MBUNGE wa Rombo Joseph Selasini (CHADEMA) awatupia lawama madiwani

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
MBUNGE wa Rombo Joseph Selasini (CHADEMA), amewatupia lawama baadhi ya madiwani kwa kukagua na kupitisha miradi ya maendeleo ambayo haijakidhi vigezo. Alisema hatua hiyo, inasababishia hasara kubwa Serikali, ambayo imekuwa ikihaha kuboresha maisha ya Watanzania.

Akizungumza wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Kilimanjaro jana, Selasini alisema pamoja na madiwani kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, lakini bado imekuwa haikidhi vigezo.

Alisema kumekuwa na matumizi makubwa ya fedha za wananchi kutekeleza miradi ambayo haiwanufaishi kutokana na mingi kuharibika mapema, kutokana na uzembe wa watu wachache.

“Fedha nyingi za wavuja jasho, zimekuwa zikitumika kifisadi na kutekeleza miradi isiyo kidhi vigezo na cha kusikitisha zaidi madiwani wamekuwa wakikagua miradi hii na kufumbia macho,” alisema Selasini.

Alisema miradi hiyo, iliyojengwa chini ya kiwango ni Shule ya Sekondari ya Mamsera ambayo sakafu yake, ilijengwa kwa kipindi cha miaka mitatu, lakini imebomoka yote.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi alisema ili kuepuka mgongano wa kupokea miradi iliyo chini ya kiwango, inapaswa miradi yote isipokelewe mpaka ikaguliwe na wakaguzi wa nje.

“Kwa miradi ya ujenzi, wakurugenzi watumie wakaguzi wa nje ili kuepusha migongano ya mara kwa mara na kuisababishia hasara Serikali, jambo hili linasababisha wananchi kukosa imani na Serikali yao,” alisema.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akifungua kikao hicho, aliagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Kilimanjaro, kutoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara kwa wananchi.

Alisema kama elimu, itatolewa ipasavyo itasaidia kuondoa uvamizi katika hifadhi za barabara unaofanywa na wananchi ili kuondoa migogoro.
 
Back
Top Bottom