Mbunge wa Tandahimba kupitia CUF, Katani Katani ajiuzulu na kujiunga CCM

Huyo mzee anatanga tanga tuu. Mh Rais ameshasema, hilo jimbo apewe Msanii wa Bongo flavor, Mr Harmonize. Anyway, baada ya uchaguzi watampa walau uDC.
 
Hapa ndio unakumba rasimu ya warioba kwamba MTU akiwa kiongozi tukiona minendo yako sio mzuri tunakufukuza kabla muda wako kuisha na kumchagua mbona Wangenyooka maana huu ni usaliti
 
Vipi wapiga kura wa upinzani nao wamehama?
Swali zuri sana. Wanapokwama ni kufikiri kuwahamisha wapinzani walioshinda maeneo yao kutawapa hakika ya kushinda uchaguzi ujao. Iwapo ccm inakubalika kwa asilimia 80 waweke tume huru ya uchaguzi na uwanja huru wa mapambano kisha tusubiri matokeo huru.
 
Katani sijui hukumbuki 2010 tulipohama mji ili kushikiza use mbunge, hukumbuki ffu walivyotupiga hukumbuki tulivyokufa sa.WA

Hukumbuki tulivyoamua kuchukua jukumu 2015 ili uwe mbunge
Hakika tunaumia na tunalia

Ulikubali kuipigania korosho nasi mpaka tukapata bei nzur hata kabla ya magufuli kuliko eneo lolote tz lkn haututazami sisi
Tunajua ukishakuwa mbunge hufanani tena na sisi basi ungetudanganyadanganya mpaka mwisho.

Siamin unastahili haya

Sijui kama tandahimba utakaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boniphace Kichonge,
Wenye dhiki ya maisha ni wananchi wa hali ya chini ambao hawajui kama nchi hii ilipata uhuru au bado ipo chini ya mabeberu, hivyo hao wabunge wanaohama hama kila kukicha wapo kwa maslahi yao binafsi na familia zao tu.
 
Back
Top Bottom