Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM) avuliwa ubunge na mahakama!

DOMA

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
944
365
Wakuu leo ndiyo kunatolew hukumu ya kupinga matokeo ya ubunge wa sumbawanga mjini wa Aeshy Hilaly Halphany CCM dhidi ya mwalimu Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema ambaye anadai kuchakachuliwa katika uchaguzi huo.

Madai miongoni ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa kanisa katoliki, nk kwa sharti la kumpigia kura mbaya zaidi ni kwa mkurugenzi mwanamama kutoa ushahidi wa kupinga ushindi wa mbunge huyo, mkurugenzi huyo alihamishwa muda mfupi mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutolewa na kupelekwa wilaya ya Ileje.

Moja ya kituko katika kesi hii mara baada ya mbunge huyo kuulizwa kama anaamini na kusema hajui kama alishinda ila mkurugenzi ndiye anayejua ushindi huo, kimsingi ulinzi umeimalishwa kwani yaweza kuwa mbaya endapo Aeshy atatangazwa mshindi, askali wapo wa kutosha, washawasha na mabomu, lakini kesi hii ilikosa umaarufu kwa kuwa waandishi njaa wote walikuwa upande wa Aeshy mpaka ripota wa ITV Joshua joel update tutawaletea mara kesi itakapoanza....

Kamanda Doma.

UPDATES:
Umati umejitokeza kwa wingi sana na watu wamejaa ndani hivyo imebidi spika zifungwe nje lakini gari la polisi limekuwa likizunguka kuonya juu ya uvunjifu wowote wa amani.

Muda mfupi ujao jaji ataingia ila naona makamanda wengi sana kutoka sehemu mbalimbali wakiwa ndani ya magwanda

Jaji ameingia na kuanza kusoma kesi kwa lugha ya kiingereza na kesi nzima ina takribani kurasa 68

Mawakili wanaendelea kutoa utetezi wao wa mwisho lakini umati uliopo unatisha na Licha yakuonekana wafuasi wengi ni wa Chadema lakini Askari wameondolewa na kuashiria uwezekano wa chadema kushinda kesi.


Yuko kwenye hoja namba 15 na ameiunganisha hoja namba 14 anadaiwa kutoa hongo! Wakuu tuombe Mungu mambo yanawezakuwa mazuri jaji anakubaliana hoja ya walalamikaji, Mungu saidia Democrasia.

Naendelea kuwajuza!
Hoja za mwisho zinaweza kuwabana Magamba lakini naona Polisi wameanza kumwagika
UPDATES
mashabikina wafuasi wa Chadema wanashangilia nje ya mahakama kwa mbwembwe japo jaji bado hajatoa tamko
UPDATES
HATIMAYE CHADEMA WAIBUKA NA USHINDI NA UCHAGUZI KUTANGAZWA KURUDIWA UPYA BAADA YA BWANA AESHY KUKUTA NA KOSA LA KUTOA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI HUO. Chademaaaaaaaaaaaaaaaaa vemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
UPDATES
Bwana Aeshy ametangaza kukata rufaa ya kupinga kutenguliwa kwa ushindi wake
 
Huyo jamaa si ndo huwa anamalori na sheli za mafuta hapo Sumbawanga, nimshabiki mkubwa wa Arsenal na anapenda sana maua.
Alimwaga hela sana ili ashinde na ilibidi aingie mfukoni zaidi kwa kutoa M50 baada yakugundulika kashidwa akahonga ili atanganzwe mshindi! Mungu hapendi dhuruma hata mkimtunuku huo ushindi Mungu atachukia then atawaadhibu
 
Kamanda Doma omba MoDs wakudilishe heading kipengele cha tetesi maana mpaka hapo hujabashiri kama mbunge huyo anaweza kuvuliwa au laah.

Umeeleza kilochotokea.

Usikose kituhabarisha yatakayojiro huko kwa kila hatua. Waandishi wa habari wanaweza kuwa njaa lakini SI MWANAJF, hiyo ndiyo imani yangu.
 
Tunashukuru mdau. Endelea kutujuza. Hapo ndio tutajua km mahakama kuna haki ama haki zipo kwenye mifuko ya suruali ya mafisadi.
 
Dah,sijawah kuickia hyo kesi hata siku m0ja,nachokumbuka ni kwamba wakat wa kampeni za mwk 2010,kuna mg0mbea alitoa msaada KANISANI,lakin hata kama Joshua Joel alihongwa asiripot bado sion tatizo,yeye amehongwa je itv ndo chanzo pekee cha habari?
 
hapa sumbawanga nimewahi sema hakuna waandishi wa habari kabisa na kama wapo wawakilishi wa vyombo vya habari basimhawajui habari gani walipoti na wengine ni marafiki na wanachama wa ccm kwa hiyo hawwezi kulipoti vema na inawezekana wamehongwa. Mkubwa kwa kesi hiyo usisite kutujuza kitakachoendelea maana wengine tuko mbali kidogo.
 
kimsingi ulinzi umeimalishwa kwani yaweza kuwa mbaya endapo Aeshy atatangazwa mshindi, askali wapo wa kutosha, washawasha na mabomu, lakini kesi hii ilikosa umaarufu kwa kuwa waandishi njaa wote walikuwa upande wa Aeshy mpaka ripoter wa ITV Joshua joel update tutawaletea mara kesi itakapoanza....
Kamanda Doma
Mkuu asante kwa kutujuza. Bila shaka suala la ulinzi kuimarishwa kwa sasa linaleta mashaka endapo mahakama zetu zinatenda haki. Huwezi kushangaa kuwa endapo ulinzi unawekwa mahakamani na hakimu hatendi haki wananchi wanaweza kufuata huko nyumbani kwake kumwuuliza haki. Mambo haya hayaitaji ulinzi bali ni kutenda haki ili tuishi kwa raha bila kufuatwa na mizimu kwa wale tunaowatendea mabaya
 
MUNGU IBARIKI CHADEMA HAKI ITENDEKE SWALI: kama MAHAKAMANI ndo kunatolewa HAKI huo ulinzi wa polisi wa nini? Tena jamani?? 2pe ripoti KAMANDA
 
Doma ni kijiji cha mwisho kabla ujaingia mikumi ukitokea moro maarufu kwa kilimo cha nyanya na malijuana. DOMA na wewe usinunuliwe wala usiogope ndumba nasikia kuna mtu alitundika koti hewani uko
 
Raia wamejitokeza kwa wingi sana, askari kibao ukumbi umejaa sana, hukumu bado haijaanza kusomwa wanasubiri wafunge spika kwa nje.

UPDATES:
Jaji bado hajaingia, raia waliojipambanua ni CDM na ndo wengi zaidi ya 95% na wamekula kombati, wapo makamanda toka mkoa mpya Katavi toka Mpanda mjini na Tunduma
 
Back
Top Bottom