Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 5,703
- 15,156
Mbunge wa Muleba kusini Prof Anna Tibaijuka leo tarehe 3, April 2020 wakati akichangia bajeti ya Waziri Mkuu ameliaga Bunge na kutangaza rasmi kuwa hatagombea tena ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Prof. Tibaijuka ameliaga Bunge kwa kilio cha kuhukumiwa bila kusikilizwa kwenye sakata la Tegeta Escrow ,amesema hali hiyo ilimuumiza sana na ameacha andiko lake kwa Waziri Jenista Mhagama akilitaka bunge lifanye mabadiliko ya kusikiliza kwanza watuhumiwa kabla ya kuwahukumu.
Prof. Tibaijuka amesema baada ya kustaafu rasmi ubunge sasa anaenda kuwa mwandishi wa vitabu ili ayaweke kwenye kumbukumbu yote mengi aliyojifunza kwenye safari yake ya utumishi.
My take
Na wabunge wengine waliokaa muda mrefu bungeni kama akina Mbowe ni vizuri wakaiga mfano wa Prof Anne Tibaijuka wa kustaafu kwa hiari na kuachia wengine siyo kusubiri mpaka uzomewe jimboni na wananchi kwamba wamekuchoka ondoka.