Mbunge wa Mtwara Mjini akamatwa kwa uchochezi!

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnein Murji ametiwa mbaroni na Jeshi La Polisi kwa tuhuma za uchochezi na kuhusika katika vurugu zilizotokea hivi karibuni katika viunga vya mji wa Mtwara.

Habari za kuthibitika zinaeleza kwamba mbunge huyo amekamatwa saa 2:30 jioni hii naanashikiliwa katika kituo Kikuu cha Polisi
Mjini Mtwara.

Katibu wa Mbunge huyo Meckland Millanzi amethibitisha kukamatwa kwa Murji na kwamba anahusishwa na mvurugu hizo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Advera Senso amesema kwamba Murji amekamatwa hivi punde nyumbani kwake
katika eneo la Shangani.

Taarifa zimebainisha kwamba Murji amekamatwa na kwamba hati ya kumkamata imeeleza anatuhumiwa kuchochea vurugu za kupinga gesi ya Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam.

Siku chache zilizopita zilizuka vurugu kubwa katika mji wa Mtwara na viunga vyake baada ya wananchi wa mji huo kuandamana baada ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kusomwa na Waziri wa wizara hiyo kueleza msimamo wa serikali kwamba mpango wa kusafirisha gesi jijini Dar es Salaam uko pale pale.

Awali kabla ya vurugu hizo kutokea shughuli mbalimbali za kijamii zilisimama huku watu wasiofahamika kusambaza vipeperushi kuhamasisha kusimama kwa shughuli hizo.

Kutokana na vurugu hizo baadhi ya watu walipoteza maisha, nyumba kuchomwa moto na madaraja kuharibiwa vibaya.

Mpaka sasa watu zaidi ya 80 wamekamatwa na jeshi la polisi na kushtakiwa mahakamani.
 

Attachments

  • 1178.jpg
    1178.jpg
    19.4 KB · Views: 1,514
Sakata bado halijaisha.?
Juzi jk kaongea akiwa Japan kuwa gesi lazima itoke Mtwara, kumbe ishu bado mbichi kabisa.!!

Labda itakua ndio mapembe alioyosema jk.!
 
Ni kweli

Mbunge wa Mtwara
Mjini, Hasnein Murji ametiwa mbaroni na
Jeshi La Polisi kwa tuhuma za uchochezi na
kuhusika katika vurugu zilizotokea hivi
karibuni katika viunga vya mji wa Mtwara.
Habari za kuthibitika
zinaeleza kwamba mbunge huyo
amekamatwa saa 2:30 jioni hii na
anashikiliwa katika kituo Kikuu cha Polisi
Mjini Mtwara.
Katibu wa Mbunge huyo Meckland Millanzi
amethibitisha kukamatwa kwa Murji na
kwamba anahusishwa na mvurugu hizo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Advera
Senso amesema kwamba Murji
amekamatwa hivi punde nyumbani kwake
katika eneo la Shangani.
Taarifa zimebainisha kwamba Murji
amekamatwa na kwamba hati ya
kumkamata imeeleza anatuhumiwa
kuchochea vurugu za kupinga gesi ya
Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam.
Siku chache zilizopita zilizuka vurugu
kubwa katika mji wa Mtwara na viunga
vyake baada ya wananchi wa mji huo
kuandamana baada ya bajeti ya Wizara ya
Nishati na Madini kusomwa na Waziri wa
wizara hiyo kueleza msimamo wa serikali
kwamba mpango wa kusafirisha gesi jijini
Dar es Salaam uko pale pale.
Awali kabla ya vurugu hizo kutokea
shughuli mbalimbali za kijamii zilisimama
huku watu wasiofahamika kusambaza
vipeperushi kuhamasisha kusimama kwa
shughuli hizo.
Kutokana na vurugu hizo baadhi ya watu
walipoteza maisha, nyumba kuchomwa
moto na madaraja kuharibiwa vibaya.
Mpaka sasa watu zaidi ya 80
wamekamatwa na jeshi la polisi na
kushtakiwa mahakamani.
 
Mbunge wa Mtwara mjini Hasnein Murji amekamatwa na jeshi la polisi kwa uchochezi na kuhusika katika vurugu zilizotokea hivi majuzi katika viunga vya mji wa mtwara na maeneo jirani.

Habari zilizo patikana hivi punde zinaeleza kwamba mbunge huyo amekamatwa usiku huu saa 8:30 akuwa nyumbani kwake katika eneo la shangani na anashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi mjini mtwara

Piga Risasi tupa kule huyo Panya!

 
Hapa nahisi kuna viongozi wakubwa wa upinzani wanafuatia!hii ni kuonyesha kua mbona hata wa ccm wameshikwa na hivyo kupunguza malalamiko.lets wait!
 
Ningeshaa sana serikali isingekamata huyu jamaa, it was very clear kwamba alikuwa hajihusishi kabisa kutuliza ghasia... wathungu wanasema "Either you are with us or...".

Jeshi la polisi fanyeni kazi zenu kwa utaalamu bila kujali chama, kudos.
 
Panya wakikamatana panya wanatazamana!

Nahisi ulitaka kumaanisha paka, otherwise sijakuelewa.

MM, Sikio la kufa huwa halisikii dawa, CCM sasa hivi watakuwa wanafanya vitu vya ajabu ajabu tu, kama wajenzi wa mnara kule baberi walivyochanganyikiwa.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom