo mchezo ndio uliochezwa Nyamongo pia na kwa vile mgodi wa Nyamongo uko karibu na watu kilichotakiwa ni kuhamisha kabisa mji huo kuuweka sehemu nyingine. Nchi zingine wawekezaji wanawajengea wenyeji nyumba sehemu nyingine na kuwalipa fidia.
Hapa kwetu sheria ni mbovu eti ardhi haitathminiwi kwa mali iliyoardhini ila zile zile zilizoko juu ya ardhi kama nyumba, mimea na hata kama ardhi hujailima na kuwa na kitu juu yake haihesabiwi. Hizi ni sheria zilizotungwa na wakoloni kuwanyonya waafrika na serikali za kiafrika hasa Tanzania ilizing'ang'ania kuendeleza huo unyonyaji wa kikoloni.
Kinachotakiwa ni kuwalipa wananchi wa Nyamongo, kuwatafutia njia mbadala za kiuchumi na kuwahanisha kwenye makazi mengine bora.
Lakini pamoja na hayo yote haiwapi wananchi wa Nyamongo uhalali wa kuingilia shuguli za mgodi kwa kuvamia kwa lengo la kuiba dhahabu. Hawa watu wanapoingia mgodini wanaingia kivita kabisa. Nikifika hapo sina utetezi kwao kwani ni wezi kama walivo wezi tunaowachoma moto au wezi wa ng'ombe tunaowadunga mishale na mikuki huko kwetu. Watu watalaumu polisi wametumia nguvu kupita kiasi lakini ungetegemea wangefanya nini? Wangekimbia? Hawa sio waandamanaji wanaotembea kwa amani kudai kutoa malalamiko yao kama ilivokuwa Arusha. Hawa ni wezi. Sisi tunaokaa katika mazingira hayo tunaelewa. Ukuriani wizi uwe wa ng'ombe au katika mazingira ya madini kama Nyamongo huchukuliwa kama utafutaji hivo hulindwa na hata serikali ya kijiji. Mfano watu wameenda kuiba sehemu nyingine na kuleta ng'ombe wa wizi kijijini, wenye ng'ombe wakiwafuata ng'ombe na kuwakuta wenyeji wa kijiji ikiwemo serkali ya kijiji watapigana vita na wenye ng'ombe. sio wezi tu wanawajibika kuwalinda ngombe waliowaiba ikiwa ni pamoja na kupigana vita na kuuana ila kijiji kizma sasa kinaingilia kuwasaidia wezi wao walioleta ng'ombe wa wizi kijijini.
CDM isiingie kichwa kichwa kuwasupport wezi ambao wangestahili kwenda gerezani ila wanalindwa na hayo mazingira niliyoyaeleza hapo juu.

Sio lazima uchangie kila thred, ama kila unachokiona na kukisoma. Na kama kitu hukifahamu vizuri usijifanye mjuvi ili uonekane unajua ama umechangia, wakati mwingine unatakiwa usome mawazo wa wenzako wenye ufahamu wa jambo husika.
Kujifanya mjuvi wa mambo ambayo umesimuliwa, hujawahi kuishi ama kufika neo husika, ama ndo ile mtu unakwenda unakaa siku moja unaondoka na kujifanya umekaa tarime na unawafahamu sana wakurya na tabia zao. Huo mimi nasema ni upumbavu kuja hapa kushabikia vifo vya watanzania wenzetu wasio na hatia na kuwaita wezi. Yani umekaa nyumbani kwako unamsikiliza kagasheki anaongea utumbo na wewe unakuja hapa kushadidia kwamba ni wezi.

