The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 617
- 1,797
Leo Jumanne, tarehe 30 Machi, 2021, Mbunge wa Jimbo la Mlimba mkoani Morogoro, Godwin Kunambi ametoa mapendekezo ya kujenga monument ya kuenzi kazi iliyofanywa na rais Magufuli.
Akichangia hoja Bungeni, Kunambi amesema:
Kazi kubwa ambayo mimi naomba nishauri Bunge letu tukufu ni... amefanya mambo makubwa ndani ya nchi na kukumbukwa kwake itakuwa ni jambo la msingi sana.
Ukienda South Africa pale Johannesburg, utaona kuna mnara pale lakini pia kuna sanamu zuri sana ya Mandela, wanaita Mandela Square.
Kwa kazi kubwa aliyoifanya kuhamisha makao makuu yetu ya nchi kuja Dodoma; hapa Dodoma kuna eneo tengwa la serikali; lina hati miliki maeneo ya Chimwaga. Na Chimwaga tunaifahamu kihistoria — zaidi ya heka 100 zimetengwa pale kwa ajili ya recreational park, eneo la mapumziko.
Niombe kushauri Serikali; ingefaa tujenge monument pale. Tujenge monument ambayo wajukuu, watoto na kizazi kijacho kitakuwa kinasema, "Magufuli ni nani?"— wanakwenda pale.
Na hii itasaidia kumjengea heshima kubwa kwa aliyotutendea Watanzania.