Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,580
- 6,119
Halafu huyu anaitwa eti na yeye Mpiganaji. Ndiyo hawa wanauguwa na wanaishia kutelekezwa na CCM kwenye vitanda vyao na kuanza kulia wapelekwe India kwa Matibabu.Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba, alidai kuwa wakati wa kampeni, Marando alikuwa akitumia lugha kali na za kashfa hivyo iwapo atachaguliwa kuwa spika atakuwa na lugha hizo hizo au atajirekebisha.
Swali hilo lilionekana kumkera Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ambaye alitaka kupata mwongozo wa mwenyekiti wa kikao hicho, lakini kwa mara ya pili aligonga mwamba kwa kuelezwa na mwenyekiti kuwa hicho si kikao cha Bunge.
Marando katika majibu yake alimweleza mbunge huyo kuwa uchaguzi unaendeshwa kwa kanuni na maadili na mtu anayeyakiuka anachukuliwa hatua.
"Mimi sijawahi kulalamikiwa na mtu yeyote kuwa nimekiuka maadili ya uchaguzi hivyo hayo madai ya mbunge kuwa niliwahi kutumia lugha kali si sahihi hata kidogo," alisema Marando kwa kujiamini na kushangiliwa.
Nkumba, unatuangusha bana. Si lazima useme na wakati mwingine ni heri ukae kimya. I believe you can do better than those Mipasho. Wewe Mtu wa Sikonge na Taarabu wapi na wapi?