Tangu lini polisi wa tanzania wakawa na jeuri ya kupambana na wezi achilia mbali majambazi, kila siku tunashuudia polisi wakiwaua raia wema wasio na hatia na wasio na silaha za moto. Mbona majambazi wanapovamia kwenye mabenki, maduka na migodini huwa hawawezi kupambana nao hadi kuwaua? ni matukio mangapi yanayodhihirisha kwamba polisi wetu wanaonekana kutenda kazi wanapokabiliana na raia wasio na silaha?maandamano ya arusha raia walikuwa na silaha?mauaji ya mbarali wananchi walikuwa na silaha za moto? mauaji ya arusha mwaka jana wale vijana wawili walikuwa na silaha? mauaji ya raia ukerewe polisi walikuwa wapi? mauaji ya majambazi mwanza wananchi si ndio waliwaua ndipo baadae polisi wakajitokeza
kuwashukuru wananchi? ni wapi polisi wameweza kupambana na wezi ama majambazi?
Halafu usivyokuwa na akili unasema chadema isiwasupport wezi! watu wengine hamnazo kabisa!yani serikali imeua raia wake, halafu kabla hata uchunguzi haujafanyika inawalazimisha wazike, ili iweje? wanataka kuficha nini? wafiwa wenyewe kuwaomba chadema wasimamie uchunguzi wa miili ya marehemu ni kutokana na imani waliyonayo kwa viongozi hao na chama chao. Sasa nakushangaa unakuja hapa na stori za vilabu vya wanzuki kujaribu kupotosha watu. Achana kabisa na watu wa nyamongo wala hawahitaji mawazo yako wala ushauri wako, wao wanaishi maisha yao na wewe endelea kuishi maisha yako. Wataendelea kupigania maisha yao na rasilimali zao hata kama polisi wenu wataendelea kuwapiga risasi na kuwaua lakini utafika wakati watakubali kwamba nyamongo si bulyanhulu wala buzwagi ama geita, haki ya wananchi wale itapatikana tu, iwe kwa hiari ama kwa nguvu!!
 
