STRUGGLE MAN
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 8,638
- 16,566
Mbunge wa Pakistan mwenye asili ya Tanzania alaani ubaguzi wa rangi Marekani
Mbunge mmoja wa Pakistan mwenye asili ya Afrika amekosoa vikali vitendo vya utumiaji mabavu na ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa Marekani wenye asili ya Afrika.
Mbunge huyo wa jimbo la Kusini mwa Pakistan mwenye asili ya Tanzania amelaani vikali wimbi la ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi ya Marekani dhidi raia weusi wa nchi hiyo.
Tanzilah Qanbarani mwenye umri wa miaka 41 ni mwanamke wa kwanza kutoka jamii za walio wachache kujitosa katika siasa na kugombea ubunge nchini Pakistan. Anasema lengo lake kuu la kuingia kwenye siasa ni kupigania maslahi ya jamii za walio wachache.
Mbunge huyo wa Uttar Pradesh nchini Pakistan amesema, "jamii zetu zinapaswa kuwa huru na kuwa mbali na vitendo vya kibaguzi haswa ubaguzi dhidi ya watu weusi."
Maandamano ya kulaani ubaguzi dhidi ya watu weusi yameshuhudiwa ndani na nje ya Marekani
Ameashiria kuhusu matatizo yanayowakali watu weusi wa jamii ya Sheedi katika nchi hiyo ya Asia ambapo amesema watu wa jamii hiyo wanabaguliwa hata katika sekta ya elimu. Aghalabu ya watu 250,000 wa kabila la Sheedi wanaishi kusini mwa mkoa wa Sindh, na katika maeneo ya kusini mwa Punjab.
Kadhalika amelaani mauaji ya kikatili ya George Floyd aliyekuwa na umri miaka 46, ambaye aliaga dunia baada ya kukabwa shingoni kwa goti na polisi mzungu kwa jina la Derek Chauvin kwa muda wa dakika tisa huko Minneapolis jimboni Minnesota Mei 25 mwaka huu. Kifo cha kikatili cha raia huyo Mmarekani mweusi mwenye asili ya Afrika kimeibua maandamano makubwa nchini Marekani na katika nchi nyingine huku watu wakiendelea kupinga vitendo vya mabavu vya polisi na ubaguzi wa rangi nchini Marekani.