Mbunge wa Rorya abadili rangi ya gari la kubebea wagonjwa kwa kile alichoita maslahi mapana ya wananchi wake

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,938
25,281
"Nimewasikia wananchi wangu na tumefanya mabadiliko ya rangi ya gari hili (Ambulance) kwa maslahi mapana ya Wana Rorya wote bila ya kujali vyama vyao.

Poleni sana kwa wale waliovurugwa na rangi ya awali, nia yetu ni njema kwa watu wote wa Rorya" Mhe. Jafari Chege Mbunge, Rorya.

20210201_195151.jpg
20210201_195156.jpg
 
Amefanya kitu kizuri, utu. Kuwasaidia ndugu, raia wako wote bila kujali itikadi, vyama vyao, uwezo wao. Haijawi kuwa kitu kibaya.

Kama ana nia ni ya dhati kuwasaidia wote, mpe nafasi.
Kama kweli atakuwa na akili zinazofanya kazi,ila mwenye taarifa za kuthibitisha hili atuwekee humu.
 
Tanzania yetu haiishi vituko,ukienda pale traffic dept. Kuna sheria ipo inayozungumzia ni rangi gani magari ya kubeba abiria yanatakiwa yawe na rangi gani pamoja na rangi ya vingora vyao,bluu na lights za bluu(polisi) etc etc sasa kwenye ile wilaya mkuu wa traffic hii so called ambulance ilitakiwa iandikiwe traffic fine na kubadilisha alama zake pamoja na rangi inayotakiwa kisheria.hapa ndio matunda ya 5 mingine.
 
"Nimewasikia wananchi wangu na tumefanya mabadiliko ya rangi ya gari hili (Ambulance) kwa maslahi mapana ya Wana Rorya wote bila ya kujali vyama vyao.

Poleni sana kwa wale waliovurugwa na rangi ya awali, nia yetu ni njema kwa watu wote wa Rorya" Mhe. Jafari Chege Mbunge, Rorya.
View attachment 1691850View attachment 1691851

Nimecheka kwa nguvu, kabadali rangi ya gari ila kabakiza picha yake. Au yeye ni baadhi ya dawa za hospitali?
 
"Nimewasikia wananchi wangu na tumefanya mabadiliko ya rangi ya gari hili (Ambulance) kwa maslahi mapana ya Wana Rorya wote bila ya kujali vyama vyao.

Poleni sana kwa wale waliovurugwa na rangi ya awali, nia yetu ni njema kwa watu wote wa Rorya" Mhe. Jafari Chege Mbunge, Rorya.
View attachment 1691850View attachment 1691851
Pamoja na hayo mbona kama hii ya pili ni kama photo shop?
 
Tanzania yetu haiishi vituko,ukienda pale traffic dept. Kuna sheria ipo inayozungumzia ni rangi gani magari ya kubeba abiria yanatakiwa yawe na rangi gani pamoja na rangi ya vingora vyao,bluu na lights za bluu(polisi) etc etc sasa kwenye ile wilaya mkuu wa traffic hii so called ambulance ilitakiwa iandikiwe traffic fine na kubadilisha alama zake pamoja na rangi inayotakiwa kisheria.hapa ndio matunda ya 5 mingine.

Ni ukweli kutoka Dar hadi Mbinga tulisimamishwa mara sita. Tukapigwa faini ya laki 90000.

Ni kwamba wanaongea. At times, many times, hawako fair.

Isimamishe hiyo gari, anapigiwa simu traffic wa kituo kinachofuata.
 
Kati ya wabunge wanaoonekana watafeli mapema Ni huyu. Eti anakuja ambulance anaweka chats ya CCM . Najua ubunge wamepata kupitia ubabe wa tume Sasa isijekuwa kila kitu CCM
 
Back
Top Bottom