Chanzo cha mgogoro Tarime chaelezwa


Nyaronyo Kicheere


BAADA ya mauaji ya watu saba wilayani Tarime mahali ambapo kampuni ya Barrick Afrika Gold inaendesha shughuli za uchimbaji dhahabu yametokea malumbano baina ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), serikali na Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine, kwa upande mmoja na wananchi kwa upande mwingine.
Mbunge Nyangwine, anadai alifuatana na wenzake waliotoka kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, aliye ziarani mkoani Mara, Willson Mukama, ambao hawakupata nafasi kuvua sare za CCM. Kama nitakavyojadili hapa huu ni uongo mtupu.
Pia Nyangwine anadai kupigwa kwake mawe na wananchi kumetokana na uchochezi wa kisiasa na akasisitiza kuwa si vizuri watu wengine kutumia matatizo ya wananchi kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
Ushahidi uliopo ni wa CCM kufurahia misiba na kujinufaisha nayo. Mbagala kwenye mabomu makada wa CCM walivaa sare wakajidai kutoa msaada lakini wakatoweka na mahema, maharage, sabuni, mafuta ya kupikia na mchele vyote msaada wa waathirika wa mabomu.
Pia kwenye msiba wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Katibu Mkuu wa TANU na CCM na Waziri wa Ulinzi, Simba wa Vita, Hayati Rashid Mfaume Kawawa, makada wa CCM walikuja na sare zao na kugeuza msiba wa kitaifa kuwa msiba wa CCM! Mbaya sana hii.
Siku ya Jumatano Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Kaghasheki, alidai eti kuna chama kimoja cha siasa kinatumia msiba huo wa Tarime kujinufaisha kisiasa na kwamba chama hicho kilikuwa kinawazuia wafiwa kuchukua maiti za wapendwa wao na kuzizika.
Ilipofika Alhamisi Kaghasheki akageuza kibao akidai kwamba vurugu za Tarime zimesababishwa na uchochezi unaofanywa na mbunge mmoja wa chama kimoja cha siasa kutoka mkoa wa mbali ambaye katembelea eneo hilo la mgodi.
Hesabu zangu zinaonyesha polisi wameua watu wengi sana tangu mgodi huo uanze. Nilipoacha kuhesabu walikuwa wameshauawa watu 70! Je mara zote hizo polisi walipokuwa wanaua watu ilisababishwa na mbunge kutoka nje ya mkoa kuchochea mauaji?
Hawa wote ni waongo kwa sababu wanaujua ukweli lakini hawataki kuusema ukweli huo. Hawa ni viongozi ambao kama wenzao walio wilayani Tarime wanazungumza lugha ya kampuni inayochimba dhahabu pale ya Barrick Africa Gold. Viongozi hawa hawaielewi lugha inayozungumzwa na wananchi.
Nitajaribu kusema lugha ya wananchi kwa kueleza mambo 12 ambayo hayabishaniwi na mtu yeyote awe Barrick, serikali, viongozi wa CCM, polisi wala Wizara ya Nishati na Madini.
Kwanza; Barrick haina kitalu hata kimoja kinachochimbwa dhahabu pale Nyamongo kwa sasa. Maeneo yote yanayochimbwa dhahabu ni vitalu vya vijiji vya Nyangoto, Nyamwaga, Genkuru, Kerende na Kewanja. Kitalu kingine ni mali ya Chacha Msabi maarufu kama Keng'anya Enterprises.
Pili; vijiji hivyo vilikabidhi hati za vitalu vyao vya kuchimba dhahabu kwa kampuni ya Afrika Mashariki Gold Mines ambayo iliuza kwa kampuni ya Placer Dome ambayo nayo iliuza kwa mwekezaji wa sasa Barrick Africa Gold inayomiliki mgodi wa North Mara Gold Mine Limited.
Tatu; kwamba makabidhiano ya hati hizo yalifuatia mazungumzo na makubaliano yaliyotiwa sahihi na wahusika wote kuwa kampuni hiyo ya uchimbaji dhahabu italipa asilimia moja ya mapato yake kutoka eneo la kijiji lililochimbwa na kampuni yenyewe kuchangia asilimia nyingine moja.
Nne; kwamba kulingana na makubaliano hayo kampuni ilipaswa kuunda mfuko wa dhamana (Trust Fund) ambao ungewekwa fedha hizo kwa sababu ni nyingi na kwamba kampuni nayo ingechangia asilimia moja kwa kila asilimia moja ya vijiji.
Tano; ni kwamba kampuni ya Keng'anya Enterprises inayomiliki eneo maarufu la uchimbaji wa dhahabu la Gokona nayo itapata asilimia moja ya mapato na itachangia asilimia moja ya kipato chake kwenye mfuko wa dhamana na kampuni nayo ingechangia asilimia nyingine moja kwenye mfuko huo.
Sita; ni kwamba miongoni mwa masharti ya vijiji na Keng'anya kukabidhi hati za vitalu vyao kwa kampuni ni kila kijiji na Keng'anya kuteua mwakilishi mmoja mmoja atakayewawakilisha kwenye uchimbaji na kukagua mahesabu kuhakikisha havidhulumiwi na kampuni.
Saba; ni kwamba kutokana na Barrick kutotekeleza mapatano hayo kesi mbili zilifunguliwa na Keng'anya Mahakama Kuu ya Tanzania akiwakilishwa na Wakili maarufu nchini Saidi Hamad el Maamry.
Kesi hizo ni Civil Case No. 298 ya 1997 na Civil case No. 315 ya 2002 ambazo kwa kujua haiwezi kushinda Barrick ilitafuta mwafaka nje ya mahakama na mwafaka huo kusajiliwa mahakamani kama uamuzi wa mahakama wa Desemba 15, 2004.
