Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini kuondoka CHADEMA na kujiunga NCCR Mageuzi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,376
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasin ametangaza kuachana Chama Cha CHADEMA na kujiunga na NCCR - Mageuzi baada ya kumaliza kipindi chake cha Ubunge

Awali, kulikuwa na taarifa zinazoeleza kuwa Mbunge huyo ameonesha kusikitishwa baada ya kuondolewa bila kupewa taarifa kwenye 'Group la WhatsApp' la Wabunge wa CHADEMA

Imeeleza kuwa katika ‘group’ hilo yumo pia Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe
 
Mbunge wa Rombo Joseph Selasini ametangaza kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kurejea chama cha NCCR Mageuzi baada ya kumalizika kwa vikao vya bunge.

My take:Taratibu tutazungumza lugha moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kete yao inaweza kuja kuwagarimu ikifeli..Kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu.Itakuaje hiyo nafasi wasipopewaaa?Me naamini vyama vyenye mwelekeo kwa sasa ni vi3 tu.Huwezi kumwambia hata mtoto wako wa miaka 10 unatoka kwenye vyama hivi eti unaenda NCCR akakuelewa...!!!!
 
Chadema watabaki wasiojielewa

Wengi wenye vyeo Chadema walitokea Nccr mageuzi, hii inamaanisha kuwa Nccr mageuzi Ndio chama bora cha upinzani
 
Na Corona yote hii bado unajihakikishia kuwa eti nikimaliza ubunge nahamia NCCR? Wakili mwenzake na rafiki yake mkubwa mzee Mmanda alikuwa kwenye tv Alhamisi ila tunavyoongea hapa ameshazikwa huko Mtwara asubuhi hii na watu nane. Akae kimya kwanza maana kila mtu uelekeo wake ni kwenye Corona.
 
Mbatia anampango ngani na upinzani tanzania yani watu wako busy wanatafuta upinzani thabiti tz.yeye anauporomosha mungu akusamehe mzee wa majanga
 
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasin ametangaza kuachana Chama Cha CHADEMA na kujiunga na NCCR - Mageuzi baada ya kumaliza kipindi chake cha Ubunge

Awali, kulikuwa na taarifa zinazoeleza kuwa Mbunge huyo ameonesha kusikitishwa baada ya kuondolewa bila kupewa taarifa kwenye 'Group la WhatsApp' la Wabunge wa CHADEMA

Imeeleza kuwa katika ‘group’ hilo yumo pia Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe
Kituo cha mapumziko akisubiri kuunganisha ndege kwenda nchi ya kijani.
 
Back
Top Bottom