Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko amjibu Spika Ndugai kuhusu kurudisha Posho

Hahaha Mkuu naomba unijibu maswali yangu


Umesema Alexander the great alikuwa shoga Ndio ali kuvutia huko Kwasababu yeye alikuwa ni akili kubwa ?

Je kwa kiasi Gani imeathirika toka uanze hiyo tabia?
Je hujutiii huo ushetani mkuu? Na vipi jamii inskuchukuliaje?

Ninavyojua kwenye chama chenu kuna wabunge wawili wanatuhuma km ulizozikiri hapa ! Je chama kina ruhusu hili jambo ?
Mh,,ndo maana mi husema,haunaga point,,Basi kwa mawazo yako umeona unatoa point kubwa mno kuongelea upunga.
Badala ujitete,maana umeonaga kwanza you have unstable mind,,yaani unhinged,au kwa kiswahili Nut upstair zimetela,,yaani zimekuwa loose,
Juu kila unachopost humu Ni utopolo,yaani hakina substance,,
Vilevile wewe Ni mtu wa chuki,au kueneza chuki,inaonekana makuzi yako,I mean upbringing yako iko na matatizo,
Ukute pengine ulikuwa abused udogoni kwako,that is why hata terminology ya punga imestick kwako Kama ruba,
So hivyo vyote,vinajionesha kwenye matendo yako humu,wewe Ni umejaa chuki,unaona raha kuona watu wakiumia,na hii inakucompasate kisaikolojia vile wewe uliumizwa utotoni,
 
Mkuu Mimi najua jinsi vijana Wengi walivyoharibika sababu ya upunga tunakutana nao mtaani

So napata picha jinsi ulivyo Ndugu yangu

Huyu alexender the great alaaniwe yeye na kizazi chake kwa kukuingiza kwenye upunga
Pole sana Ndugu yangu
Usiongee vitu usivyovijua,,dhambi ndo Nini?
 
Mbona wanawalazimisha wabunge wenzao wa CHADEMA nao wasusie vikao? SIi kila mbunge alipaswa ajitathmini mwenyewe.

Kama kaingiziwa pesa bila kujua si arudishe, Spika amewataka warudishe hiyo posho . Suala la kuwa karantini Dodoma halina uhusiano na posho. Hizo shughuli za jimbo anazodai kuendelea nazo ni kazi yake na analipwa mshahara.
Hujaelewa soma upya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha Mkuu naomba unijibu maswali yangu


Umesema Alexander the great alikuwa shoga Ndio ali kuvutia huko Kwasababu yeye alikuwa ni akili kubwa ?

Je kwa kiasi Gani imeathirika toka uanze hiyo tabia?
Je hujutiii huo ushetani mkuu? Na vipi jamii inskuchukuliaje?

Ninavyojua kwenye chama chenu kuna wabunge wawili wanatuhuma km ulizozikiri hapa ! Je chama kina ruhusu hili jambo ?
Ha ha ha,kwahiyo Alexandra siyo punga,kawa shoga Tena?
Nasema hivi,,wewe hauna impact yeyote kwenye chama,na hizo kelele zako humu zinatufanya wanaccm kuonekana hopeless,hauna point unabwabwaja mambo yasiyo na kichwa Wala mguu,wewe unadhani unasaidia lakini badala yake wewe unaharibu taswira nzuri na iliyotukuka ya chama chetu,haufai hata chembe
 
Mkuu sikujua tofauti ya punga na shoga ni nini?
Na mtu mwenye akili Alexandria the the great ali ku insipire kuingia kwenye upunga alikuwa mtu gani

Naomba unifafanulie wewe umekaa upande wa shoga au punga
Ha ha ha,kwahiyo Alexandra siyo punga,kawa shoga Tena?
Nasema hivi,,wewe hauna impact yeyote kwenye chama,na hizo kelele zako humu zinatufanya wanaccm kuonekana hopeless,hauna point unabwabwaja mambo yasiyo na kichwa Wala mguu,wewe unadhani unasaidia lakini badala yake wewe unaharibu taswira nzuri na iliyotukuka ya chama chetu,haufai hata chembe
 
ANAANDIKA MHE. ESTHER MATIKO (MB) AKIFAFANUA KWENYE KUNDI LA WHATSAPP LA TARIME ISHI NA MIMI

Bora ucheke Mdogo wangu..!
Hii nchi ni ya ajabu sana...! Juzi niliandika hapa posho zetu kama Michango nikaweka ( Perdiem 120,000/= n sitting 220,000/=) jumla 340,000/=. Maana hatuingii bungeni tupo karantini jamani pamoja Na kujichunguza afya..!

Mhe Spika anasema tumechukua posho...😳!

Posho ya kujikimu wanadai kutuwekea tarehe 1/5/2020 tukiwa karantini? Sijui Nini kipo nyuma ya pazia?

Kwa kawaida posho ya kujikimu huwa tunajaza form ndipo unaingiziwa kwenye account yako..! Na Tumekuwa tunafanya hivyo siku zote. Jana nimeshtuka kusikia eti kuna posho tumeingiziwa Maana sijaenda bank nipo karantini hapa Dodoma sitoki hata nje..! Kwa hiyo sijui kama kweli ama lah.