Nane; ni kwamba hadi leo hii pamoja na Barrick kuchukua hati za vijiji na kuchimba tangu 2004 haijaanzisha, haijaunda wala kusajili mfuko wa dhamana na kwa maana hiyo Barrick haijawahi kuvilipa vijiji hivyo chochote kulingana na mkataba uliowezesha ipate kibali cha kuchimba eneo hilo.
Tisa; ni kwamba hadi leo hii si vijiji wala Chacha Msabi kwa maana ya Keng'anya Enterprises aliyechagua au aliyeteua mtu anayekagua mahesabu na kuhakikisha kiasi cha dhahabu inayochimbwa! Barrick wanajichotea tu na kusafirisha makwao.
Kumi; ni kwamba viongozi karibu wote wa CCM na serikali wilayani Tarime ambao wangesaidia wananchi kwenye mgogoro na mgodi wamepewa tenda mgodini na hivyo hakuna hata mmoja anayewasikiliza wananchi.
Hii ndio sababu Barrick inatumia hati za vijiji kuchimba dhahabu lakini hailipi asilimia moja kama ilivyokubaliwa na hakuna anayefanya chochote badala yake Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele, anavilazimisha vijiji eti vipokee dola za Marekani 100,000 ili viingie mkataba mwingine na Barrick na kuacha madai yao yote! Huu ni upuuzi mtupu.
Mbaya zaidi ni jambo la 11 lisilobishaniwa kwamba hadi leo hii hakuna kiongozi hata mmoja wa CCM, serikali, polisi wala kiongozi wa halmashauri ambaye alifika Nyamongo na kuongea na wananchi kabla ya kuongea na uongozi wa mgodi.
Wote wanaofika Nyamongo (ukiondoa viongozi wa CHADEMA) huingia mgodini kwanza wakazungumza, wakaelekezwa, huenda pia wakapewa chochote kabla ya kutoka nje na kuuliza wananchi wana matatizo gani na mgodi!
Hata Rais Benjamin Mkapa alipofika Nyamongo aliingia mgodini na kutoka akatokomea bila kuonana na wananchi. Mbaya zaidi siku hiyo wananchi 60 walikamatwa wakawekwa ndani na waliachiwa baada ya Mkapa kuondoka!
Kumi na mbili; ni kwamba mgodi wa Barrick ndio wenye polisi na umewaamuru kumkamata mtu yeyote anayekutwa na mawe ya dhahabu na kumnyang'anya na imewahi kutokea mashine na mali za wachimbaji kuharibiwa na polisi kwa amri ya Barrick.
Ikumbukwe kwamba asilimia 60 ya wakazi wa Nyamongo ni wachimbaji katika maeneo ya Tigite, Nyankuru, Kerende, Mosege, Komarela, Monanka na Nyabikondo.
Sasa swali ni kwa nini watu wasiwe na mawe ya dhahabu au mashine za kusagia kama wachimba dhahabu? Na wakikutwa nayo wanyang'anywe na polisi kwa amri ya Barrick?
La kumi na tatu la kufungia kazi ni kwamba uvamizi wa mgodi hufanywa na polisi katika kitu kinachoitwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Mchongo'.
Kuna mchongo wa OCS, kuna mchongo wa OCD, kuna mchongo wa OC-CID, kuna mchongo wa RPC, RCO na kadhalika.
Kunapokuwepo mchongo kinachotokea ni kwamba wananchi waliotoa pesa au waliokubaliana na polisi hupakiwa kwenye gari la polisi na kuingizwa mgodini kuchimba dhahabu na mapato hugawiwa kwa waliolipa pesa na kiasi kikubwa kwa mwenye mchongo.
Vurugu hutokea kama wakati mchongo unaendelea wananchi wengine wanapata habari na kukimbilia kuchanganyika na waliopangwa kwenye mchongo huo. Hapo polisi huingilia kutaka kuwazuia wale ambao hawakuwemo kwenye mchongo tangu mwanzo.
Kwa sababu jambo lenyewe linakuwa la siri na polisi hawataki kufahamika kama ndio chanzo cha mchongo ule hulazimika kutumia nguvu ikiwamo kupiga risasi wananchi ambao hawakuwamo kwenye mchongo tangu mwanzo.
Nimeambiwa kuwa uongozi wa polisi unalijua hili na unanufaika; ndiyo maana mauaji Nyamongo hayaishi.
Pia michongo hii inafahamika hata Ikulu kwa sababu walifahamishwa kwa barua maalumu ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyangoto Elisha Marwa.
Mwenyekiti huyo alipotaja hadharani mkutanoni kuwa polisi ndio chanzo cha mgodi kuvamiwa alifuatwa na polisi, baadaye nyumbani kwake akapigwa karibu kufa; aliponea Mwanza, hosptalini Bugando. Alipopona ndipo akaandika Ikulu kulalamika.
Mimi Nyaronyo Mwita Kicheere namtaka anayebisha hili la polisi kuwa chanzo cha kuvamiwa mgodi aitishe mdahalo wahudhurie wenyeviti wa Nyangoto, Kerende, Matongo, Kewanja, Nyamwaga, Nyakunguru, Genkuru, Mrito, Nyarwana na Gibaso.
Pia katika mdahalo huo wahudhurie polisi na wachimbaji wadogowadogo wa Nyamongo ambao nina uhakika watatoa ushahidi namna wanavyovalishwa magwanda ya polisi na kofia waonekane kama polisi ndipo waingizwe mgodini kuchimba dhahabu!


Source: Tanzania Daima, 20/05/2011
tuyafukue upya e?
 

Attachments

  • VID-20180712-WA0016.mp4
    13.1 MB · Views: 11
Back
Top Bottom