Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola aionya Jamhuri kumsotesha Mahakamani

MUGASHA THE HERO

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
327
204
Kangi Lugala, Mbunge wa Mwibara ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa onyo kwa Jamhuri kwa kukwamisha kuwasomea maelezo ya awali katika kesi inayowakabili.

Lugola, Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Lupa na Murad Sadiq, Mbunge wa Mvomero wanatuhumiwa kuomba rushwa ya Sh. 30 mil kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Gairo tarehe 15 Machi mwaka huu.

Lugola alitoa madai hayo jana mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo baada ya wakili wa serikali Denis Lekayo kueleza kuwa, waendesha mashtaka wa kesi hiyo hawapo.

Wakili Lekayo alidai kuwa, shauri hilo liliitishwa kwa ajili maelezo ya awali lakini waendesha mashtaka hawakupo.

Kutokana na maelezo hayo Lugola aliiomba mahakama ikemee tabia hiyo ya kuahirishwa kesi mara kwa mara.

Lugola alisema kitendo hicho kinawanyima haki yao ya msingi ya kufanya shughuli zao za Bunge.

Baada ya Lugola kueleza hayo, wakili wa Serikali, Denis Lekayo aliiomba mahakama radhi na kusema ‘tutafanya haraka kesi iendelee.’

Hakimu Simba alisema, kauli iliyotolea na mshitakiwa ni ya msingi. Baada ya kueleza hayo aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 12 Julai mwaka huu kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

Chanzo: Mpekuzi
 
Huu Ujasiri wa Mshtakiwa kudai Mashtaka unatoka wapi?isije kuwa hizi kesi zilizofunguliwa haraka haraka kipindi kile ni kesi za kutuaminisha hapa kasi tu na kulizima bunge kama tulivyoona,ilihali Waendesha mashtaka hawana ushahidi wa kutosha,Serikali ikishindwa hii kesi ijichukulie hatua yenyewe na kujitathmini Upya.

Anyway Muhudumu naomba niletee Shisha nyingine mengine hayana msingi kwangu.
 
Pamoja na mapambano makali dhidi ya rushwa na mahakama ya mafisadi, Mshitaki haonekani?????....hizi ni dalili za kusafishwa
 
Duuu mleta uzi Umetisha!
Swali:Hivi shisha ndio "hooker" ama ndio nini?
I mean shisha ni kitu gani?
 
Huu Ujasiri wa Mshtakiwa kudai Mashtaka unatoka wapi?isije kuwa hizi kesi zilizofunguliwa haraka haraka kipindi kile ni kesi za kutuaminisha hapa kasi tu na kulizima bunge kama tulivyoona,ilihali Waendesha mashtaka hawana ushahidi wa kutosha,Serikali ikishindwa hii kesi ijichukulie hatua yenyewe na kujitathmini Upya.

Anyway Muhudumu naomba niletee Shisha nyingine mengine hayana msingi kwangu.
Nakuhakikishia hakuna kesi hapo, PCCB walikurupuka ili kumlizisha bosi wao
 
Huu Ujasiri wa Mshtakiwa kudai Mashtaka unatoka wapi?isije kuwa hizi kesi zilizofunguliwa haraka haraka kipindi kile ni kesi za kutuaminisha hapa kasi tu na kulizima bunge kama tulivyoona,ilihali Waendesha mashtaka hawana ushahidi wa kutosha,Serikali ikishindwa hii kesi ijichukulie hatua yenyewe na kujitathmini Upya.

Anyway Muhudumu naomba niletee Shisha nyingine mengine hayana msingi kwangu.
Kwani upendo sanaa ya maigizo?
 
Ni haki ya mshtakuwa kwa mujibu wa sheria
 
Naona hawa jamaa hawakumuelewa muheshimiwa. Inatakiwa wamalizane nao haraka haraka na siyo mikesi kesi hiii.
 
Kangi Lugala, Mbunge wa Mwibara ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa onyo kwa Jamhuri kwa kukwamisha kuwasomea maelezo ya awali katika kesi inayowakabili.

Lugola, Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Lupa na Murad Sadiq, Mbunge wa Mvomero wanatuhumiwa kuomba rushwa ya Sh. 30 mil kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Gairo tarehe 15 Machi mwaka huu.

Lugola alitoa madai hayo jana mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo baada ya wakili wa serikali Denis Lekayo kueleza kuwa, waendesha mashtaka wa kesi hiyo hawapo.

Wakili Lekayo alidai kuwa, shauri hilo liliitishwa kwa ajili maelezo ya awali lakini waendesha mashtaka hawakupo.

Kutokana na maelezo hayo Lugola aliiomba mahakama ikemee tabia hiyo ya kuahirishwa kesi mara kwa mara.

Lugola alisema kitendo hicho kinawanyima haki yao ya msingi ya kufanya shughuli zao za Bunge.

Baada ya Lugola kueleza hayo, wakili wa Serikali, Denis Lekayo aliiomba mahakama radhi na kusema ‘tutafanya haraka kesi iendelee.’

Hakimu Simba alisema, kauli iliyotolea na mshitakiwa ni ya msingi. Baada ya kueleza hayo aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 12 Julai mwaka huu kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

Chanzo: Mpekuzi
Hivi huyo lugola hajisikii ganzi?shughuli gani za bunge anasema?kulilia maslahi yao ndiyo shughuli?
 
Huu Ujasiri wa Mshtakiwa kudai Mashtaka unatoka wapi?isije kuwa hizi kesi zilizofunguliwa haraka haraka kipindi kile ni kesi za kutuaminisha hapa kasi tu na kulizima bunge kama tulivyoona,ilihali Waendesha mashtaka hawana ushahidi wa kutosha,Serikali ikishindwa hii kesi ijichukulie hatua yenyewe na kujitathmini Upya.

Anyway Muhudumu naomba niletee Shisha nyingine mengine hayana msingi kwangu.
Teh teh shisha nyingine wew mkuu wewe unataka kumchokoza Majaliwa nini.
 
Back
Top Bottom