Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Mbunge wa Moshi Mjini (CHADEMA), Mh. Jaffary Michael katika Waraka wake alioutoa Jana kwa umma, alisema kuwa, kinachofanya kiongozi aonekane bora kuliko mwingine ni uadilifu, usminifu, uthabiti na uimara katika kusimamia kodi za wananchi na rasilimali nyingine ili ziwaletee wananchi maendeleo. Mbunge huyo ambayo ni Waziri Kivuli wa Wizara ya TAMISEMI, Kambi Rasmi ya Upinzani alieleza kuwa, ubora wa Rais, pamoja na Wabunge na Madiwani, utapimwa kwa jinsi walivyoweza kusimamia kodi ya wananchi kuleta maendeleo kwenye maeneo yao ya uwakilishi.
Jaffary aliwaasa wananchi kuwa wakati wa uchaguzi, wapime uaminifu wa viongozi wao katika kusimamia kodi zao na baada ya kuwachagua wapime ubora wao kwa jinsi wanavyoweza kusimamia rasilimali za wananchi katika kuleta maendeleo.
Sasa kama hata Wabunge wa upinzani wanalielewa hili, mbona Uongozi wa CHADEMA unawadhihaki wananchi? Hivi kweli ilikuwa busara kwa CHADEMA kutoa taarifa ya Chama chao kupinga suala la Makinikia? Je walitaka kutuambia nini umma, kwamba kwa sababu Serikali ya CCM haijawashirikisha vyema basi ni bora Taifa lishindwe kwenye majadiliano?
Kosa ambalo CHADEMA walilifanya juzi, ni sawa na kosa linalofanywa na mvulana kumtongoza msichana, siku ambayo amefiwa na mtu muhimu kwake, hapo unategemea nini?