Mbunge wa Ngorongoro(CCM), Ashindwa Kazi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Vyombo vya usalama mkoani Arusha, vinazishikilia bunduki 103 zikiwamo za kijeshi wilayani Ngorongoro sambamba na magunia 270 ya bangi wilayani Arumeru.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda alitoa taarifa hiyo juzi katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na kusema; “Arusha sasa ni shwari.”

Alisema ndani ya wiki mbili tu, silaha hizo 103 zimesalimishwa wilayani Ngorongoro na zipo mikononi mwa polisi kutokana na agizo la Serikali kuwataka wananchi wazisalimishe.

Alisema katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana, jumla ya magunia 270 ya bangi yalikamatwa wilayani Arumeru na ekari 25 za mashamba yake ziliteketezwa.

Ntibenda alisema magunia hayo ya bangi na mashamba yake yamebainika katika operesheni dhidi ya kilimo cha bangi iliyofanyika katika vijiji vya Kisimiri Juu, Ibimbwa, Ngarenanyuki na Oldonyosambu.

“Katika kipindi hicho pia, katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha, jumla ya kilo tatu za dawa za kulevya; cocaine na heroini na kilo 1,800 za mirungi zimekamatwa,” alisema.

Ntibenda alisema watu 180 walikamatwa kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na 160 kati yao wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.

“Kwa ujumla mkoa wa Arusha sasa ni salama. Napenda kuvipongeza vyombo vya usalama kwa kazi nzuri wanayofanya,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema baadhi ya wananchi waliosalimisha silaha hizo walikutwa na bunduki za kivita aina ya K47 na SMG zisizoruhusiwa kumilikiwa na raia.

Alisema wapo baadhi ambao silaha zao zilikuwa zikimilikiwa kihalali lakini walishindwa kutoa maelezo yanayoridhisha ya mahali walikopata risasi za ziada baada ya 30 za awali kwisha ambazo hutolewa kisheria.

Alisema wanaendelea kuzishikilia silaha hizo na baada ya uchunguzi wanaweza kuwarudishia wanaozimiliki kihalali.
 
Kijiji cha kisimiri ni maarufu kwa ulimaji wa bangi ...hata kijiji cha Ngarenanyuki.

Pia kijiji cha oldonyosambu ni walimaji wakongwe wa bangi pamoja na uuzaji wa pombe haramu ya gongo....Kote huku kuna wabunge kupitia Chadema...!

Kama ni kushindwa kazi basi Nassari na mwenzake meseyeki waachie ngazi mapema
 
Hiyo taarifa ingetolewa na RPC ingependeza zaidi. Au Mkuu wa Mkoa wa Arusha ana hofu ya kusoma risala kama ya "Dokta" Rutengwe!?
 
Sasa uhusiano wa hii habari na Mbunge kushindwa kazi yake ya Ubunge ukoje mkuu??
 
Hongera mkuu wa mkoa kwa kazi nzuri, nawaomba ukawa tuweke Silaha chini tuipongeze kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa arusha kwa kazi nzuri
 
Kijiji cha kisimiri ni maarufu kwa ulimaji wa bangi ...hata kijiji cha Ngarenanyuki.

Pia kijiji cha oldonyosambu ni walimaji wakongwe wa bangi pamoja na uuzaji wa pombe haramu ya gongo....Kote huku kuna wabunge kupitia Chadema...!

Kama ni kushindwa kazi basi Nassari na mwenzake meseyeki waachie ngazi mapema
bangi ya kisimiri inavutwa dunia nzima na wanajua awawezi kwenda kuichoma
 
Vyombo vya usalama mkoani Arusha, vinazishikilia bunduki 103 zikiwamo za kijeshi wilayani Ngorongoro sambamba na magunia 270 ya bangi wilayani Arumeru.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda alitoa taarifa hiyo juzi katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na kusema; “Arusha sasa ni shwari.”

Alisema ndani ya wiki mbili tu, silaha hizo 103 zimesalimishwa wilayani Ngorongoro na zipo mikononi mwa polisi kutokana na agizo la Serikali kuwataka wananchi wazisalimishe.

Alisema katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana, jumla ya magunia 270 ya bangi yalikamatwa wilayani Arumeru na ekari 25 za mashamba yake ziliteketezwa.

