Mbunge wa Nkenge, Asumpta Mshama lazima ung'oke 2015!

Daaah,yani nilikuwa najiuliza hivi ni kwanini mapadri wanamwagiwa tindikali na wengine wanapigwa risasi sikuwa na napata majibu! lakini kwa huyo padri anachokifanya ni dhahiri kuwa anatumiwa kisiasa,yani padri mzima badala ya kumtumikia Mungu anakubali kutumia madhabahu ya Mungu kuchafua watu kwa maneno ya uongo,sijui amelipwa sh. ngapi?Eti asipigiwe kura!!!!!!!!Wampigie nani sasa???? Ana mpango wa kuacha altare na kugombea ubunge? Kweli mwisho umefika......unafiki,chuki kila kona hata kwa mapadri
mwambie alipe deni na padri atakosa la kusema
 
Hapa tunacho kizungumzia ni huyu asumta,habari ya padri hiyo ni mengine,na kama huyo mbunge ni jf member ni afadhali aisome hii habari,ingawa anajua.
 
Wewe kama unajiona unampenda basi atapata kura yako na ya familia yake kutoka kwao kijunja,lakini sehemu zote kiziba tumekachoka haka kamama.
 
tatizo ni bei ya mkaa broo.hilo jina mshana kwanza lakipare imekuwaje huko uhayani?pili kagera haiwezi kuendelea hata kidogo kwa sasa,kwanza wasomi wengi wakihaya wanawekeza dsm kuliko uhayani,wanamashule kibaoya binafsi dsm but kwao hakuna kitu,pili wahaya ni wapenda sifa sana so wawekeze uhayani wamwoneshe nani ili wajisifie?wao wanataka sifa,.but nahisi wanampango wa kuufuta mkoa wao wahamie dsm coz kila anayejanjaruka akitoka kagera hageuki nyuma.
 
Akiwa ni miongoni mwa wabunge wa CCM waliopita bila kupingwa, mbunge huyu amekua kama mtalii katika bunge letu mjini Dodoma.
Aliyekua mgombea wa ubunge kupitia CDM maarufu kwa jina la " Focus" alijitoa dakika za mwisho na kumfanya mama huyu kupita bila kupingwa. Lakini cha ajabu huyu mama hajawai kuisimamia serikali kutokana na ahadi alizozitoa mh Rais ikiwamo kuunganishwa kwa jimbo la Ngenge katika gridi ya taifa.
Sasa basi sisi kama vijana tunakuahidi mh Mbunge kwamba hautorudi mjengoni tena baada ya 2015!
TUMECHOKA

Picha tafazali
 
Huyu Mhe. Asumpta hafai hata kidogo kuwakilisha mkoa wa wapambanaji kama Kagera. Nikikumbuka matusi, vijembe, hoja za uongo na dharau wakati wa bunge maalumu la katiba. Hatuwezi kuwa na mbunge wa mipasho wa namna hii katika maswala muhimu kama kutunga katiba mpya.
 
inasemekana huyo phocas hakuongwa, ila alinyamazishwa kutokana na huyu jamaa kwa muda mrefu amefanya mikataba mingi na serikali kwa upande wa shughuli yake ya mziki. kwa wale wa kagera sina shaka kama kuna mtu ambaye hamfahamu huyu Phocas amekuwa mpiga mziki maarufu Mkoa wa Kagera. Na amepiga mziki katika matamasha mbalimbali ya serikali na ccm pia kama hafla za Mwenge, mikutano ya CCM. na inasemekana CCM walipoona kagombea kupitia upinzani ( CDM ), kama kawaida yao kwa kuwaogopesha wafanya biashara wakisema amefanya shughuli zake za kimziki kwa kiibia serikali kwa kutokulipa mapato
 
Wewe kama unajiona unampenda
basi atapata kura yako na ya familia yake kutoka kwao kijunja,lakini
sehemu zote kiziba tumekachoka haka kamama.

kwao sio Kijunja ni Nkaka pia huyu mama kaolewa na mwanaume wa kigogo wanaishi Dodoma kitendo cha kuja kugombea Nkenge ni mambo ya ajabu ifike mahali wana Kiziba tujitambue
Alijidai kujenga shule akaishia vyumba viwili mpk leo
 
Ng'oa hiyo kamanda.Ni miongoni mwa wabunge wa CCM wenye hoja dhaifu. Yeye anachojua ni kuitetea ccm hatakama imefanya blander ya wazi.
 
Mtoa madam ndio mgombea 2015. Jipange CCM ni watembeza hela km jimbo wanalitaka. Bado huonekani kuwa strong link.
 
Huyu mama alichaguliwa kwa vigezo gani ? Mbona ni kama akili anaziacha nyumbani waqt anakwenda bungeni. anatoa matatizo halafu mwisho anaunga mkono hoja kwa 100%
 
ukikumbuka wabunge wa zamani kutoka huko akina Kinyondo ukalinganisha na huyu basi unaweza kutoa machozi, lakini ndio hali halisi utafanyaje!!
 
Huyu ni kilaza kabisa jimbo lake halina maji lkn juz sijaona hata anauliza swali kwa Magembe badala yake mwishon analalamika eti aliomba kuchangia lkn hakupewa nafasi ndo mwenyekiti zungu akamuumbua kuwa anatabia ya kuchelewa kuingia bungeni wakat wenzake wanawahi, sijui anafanya biashara dodoma! 2015 apigwe chin huyu km rais wa malawi
 
Back
Top Bottom