Kwa hiyo tumeingiziwa posho Za kujikimu bila kusaini? Upendo wa agape huu...! Ambao ghafla tulioingiziwa Fedha Za kujikimu bila kujua tunaitwa wezi? Hapa wanasheria waje watusaidie.

Turudi kwenye uhalisia. Let us assume Yaani tufanye wabunge wa Chadema walijaza form ya posho ya kujikimu( perdiem) Na kusaini labda tarehe 28/4/2020 kwa siku 16. Na hivyo siku 14 kuwa za karantini..! Sasa uhalali wa Mhe Spika kusema turudishe posho ya kujikimu unatoka wapi? Maana sio posho ya kikao kwamba umelipwa bila kuhudhulia?

Hii ni posho ambayo unalipwa kulipia hotel/ chakula n.k. Ukiwa kwenye kituo cha Kazi ambacho ni Dodoma. Sote Twajua matumizi ya perdiem..! Na wabunge wapo Dodoma kwenye karantini Lkn wanafanya majukumu yao mengine ya kibunge kwa njia ya mtandao sio lazima wawepo bungeni.

Kuna wabunge wengi sana wa CCM hujaza form Za hii posho siku ya kwanza Na kuondoka..! Je alishawataka kurudisha hizo Fedha tunawajuwa tena kwa majina. Ni dhahiri hajawahi Na hawezi kwakuwa hizi si posho Za kitako ( sitting allowance) bali ni posho ya ambayo hulipia Malazi Na chakula.

Niseme tu nimesikitika sana kwa hili , inaonekana kuna hidden agenda..! Probably more to come as he said it yesterday...!

Binafsi nafuata masharti ya matabibu ( wataalam wa afya)Najitenga na kujichunguza afya yangu. Marehemu Mhe Ndassa alikuwa Kaka yangu Na rafiki wa kweli kwangu , karibia kila siku nilikuwa naenda kwenye kiti jirani na kuteta naye hata siku Mbili kabla ya umauti wake. Hivyo lazima nijitenge kwa Muda.

Kwangu mimi afya yangu Na ya wale ninao wazunguka ni Muhimu sana kuliko hizo posho.! Kwa Miaka miwili tulikuwa kwa asilimia 80 tupo mhakamani wakati wa Bunge la bajeti sikuona walau hata barua ya Bunge ikiomba mahakama walau wazingatie vikao Vya Bunge Na kufanya kila baada ya siku 14 au mwezi..! Tuliweza poteza posho ya vika Zaidi ya siku 200 kwa wabunge Saba wa Chadema tuliokuwa Na kesi ( Mhe Mbowe, Mnyika, Heche, Mdee, Bulaya, Msigwa Na mimi). Ambapo posho Za vikao tu ni 220,000 * 200 ni 44,000,000/= (44ml).

Nilipelekwa gerezani kwa hilasiku 104 hapa napo nilikosa mamilioni ya shilingi, nilikosa fursa ya kuwawakilisha Wananchi wangu bungeni Na nje ya Bunge. Ijulikane tu nilifutiwa dhamana ambapo nilikuwa nimetumwa Na Bunge Kwenda Burundi , lakini sikuona Bunge wakinitetea ? Leo Nipo karantini kwa tahadhari huku nikiendelea na shughuli zangu Za uwakilishi shida ipo wapi? Maana gerezani ni total lockdown hamna hata mawasiliano.

Jana tu tulifanya kikao cha Kamati ya mfuko wa jimbo, ili kupitia bakaa ya 12.5ml ya tuliyopeleka kwenye Ujenzi wa Choo shule ya sekondari Tagota .

Tulifanya Teleconference na wajumbe na kufikia maamuzi kuwa Tshs. 2.5ml ziende kwenye manunuzi ya samani Za ofisi ya walimu ikiwemo partition ya ofisi. Maana nilipotembelea mwezi wa tatu . Nilikuta Walimu wote wapo kwenye darasa moja lilowazi hata Mwl Mkuu. Na Kilio kikubwa kilikuwa uboreshwaji wa Hiyo ofisi.

Hivyo hizi hisia hasi Na kuonekana tupo mikoani tunadhurula sio sahihi..!

Nasikitika tu kuwa hata tukiwa bungeni kwa ufinyu wa muda hatupati fursa ya kuchangia. Maana ya saa 4 tu Za kuwasilisha hotuba ya wizara, Kamati ya Bunge, hotuba ya upinzani , Michango ya wabunge, majibu ya mawaziri, hitimisho la Mtoa Hoja.......?🤔

Hapa nakuachia wewe mwananchi uone kama wawakilishi wako tunakutendea haki. Unakuta upande wa Chadema wanapata watu wawili tu au mmoja wizara labda wagawane dakika tano .

Nilitarajia Bunge liende hadi July na Vikao vifanyike hadi Jumamosi. Maana tulipunguza masaa ya kikao kutoka saa nane kwa siku hadi saa 4 kwa siku .

