pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,344
Siku ya 40 ya mwizi hatimaye ilitimia kwa Mbunge wa Sirisia John Waluke na mshukiwa mwenza Grace Wakhungu, kwenye kesi ya ufisadi dhidi yao ndani ya mahakama ya ufisadi(Anti-Corruption Court) jijini Nairobi hivi majuzi.
Hii ni baada ya Chief Magistrate Elizabeth Juma kuwapata na hatia, wao na kampuni yao ya Erad Supplies and Contracts Limited, kwenye wizi wa KES 247Million za NCPB(National Cereals and Produce Board). Ambapo wawili hao na Erad Ltd walipokea hela kwenye kandarasi hewa ya kuwauzia NCPB mahindi miaka miwili iliyopita.
Mbunge John Waluke na Grace Wakhungu ambao walikuwa 'directors' wa Erad Supplies watahudumia vifungo vya miaka 67 na 69 mtawalia au walipe faini ya jumla ya KES 2.1Billion. Kongole kwa hakimu Elizabeth Juma na idara ya mahakama pia, kwa kazi nzuri hii kwenye vita vikali hivi dhidi ya ufisadi. Kazi iendelee.