Mbunge wa Mbeya Mjini kuputia Chadema Sugu Aja na Kampeni ya Vyoo Mashuleni

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi 'Sugu' amekuja na kampeni ya kuhakikisha tatizo la vyoo vya mashule katika jimbo hilo ambalo ni ubovu na ukosefu wa vyoo unapunguzwa na baadaye unamalizwa ambapo ameanza kampeni hiyo kwa kuhakikisha anaongeza nguvu katika kusaidia ujenzi wa vyoo hivyo katika baadhi ya shule zilizopo katika jimbo hilo kupitia kupitia Mfuko wa maendeleo ya Jimbo, Ofisi ya Mbunge na wadau wa maendeleo huku akisisitiza kwa shule kongwe ni vyema nguvu za waliosoma shule husika zikusanywe ili kusaidia tatizo hilo.

Katika kutekeleza Kampeni hiyo Alhamisi tarehe 22 Novemba, 2018 ameendelea na ziara ya kutembelea shule mbalimbali kwa lengo la kukagua hali ya vyoo pamoja na maendeleo ya ujenzi wa vyoo kwenye maeneo aliyoyasaidia kupitia Mfuko wa Jimbo, ziara hiyo pia ililenga kukagua shule ambazo wanatarajia kuzisaidia kutekeleza ujenzi huo.

Mbunge huyo ameweza kuzitembelea shule kadhaa ikiwemo Shule ya Msingi Kalobe (Kata ya Kalobe), Shule ya Msingi Mabatini (Kata ya Mabatini), Shule ya Sekondari Itiji (Kata ya Itiji), Shule ya Msingi Iziwa (Kata ya Iziwa) Shule ya Sekondari Mwansekwa (Kata ya Mwansekwa), Shule ya Msingi Sinde (Kata ya Sinde), Shule ya Msingi Hayanga (Kata ya Isyesye), Shule za Msingi Nero na Mapambano (Kata ya Iyela) na Shule ya Msingi Muungano iliyopo Kata ya Forest.

Akifafanua katika ziara hiyo Mbunge Mbilinyi amesikitishwa na hali ya vyoo katika mashule mbalimbali aliyotembelea na kuiasa jamii na wadau wa maendeleo kusaidia katika suala zima la ujenzi wa vyoo ambapo amepongeza juhudi zinazoendelea za utatuzi wa tatizo hilo kupitia wananchi wakiwemo wadau mbalimbali ambapo ameahidi kuongeza nguvu kwa kuchangia jitihada hizo ili kuhakikisha mazingira ya vyoo ambayo ni muhimu sana katika kuwaweka Wanafunzi katika mazingira salama ya kujifunza kutokana na ukweli kwamba tatizo la choo kwenye shule linapunguza hari ya wanafunzi kupenda mazingira ya shule na hivyo kupelekea hata kushuka kwa ufaulu wa watoto mashuleni.

Mbunge huyo wa Mbeya Mjini amesema atatoa ripoti ya ziara hiyo ikiwa ni pamoja na kuelezea hali halisi ya alichokiona katika shule hizo pamoja na kuelezea fedha walizotoa awali na mpaka sasa na wanazotarajia kutoa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ili kupunguza tatizo hilo la ubovu na ukosefu wa vyoo mashuleni na miradi ya maendeleo kwa ukumla, aidha Mbunge amesisitiza kuwa utoaji wa taarifa za miradi ya maendeleo kwa wananchi ikiwemo miradi ya mfuko wa jimbo umekuwa ni utamaduni wa kawaida kwake tangu aliposhika nafasi hiyo ya uwakilishi wa jimbo hilo la Mbeya Mjini.
IMG-20181123-WA0039.jpg
IMG-20181123-WA0040.jpg
 
Ameamua ajikite chooni..ameshaona kupambana na utawala huu ni kazi sana..utaishia kila siku kutembea na namba za mfungwa..sio jk leadership hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom