Elections 2010 Mbunge wa Sumbawanga mjini akiwa chini ya ulinzi baada ya kuvamia ofisi za CHADEMA Igunga

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Feb 9, 2010
899
1,084
Aesh akiwa chini ya Ulinzi.jpg Aesh akiwa chini ya Ulinzi.jpg muulizeni kafuata nini chadema? wakati juzi alitaka kuua watu wetu na kuchoma magari ya chama?
 
Mbona huyo jamaa mwenye shati lenye strips anaonekana kama anataka kumpa ngumi....

Duh!! Mpaka J2 tutaona mengi...
 
tutamuuliza Masaburi anatumia nini kufikili, maana inavoonesha katika kategori za kufikili km zilivoanishwa na Masaburi hii yake haipo, tutamtafuta Masaburi atufafanulie
 
Huyu si tumesikia michezo yake ni ya kutumia bunduki na mambo ya magendo, hapa kafuata nini tena jamani kama sio uchokozi?
 
Nazidi kuamini siasa ni usanii mtupu. huwa nazidi kuamini ni usanii hasa baada ya kuwaona hivi wakikunjiana ngumi halafu jioni wamekaa pamoja na kupata bia baridi huku wananchi wakiendeleza chuki!
 
Mleta thready hii naomba unijulishe hii movie iliisha vipi? Steling aliuwawa au?
 
Laiti wangejua ni mtego wangeachana nae aondoke kwa amani tu.
Utasikia baadae "katekwa na chadema"
au polisi wanafika kumuokoa kumbe ni deal wamepanga
 
Jamani hii hatari sasa ina maana watu wanataka kutoana macho kwa sababu ya uchaguzi mmbunge wa sumbawanga anafanya nini Igunga. Its one thing to campaign for votes but its another thing to attack each others because of winning votes. Inashangaza sana kuona the amount of political big-wigs waliojaa huko in the name of election. Something is not right in our politics.
 
Jamani kuna watu huwa hawafahamiki kabisa hivyo anaanzisha jambo lolote ili kupata attention ya media na watu watamfahamu. Nyie mnafikiri huyu Zuzu nani anamfahamu?
 
Jamani kuna watu huwa hawafahamiki kabisa hivyo anaanzisha jambo lolote ili kupata attention ya media na watu watamfahamu. Nyie mnafikiri huyu Zuzu nani anamfahamu?

Kumbe mbunge wa sumbawanga mjini ni dume?
me nlisikia jina "Aeshi ,sijui aisha" nkahisi mdada.
 
Hiyo Kijani ilivyokunjwa, ningekuwa mm hiyo ngumi ningeipeleka kwenye pua. paaaaah
 
Tukio lenyewe liko hivi - Ni kwamba Bashe aliomba kuja kuongea na Viongozi wa CDM kuhusu hali ya hatari iliyopo hapa Igunga. Akaja na Beno Malisa. Wakati mazungumzo yanaendelea ndipo ghafla akaingia mbunge Aeishi bila kualikwa. Vijana walipomwona adui namba moja aliyewarushia risasi majuzi tu wakaamua kumweka chini ya ulinzi. Kama sio Dr Slaa kuwa karibu sijui wangemwokotea wapi leo.
 
Back
Top Bottom