Mbunge wa Nkasi, Ally Keissy awachongea watumishi kwa Rais Magufuli

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amesema makandarasi wanashirikiana na baadhi ya watendahi watumishi wilaya ya Nkasi kutafuna fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema jambo hilo linasababisha miradi mingi kufa, mingine kutofanya kazi.
Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 8, 2019 katika ziara ya Rais wa Tanzania, John Magufuli wilayani humo Mkoa wa Rukwa.

Katika ziara yake leo Magufuli amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo barabara ya Sumbawanga – Kanazi na kituo cha afya cha Namanyere.

Mbunge huyo amesema watumishi wa umma wanashirikiana na makandarasi kuiba fedha za umma na kutotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa huduma ya maji licha ya kulipwa fedha zao.

“Mheshimiwa Rais, Serikali yako inaleta fedha lakini makandarasi kwa kushirikiana na watumishi wako wanashirikiana kutuibia. Mkandarasi peke yake hawezi kuiba hela ni watumishi wako ndiyo wanawasaidia,” amesema Keissy.

Ameanza kubainisha mradi wa ujenzi wa bwawa la Mfili ambalo ni uhai wa mji wa Namanyere. Amesema mradi huo ulikuwa wa Sh730 milioni lakini ukienda kuangalia mradi huo haufiki hata thamani ya Sh300 milioni.

Keissy amesema serikali kuu ilizuia mkandarasi kulipwa Sh300 milioni zilizokuwa zimebaki lakini anashangaa kusikia mkandarasi huyo alilipwa fedha hizo kwa siri licha ya zuio la serikali.

Mbunge huyo amezungumzia mradi mwingine wa ujenzi wa chumba cha baridi kwa ajili ya kuhifadhia samaki huko Kirando.

Amesema mradi huo wa Sh356 milioni umekamilika lakini hauna uwezo wa kuhifadhi samaki na mkandarasi ametokomea na fedha zote.

“Mradi huu ni wa Sh356 milioni lakini cha ajabu alilipwa fedha zote katika awamu tatu akamaliza hela za mradi lakini mradi hauna kitu na mashine zilizonunuliwa ni za kuhifadhi nyanya na kabichi, siyo samaki,” amesema mbunge huyo.

Keissy ameendelea kubainisha miradi mingine kwa kuangazia mradi wa umwagiliaji kwa wakulima wa mpunga huko Kirando wenye thamani ya Sh1.8 bilioni lakini amesema mpaka sasa hauwasaidii wakulima, ni mradi hewa na makandarasi wamekimbia.

Kuhusu mradi wa maji wa Namanyere, amesema mkandarasi alitaka kulipwa Sh1.5 bilioni lakini baada ya Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kufanya uhakiki akabaini kwamba Sh300 milioni zimezidi, hivyo akamtaka kumalizia kazi yake bila kulipwa hizo Sh300 milioni, naye akakubali kufanya hivyo.

“Rais ninakuomba hizo Sh300 milioni zilizookolewa zikatumike kusambaza maji katika maeneo mengine ya wilaya ya Nkasi kwa sababu changamoto kubwa katika wilaya hii ni maji, tunapata maji kwa asilimia 16 tu,” amesema.

keissy%2Bpic.jpeg
 
Kama haya yanayosemwa ni kweli basi chi hai inatafunwa kiasi kwamba JPM hana buda kufukuza kazi watumishi sehemu nyingi anazofanya ziara!!! Hawa watu wanakula kiapo wanapoteuliwa lakini hata hivyo bado wanaliibia Taifa!!!
 
Atakamatwa mkandarasi na kushitakiwa ila watumishi wa serikali wataachwa. Kasema Warioba. It takes two to tango.
 
Back
Top Bottom