Mbunge wa Tarime Nyagwine Nyambari na Mauaji ya Nyamongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa Tarime Nyagwine Nyambari na Mauaji ya Nyamongo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 13, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  SAKATA la Mbunge wa Tarime, Nyangwine Nyambari (CCM) la kudaiwa kutoa lugha ya matusi kwa wanachama wenzake na wapiga kura wakati akihutubia mkutano wa hadhara wiki moja iliyopita wilayani hapa limechukua sura mpya baada ya chama chake kuibuka na kudai “matusi ya mbunge huyo yasichukuliwe kuwa matusi ya chama.”
  Badala yake chama hicho kimelaani matumizi ya lugha za matusi zinazotolewa na baadhi ya makada na viongozi wake kwa maelezo kuwa kauli kama hizo zinachochea chuki na migawanyiko ndani ya chama na wananchi kwa ujumla.
  Mwenyekiti wa CCM wilayani hapa, Rashid Bogomba, amewaambia waandishi wa habari mjini hapa leo kuwa wanalaani kwa nguvu zote kauli zilizotolewa na mbunge huyo na kusisitiza kuwa zilikuwa ni kauli zake binafsi na hazikuwakilisha chama hicho.
  “Sisi kama chama hatuungi, hatujawahi na hatutawahi kuunga mkono kauli kutoka kwa mtu yeyote mwenye itikadi yoyote kutumia lugha zinazoashiria matusi wala uchochezi kwa wananchi na kwa sasa tunachukulia kauli ya mbunge wetu kama yake binafsi na si vinginevyo,” alisema mwenyekiti huyo.
  Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na taarifa kuwa jitihada za vikao vya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mara CCM vilivyofanyika wiki hii kujaribu kumnusuru mbunge huyo kwa kumtaka aombe radhi kwa wananchi zilishindikana.
  Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya chama hicho kililidokeza gazeti hili kuwa mbunge huyo aligeuka mbogo kwa wajumbe baada ya kutamba kuwa yeye ni shujaa aliyelikomboa jimbo hilo kutoka kwa wapinzani hivyo wamuache hivyo hivyo.
  “Unajua mwandishi, mbunge aliwageukia wajumbe kwa kuwaeleza ugumu aliopata katika kukomboa Jimbo la Tarime lililokuwa ngome ya CHADEMA na kudai alitumia nguvu na rasilimali nyingi kiasi cha kuwabwatukia wajumbe kuwa wamwache jinsi alivyo,” alieleza mtoa taarifa wetu.
  Wiki iliyopita mbunge huyo akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Sabasaba wilayani hapa alitoa kauli iliyoonekana kuwa ya matusi kwa wapinzani wake kutoka ndani na nje ya chama chake kwa kudai kuwa wote waliompinga wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wakimuita mbunge wa briefcase waende wakawaambie hivyo mama zao. “Briefcase ni mama zenu,” alisikika akisema hivyo mbunge huyo wakati wa hotuba yake hiyo.
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,853
  Likes Received: 11,974
  Trophy Points: 280
  'Briefcase ni mama zenu' hii ni kali ya mwaka ingetolewa na wapinzani nafikiri ungekuwa wimbo wa taifa wa Chiligati na Makamba na So...e.
   
 3. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  "Briefcase ni mama zenu" hahahah. Hii imenikumbusha enzi za Dr. Slaa (CDM) na Quoro(CCM) kule karatu 1995!
  Wakati wa kampeni Quoro aliwambia wananchi maendeleo yaliyoletwa na CCM wananchi hawawezi kuyaoma mpakwa atakapolala na mama zao!!
   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa alitaperiwa kama milioni 70 na taperi wa Ikulu kuwa angepata Uwaziri, sasa nadhani kachanganyikiwa maana kaanza moja kabisa hana kitu.
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Sasa wameanza matusi, tena mapema hivi! Kuna kazi.....
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  teh! Huyo hayo matusi nadhan hakusikia vyema pindi anayatoa, wenge mtafuna wale duh! Huyo Mb. shenzi sana!
   
 7. emmathy

  emmathy Senior Member

  #7
  Mar 13, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  yakitoka chadema wanasema chadema wachochez , chadema hakifai ila sababu ni ccm wanasema ni lambunge mwenye kama walivyosema ufisadi niwamtu mwenyewe sio la chama-kaz kwelikweli
   
 8. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  kumbe matusi kwa chama tawala ni ruksa ila wapinzani wakitukana wanashkiwa bango.................
   
 9. Bushloiaz

  Bushloiaz JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  No wonder anatembea na bodyguard siku hizi ,nilikutana nae sehemu moja musoma yuko na vijana am sure ni wa uwt wanamlinda
   
 10. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yeye ni mkurya lakin hawajui wakurya hata miaka 5 anaweza asiimalize
   
 11. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  huyu bwana mbunge kapinda kabisa bora arudi kuandika vitabu vya kiswahili auzie secondary lakini ubunge haumfai.anamwongoza nani sasa kama anaowatukana hawana maana kwake
   
 12. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  yle jamaa alilizwa na kim.........akaahidiwa uwaziri wa elimu akaambulua patupu........

  hili tusi lingesemwa na chadema ingekuwa sooo kinyama
   
 13. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
 14. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
 15. Eshacky

  Eshacky JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 966
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ver Sad! Mateso ndan ya Ardh ye2.
   
 16. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hakika nasema Kagasheki hajui anachozungumza, na kuna habari nyingi sana mbaya wao wanazipolisha na kusukumia upinzani!, Mwisho wa ubaya ni Aibu!
   
 17. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  mkuu ni jehanam kabisa katikati ya utajiri
   
 18. m

  musi Member

  #18
  May 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inasikitisha sana tunanyanyaswa nyumbani kwetu!wale wanaume wa nyamongo wameamua vizuri tu kuwapiga mawe
   
 19. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  mhariri wa Uhuru akichapisha hii anafukuzwa kibarua
   
 20. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Dah Its SAD, i wonder why these people are not the ones beneft the wealth beneath their feet.........Na it is a thing happening sehemu nyingi za utajiri huu........where is the Gorvenment support? kunafaida gani ya kuyachimba? for whose benefit hizo project zina shamiri!!!

  Another Paradox.....
   
Loading...