BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,845
Niliwahi kusikia kwamba Kigoda alipokuwa Waziri katika sirikali ya Mkapa alikuwa akipita nchi mbali mbali za magharibi kutafuta makampuni ya uchimbaji wa dhahabu yaingie mkataba na yeye na Mkapa wa kuchimba dhahabu katika "mgodi wao wa dhahabu". Isije ikawa huu wa Buhemba ndio mgodi "wao"
Posted Date::4/12/2008
Mbunge wa Musoma kuwasha moto kuhusu milki ya mgodi wa Buhemba
* CAG akiri, asema si mgodi wa serikali
* Waziri Ngeleja asema apatiwe muda
Na Mkinga Mkinga
Mwananchi
SUALA la umiliki wa mgodi wa dhahabu wa Buhemba mkoani Mara, limechukua sura mpya, baada ya Mbunge wa Musoma vijijini, Nimrod Mkono kuamua kupeleka bungeni hoja binafsi kupata maelezo ya kina, kuhusu nani anayemiliki mgodi huo.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalum, Mkono alisema atahitaji kupata maelezo yanayojitosheleza hasa baada ya kuonekana, serikali si mmiliki wa mgodi wa Buhemba kutokana na maelezo ya Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), na msajili wa asasi za serikali.
Mkono alisema amekuwa akiipeleka hoja hiyo bungeni mara kadhaa, lakini imekuwa ikikosa mtu wa kutoa ufafanuzi wa nani mmiliki wa mgodi huo, ambao ulikuwa chini ya Kampuni ya Meremeta, kampuni ambayo imekuwa ikipigiwa kelele na wapinzani katika masuala ya ufisadi.
Majuzi hapa wakati wa mkutano wa asasi zote, CAG ameulizwa kuhusu Buhemba, akasema hajapata taarifa zozote za mgodi huo wala hajawahi kupitia hesabu zake, na wala hajui kama ni mgodi wa serikali, alisema Mkono.
Mbunge huyo alisema kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na utata wa umiliki wa mgodi huo wa Buhemba, huku taarifa za awali zikionyesha kuwa mgodi huo ulikuwa unamilikiwa na Kampuni ya Meremeta, ambayo inamilikiwa na serikali.
Wananchi pamoja na mimi tumekuwa tukiambiwa kuwa mgodi huo ni wa serikali, lakini kwa mujibu wa CAG, pamoja na msajili wa asasi za umma walisema, kampuni hiyo haimo katika orodha ya makampuni ya asasi za umma kama ilivyokuwa inasemekana, alisema Mkono.
Ninachotaka kusema ni kwamba hapa lengo sio majungu, ila kama Mbunge wa Musoma Vijijini ambako mgodi huo upo anahitaji kujua, ili wananchi wangu pia niwafahamishe kuhusu umiliki halali wa mgodi huo, alisema Mkono.
Alisema utata huo wa umiliki wa mgodi wa Buhemba, umezidi kuwa mkubwa ambapo sio yeye wala wananchi ambao walifahamishwa kuwa mgodi huo ulikuwa unamilikiwa na nani.
Mkono aliongeza kuwa, kitendo cha kuchimba madini ya dhahabu yaliyokuwa yanapatikana katika mgodi huo, kwa kutumia jina la serikali, ni sawa na kuisaliti nchi na kuiba maliasili zake.
Mbunge huyo wa Musoma Vijijini alisema, mabilioni ya fedha yametumika katika kuimarisha mgodi huo, hata baada ya kuanza uzalishaji wa dhahabu si serikali wala wananchi ambao wamefaidika na uchimbaji madini huo.
Mabilioni ya shilingi hapa yametafunwa, huu ni ufisadi, maana kama hizo za EPA zimeundiwa task force committee kwa nini hapa pia pasiundiwe tume, alisema Mkono.
Kwa mujibu wa mbunge huyo inakadiriwa kuwa zaidi ya Sh 180 bilioni zimetafunwa kupitia mgodi huo, fedha ambazo zingeweza kuwafaidisha wananchi katika mambo mengine ya maendeleo.
Alisema kinachoendelea kushangaza wananchi wa jimbo lake ni kwamba, mpaka sasa askari wa jeshi la polisi bado wanaendelea kulinda katika eneo hilo la Mgodi wa Buhemba, wakati imefahamika kwamba serikali si mmiliki wa mgodi huo.
Katika hatua nyingine, Mkono alisema amefikisha malalamiko yake katika Tume ya Rais ya kupitia upya mikataba ya madini iliyoko chini ya Jaji mstaafu Mark Bomani na kwamba sasa anasubiri utekelezaji.
Wakati kamati ya Rais inayoshughulikia madini ilipotembelea mgodi huo, niliwaambia masuala kadhaa yenye utata hapo Buhemba, bila shaka watayafikisha kunakohusika, alisema mbunge huyo.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Heasbu za Serikali, Ludovick Utouh, alipoulizwa na Mwananchi Jumapili jana, alisema ni kweli kwamba katika orodha ya makampuni ya umma 158, kampuni iliyotajwa kumiliki mgodi huo si miongoni mwa makapuni ya umma.
Ninachokifahamu na nilichomueleza Mbunge wa Musoma vijijini, Nimrod Mkono ni kwamba katika orodha ya makampuni 158, ninayoyakagua hilo halimo, alisema CAG.
CAG alitaka maswali zaidi yaelekezwe kwa msajili aliyeko hazina, kwa madai kuwa anaweza kuwa na majibu mazuri zaidi ya hilo, na kwamba yeye ndiye mwenye mamlaka na asasi za serikali.
Naye Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja alipotakiwa kutoa ufafanuzi wake jana na msimamo wa serikali katika utata uliogubika mgodi wa Buhemba alisema jambo hilo linahitaji takwimu zaidi.
Jambo hili linahitaji takwimu zaidi halafu mimi sipo ofisini, tafadhali hebu wasilianeni na Kamishna wa Madini, atakuwa anafahamu zaidi, alisema waziri Ngeleja.
Aliongeza kuwa suala hilo linahitaji kujiandaa zaidi na kwamba yeye atamuagiza kamishna huyo wa madini atoe ufafanuzi kwa gazeti hili.
Suala la utata wa mgodi wa Buhemba limedumu kwa muda mrefu sasa, takribani miaka mitano, na kwamba mwishoni mwa mwaka jana wapinzani waliinyoshea kidole serikali kuhusu umiliki wake wa mgodi huo.
Mgongano huo pia, ulisababisha Mbunge wa Musoma vijijini, Nimrod Mkono kukataa kupokea kiasi cha sh 200 milioni kama mrabaha kwa wilaya hiyo, kwa madai kuwa haikuwa inaendana na kile kinachovunwa katika ardhi hiyo. Juhudi za Kumtafuta Kamisha wa Madini jana hazikuzaa matunda.