Ntibenda alisema magunia hayo ya bangi na mashamba yake yamebainika katika operesheni dhidi ya kilimo cha bangi iliyofanyika katika vijiji vya Kisimiri Juu, Ibimbwa, Ngarenanyuki na Oldonyosambu.

“Katika kipindi hicho pia, katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha, jumla ya kilo tatu za dawa za kulevya; cocaine na heroini na kilo 1,800 za mirungi zimekamatwa,” alisema.

Ntibenda alisema watu 180 walikamatwa kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na 160 kati yao wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.

“Kwa ujumla mkoa wa Arusha sasa ni salama. Napenda kuvipongeza vyombo vya usalama kwa kazi nzuri wanayofanya,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema baadhi ya wananchi waliosalimisha silaha hizo walikutwa na bunduki za kivita aina ya K47 na SMG zisizoruhusiwa kumilikiwa na raia.

Alisema wapo baadhi ambao silaha zao zilikuwa zikimilikiwa kihalali lakini walishindwa kutoa maelezo yanayoridhisha ya mahali walikopata risasi za ziada baada ya 30 za awali kwisha ambazo hutolewa kisheria.

Alisema wanaendelea kuzishikilia silaha hizo na baada ya uchunguzi wanaweza kuwarudishia wanaozimiliki kihalali.
Kuna tetesi kuwa utapewa tunzo ni kweli?.....
 
wewe vipi! kwani mbunge kazi yake ni kukamata silaha haramu? kwa nini husemi ufanisi umechangiwa na mbunge badala umechagua kumponda...wacha roho mbaya bana.
 
Mbunge anaingiaje hapo? Maswala ya ulinzi na usalama kweli yako katika TOR za mbunge?
 
Kacopy na kupaste halafu anataka kuilazimishia iwe scandal kwa mbunge wa ngorongoro.

Ndio kizazi kipya cha bavicha hiki...!
Nyumbu ni nyumbu tu, yaani nyumbu Serengeti hana tofauti na wa mikumi au tarangire
 
Vyombo vya usalama mkoani Arusha, vinazishikilia bunduki 103 zikiwamo za kijeshi wilayani Ngorongoro sambamba na magunia 270 ya bangi wilayani Arumeru.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda alitoa taarifa hiyo juzi katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na kusema; “Arusha sasa ni shwari.”

Alisema ndani ya wiki mbili tu, silaha hizo 103 zimesalimishwa wilayani Ngorongoro na zipo mikononi mwa polisi kutokana na agizo la Serikali kuwataka wananchi wazisalimishe.

Alisema katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana, jumla ya magunia 270 ya bangi yalikamatwa wilayani Arumeru na ekari 25 za mashamba yake ziliteketezwa.

Ntibenda alisema magunia hayo ya bangi na mashamba yake yamebainika katika operesheni dhidi ya kilimo cha bangi iliyofanyika katika vijiji vya Kisimiri Juu, Ibimbwa, Ngarenanyuki na Oldonyosambu.

“Katika kipindi hicho pia, katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha, jumla ya kilo tatu za dawa za kulevya; cocaine na heroini na kilo 1,800 za mirungi zimekamatwa,” alisema.

Ntibenda alisema watu 180 walikamatwa kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na 160 kati yao wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.

“Kwa ujumla mkoa wa Arusha sasa ni salama. Napenda kuvipongeza vyombo vya usalama kwa kazi nzuri wanayofanya,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema baadhi ya wananchi waliosalimisha silaha hizo walikutwa na bunduki za kivita aina ya K47 na SMG zisizoruhusiwa kumilikiwa na raia.

Alisema wapo baadhi ambao silaha zao zilikuwa zikimilikiwa kihalali lakini walishindwa kutoa maelezo yanayoridhisha ya mahali walikopata risasi za ziada baada ya 30 za awali kwisha ambazo hutolewa kisheria.

Alisema wanaendelea kuzishikilia silaha hizo na baada ya uchunguzi wanaweza kuwarudishia wanaozimiliki kihalali.
Wewe endelea kuzungusha mikono wakati train ishashika kasi
 
Back
Top Bottom