Mbunge wa Mbogwe amtaka Naibu Waziri wa Maji kuacha majibu ya kwenye makaratasi, ahoji vilipo visima 26 alivyotaja

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Mbogwe, Nicodemus Maganga amemtaka Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi kutofuata mambo ya kwenye makaratasi, na kufuatana naye ili akamuoneshe visima 26 ambavyo amesema vipo.

Katika swali lake, Mbunge huyo alihoji Serikali ina mpango gani wa kupeleka maji ya Ziwa Victoria katika Jimbo hilo kwa ajili ya matumizi ya wananchi.

Akimjibu, Naibu Waziri alisema hali ya upatikanaji maji ni wastani wa 55% na huduma inapatikana kupitia miradi minne ya skimu, visima virefu 26, visima vifupi 460 na matenki 50 ya kuvuna maji ya mvua nk.

Hata hivyo, Mbunge huyo hakuridhishwa na majibu yake akisema, "Tuongozane naye akanionyeshe pale vilipo. Mimi ni Mbunge wa Mbogwe na ninaishi Mbogwe, kuna tabu sana katika sekta ya maji".
 
Dodoma, Mbunge wa Mbogwe (CCM), Nicodemus Maganga ameyakataa majibu ya Serikali bungeni kuwa katika jimbo hilo wananchi wanapata maji na kuhoji vilipo visima 26 vya maji.

Akizungumza bungeni leo Jumatano Aprili 14, 2021 mbunge huyo amesema hakuna visima vya maji katika jimbo lake na wananchi wanaendelea kuteseka kwa kukosa maji wakati wote.

Akijibu swali la msingi la mbunge huyo, naibu waziri wa maji, Maryprisca Mahundi amesema katika jitihada za kutatua tatizo la maji, Serikali ilichimba visima virefu jimboni humo na vinatumika hadi sasa.

"Sijaridhishwa na majibu ya Serikali hivyo visima vimechimbwa wapi? Mimi ni mbunge wa Mbogwe na ninaishi huko lakini sijawahi kuona hayo maji naomba kujua visima viko wapi," amehoji Maganga.

Mbunge huyo amesema majibu ya naibu waziri ni ya kwenye makaratasi aliyoandikiwa kwa kudanganywa na kumuomba aende kwenye jimbo hilo akajionee mwenyewe ombi ambalo lilikubaliwa na naibu waziri huyo.
 
Huyo mbunge kajuvua tabia za kiharamia za ndiyo ndiyo ukijua kabisa kuwa waziri anadanganya.
 
Mbunge unapokea 11M kwa mwezi plus other benefits. Kima cha chini kwa serikali ni 300K hivi tuseme anashindwa kutoa pesa ya mshahara akachimba hata visima vinne tu?

Mbunge anaamini akihoji kama hivyo basi kamaliza hajui serikali za dunia ya tatu hua zina matatizo mengi ya kifedha ndiyo maana bajeti haijawahi kutosha.

Hawa wabunge no wonder utaona wanaomba kujengewa mpaka vyoo. Vyoo.

Wanatia aibu na wapo wengi kweli kweli.
 
Safi sana jembe la mbogwe pia jamaa ni chimbuko la chadema baada ya kupigwa chini 2015 akaona angie upande wa kijani

Ila bado anajitambua hawajaweza kumtoa ufahamu kama ndugu zetu walionunuliwa kwa vunj bei
 
water-shortage-by-women.jpg

Visima vya Magufuli si hivi hapa na tunachosubiri ni Ndege mpya tatu za kuwakomesha Chadema.
 
Back
Top Bottom