Hivyo tungeweka wizara ya siku moja ya zamani kuwa siku 2, Na Za siku 2 kuwa siku 4. Lkn imekuwa kinyume ya wizara zilizokuwa Za siku 2( saa 16 sasa ni saa 4 siku 1, siku 3 saa 24 sasa Ni saa 4 siku 1 na ya siku 1 saa 8 zamani ni saa 4 siku 1 ya sasa. Bajeti Kuu ya serikali ilikuwa siku 6 saa 48 sasa Ni siku 2 Yaani saa 8🤔🤔🤔🤔

Nilidhani mngepiga kelele Bunge lisifupishwe ili wawakilishi wenu wajadili draft Za bajeti Za serikali kwa kina kuliko kinachofanyika sasa..’!

Huwa kila siku nashauri humu Tarime Ishi Na Mimi ..! Tuweke itikadi zetu pembeni, ili tuwe Huru kuchambua mambo kwa jicho la tatu. Bila kufanya hivyo tunaliangamiza taifa.

Wana CCM mnauwanja mpana sana kushauri kwenye vikao vyenu. Maana kwa sasa nyie ndo mmpewa ridhaa na wananchi, ya kukusanya kodi Na kupeleka maendeleo. Nawaomba sana mtambue jukumu lenu . Naona Mmekuwa mkikwepa majukumu yenu kwa kuitafutia Chadema ubaya...!

Tushikamane tuijenge Tarime Yetu.!

Mungu awabariki..!

Corona Ipo, Corona inauwa..! Tuchukue tahadhari.!🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽

Esther Matiko (Mb)
Tarime Mjini.
Sidhani Kama wamura na waghaka tutakupa Jimbo Tena maana kila saa kesi kesi kesi, Mara hiki Mara kile full vituko tuu, five years , nangire muraa , I bhina , ibhina, ibhina, tutakuhe ichikura, aliskika mzee mmoja wa kikurya akilalamika kwa uchungu .
 
Mkuu sikujua tofauti ya punga na shoga ni nini?
Na mtu mwenye akili Alexandria the the great ali ku insipire kuingia kwenye upunga alikuwa mtu gani

Naomba unifafanulie wewe umekaa upande wa shoga au punga
Ha hujua maana?,
Punga Ni mtu anaegawa dozi,so Alexandra alikuwa punga na alikuwa smart pia,
Lakini nishakutoa wasiwasi,sitakunalii,ondoa Shaka,nilikuwa nakutania tu
 
Kwahiyo Mkuu unanivunjia kuwa punga ? Kwasababu Alexander the great alikuwa punga?

Je kuna faida yeyote ya kuwa punga?
Ha hujua maana?,
Punga Ni mtu anaegawa dozi,so Alexandra alikuwa punga na alikuwa smart pia,
Lakini nishakutoa wasiwasi,sitakunalii,ondoa Shaka,nilikuwa nakutania tu
 
Matiko tulimtoa pale UDSM kitengo cha Political Science and Sociology akiwa binti mdogo tena akiwa lecturer msaidizi. Tumemkuza kisiasa na kiimani.
I dout, kasoma MBA pale ud, kamaliza 2005, na nadhani alikuwa mwalimu pale udbs

Stay home, stay safe
Corona kills
 
Mbona humuulizii Baba mwenye nyumbani(Nahodha Hodari?)Yupo kwenye kituo chake cha kazi(Magogoni/Chamwino)?
Sio kosa lako ni ufahamu wako tu ndio mdogo mbunge ofisi yake ni Jimbo lake tu raisi mtawala wa nchi nzima ni ajabu kwa mbunge wa hai kuwa dar ila sio ajabu kwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa chato hata hai anaruhusiwa kukaa
 
Matiko acha kuwaiga kina Mdee na Bulaya watakupoteza

Wewe unaustaarabu jistukie utakufa kisiasa ukiendelea kuwaiga
Polepole nakuona unavyohangaika kumnasa huyu binti kwa dau dogo! Wale 12 wanaohudhuria nasikia umewatwist hadi wakaunda serikali ya kimapinduzi bungeni eti, wamempindua kub! Matiko siyo wa Bei ndogo, panda dau!
 
Hahaha kwani kuna biashara Mkuu
Polepole nakuona unavyohangaika kumnasa huyu binti kwa dau dogo! Wale 12 wanaohudhuria nasikia umewatwist hadi wakaunda serikali ya kimapinduzi bungeni eti, wamempindua kub! Matiko siyo wa Bei ndogo, panda dau!
 
Hahaha kwani kuna biashara Mkuu
Ndiyo! Lile furushi ulilobeba kwenda nalo segerea ukijidai ni nguo za kubadilisha za Msigwa kumbe ni pesa za kumhonga Msigwa tuliliona na ndio maana tulikutimua!
Kwanini unapendaga kubeba mabegi ya pesa kwenye gari yako Kama wanunuzi wa ngo'mbe mnadani za Nini? Una biashara ya bucha?
 
..kwa kweli ccm wamezidiwa kwa hoja.

..sijawahi kuona ccm yenye ombwe la kifikra kama hii ya awamu ya 5.
 
Back
Top Bottom